Ulishawahi kuwa na mwanamke anayekutawala?

Ulishawahi kuwa na mwanamke anayekutawala?

Codrix

Senior Member
Joined
May 18, 2019
Posts
192
Reaction score
219
Wakuu habari za asubuhi.

Binafsi niko na mwanamke anayenitawala.

1.Kila kitu changu anataka kuelewa kinaanzaje na kinaishaje, hataki nifanye jambo lolote kama hajajua, endapo asipojua anaita kwamba nimemdharau.

2.Simu yangu hata kama nina maongezi na mzazi atasema kuwa mbona ninaongea muda mrefu, labda itakuwa ni wanawake, hawezi kuelewa kwa haraka, labda umtumie screenshot ya uliyekuwa unaongea naye.

3.Ratiba anataka ziende alivyozipanga yeye, akisema twende ni twende, ukisema una kazi fulani kwa muda huo, tayari huo ni ugomvi wa siku nzima, hapo nitaitwa nina dharau, namchukulia poa nk....

4.Akipiga simu ni lazima umuambie uko wapi na unafanya nini na kama akiona ana mashaka na unachosema ni lazima umuaminishe kwa kumtumia picha ya unachokifanya, au atapiga video call.


4.Kuna kipindi hakutaka ninunue simu janja, kwa mantiki ya kwamba nitakuwa naingia mitandao mbalimbali, instagram, jf whatsapp nk...

5.Muda wa kazi nikiwa nafanya kazi fulani, lazima atauliza namaliza saa ngapi nikivukisha muda ni kosa, utasikia anasema maisha mema, unajifanya upo busy

Declaration of interest, Mimi sio kibenten yeye ni mwanachuo na mimi nina harakati zangu

Nipo nipo tu namsikilizia kwa sababu napata free p kupoteza muda kwa maana siwezi kuingia katika ndoa na mwanamke anayenitawala.

nipe experience yako.
 
Kama huwa unampa hela,anaigiza tu ili ujue kwamba anakupenda,wanawake wenye wivu ni wachepukaji wazuri tu,nina experience nao
Huwa simpi hela yoyote, yaani kuniendesha kote huko nimpe na hela?

Namsikilizia tu kwa ajili ya free p huku nafanya mambo yangu, ni sehemu ya kupumzishia tu hamu.

Nikipata option napiga chini
 
unaposema unapata p ya bure, gharama zake ndo hizo za kukutawala..........huna haja ya kupotezeana muda...najua unampa nae anakupa.....kama hupendi hizo mambo mwambie...kuna magonjwa blaza.....
Kweli mkuu gharama nayolipia ni kutawaliwa, soon nikimpata afaaye naachia ngazi, nashika kwingine.
 
Huwa simpi hela yoyote, yaani kuniendesha kote huko nimpe na hela?

Namsikilizia tu kwa ajili ya free p huku nafanya mambo yangu, ni sehemu ya kupumzishia tu hamu.

Nikipata option napiga chini
Aaah,kama hugaramiki komaa jomba yaweza kuwa anakupenda sana
 
Kuna wivu wa aina mbili
1. Wivu wa Upendo wa kweli na
2. Wivu wa kujilinda ili asijulikane kama ni malaya.

Wengi huangukia namba mbili hapo.
Ni taabu tupu.
Kweli mkuu halafu nikifanya vetting naona anaangukia namba mbili
 
Hongera kwa ung'amua mapema kuwa 'msaidizi wako' anatarajia kuwa 'kichwa'
 
Aaah,kama hugaramiki komaa jomba yaweza kuwa anakupenda sana
Hilo la kupendwa sana sio kigezo cha kuendeshwa, kuna mengi anafanya sema ni ngumu kuelezea
 
Haina haja kuumiza kichwa kama mpo mnapotezeana muda for flesh desire mkuu. maisha n kuchagua.
 
Kuwa makini na unayemsimulia haya ndugu kuna watakaokuona kama wewe ndiyo binti & yeye ndiye mvaa suruali kwenye hayo mahusiano
 
Bora huyo anayekuonyesha makucha yake mkiwa kwenye uchumba hivyo una nafasi ya kumbadilisha kabla hamjaingia kwenye ndoa

Kuliko upate mwanamke mpole kumbe anakuigizia tu ili umuoe halafu ukishamuoa ndo anaanza kuonyesha makucha yake utajuta
Sidhani kama anabadilishika, ndivyo alivyo.
 
Back
Top Bottom