Ulishawahi kusingiziwa kitu?

Mimi nilikuwa nimemaliza chuo, kutokana na ukosefu wa ajira nikawa nimejiajiri kwa kukodi stationary ya jamaa flani na internet cafe kwa makubariano nitakuwa nampa kiasi flani cha fedha kila siku.
Sasa pale alikuwa anakuja mama flani hivi wa kitanga kipini puani vikuku miguuni.
Akawa anajaza online forms flani akisubmit zinagoma, kila siku akawa anakuja kumbe anashindwa.
Siku moja akaniuliza tatizo ni nini, kumbe alikuwa hajazi kama inavyotakiwa nikamsaidia akafanikuwa submit.
Tulipomaliza tukapuga story mbili tatu akachukua namba yangu.
Usiku akanitxt umelala, mimi na heshima zote nikamjibu sijalala mama. Akauliza tunaweza kuchat au uko na wifi asije kasirika, na heshima debe nikamjibu sijaoa bado niko peke yangu mama.
Tukachat chat mimi kila sms namalizia na mama.
Akawa anakuja pale hakatiki mara aniletee hiki nara aniletee kile, alikuwa anafanya kazi NGO flani, mara aje aache gari lake pale ofisini kwangu, mara aniwekeshe ela ambayo kipindi hicho sikuwahi miliki.
Kumbe bwana watu wakaanza sema natembea naye, yani frem za jirani wote wanadai natembea naye, pia alikuwa na mwanaume anaishi naye kazaa naye watoto wawili ila anamlea maana jamaa mdogo na hana kazi naye habari zikamfikia.
Mimi sina habari wala hata wazo naona huyo mmama ananikubari sana na ana roho nzuri kweli.
Kuna jamaa yangu ndiye alikuja nizindua usingizini kuwa huyo mama ananitega na ataniletea matatizo.
Pia akaniambia watu wote wanasema ninamtafuna.
Hapo ndipo nilianza reflect mambo yake nikajiona kweli nilikuwa usingizini yani hata kushtuka kama ananitega sikuwa nimeshtuka.
Nikaanza mpotezea alikuwa anasumbua nikamwambia mazoea yapungue akauliza shida nini nikamwambia watu wanasema natembea naye, eti akauliza kwani shida iko wapi nkitembea naye...
Ni mambo mengi yalitokea ila mpaka leo kuna watu hawaamini kuwa sikuwahi tembea na huyo mama
 
Daah bora mwenye mali hakukufanyia mbaya maana!!
 
Daah bora mwenye mali hakukufanyia mbaya maana!!
Kuna siku akanipeleka kwake nimrekebishie DSTV, mara mwenye mali kaja ameliwa nikamsalimia hakuituka akapitiliza mpaka chumbani mimi nikadhani labda ulevi.
Sema mwenye mali alikuja gundua mimi mtu poa baada ya siku moja kuiba simu ya mkewe akaanza soma sms za mkewe na majibu yangu.
Mpaka leo jamaa rafiki yangu alikuja gundua I was innocent ila sasa wananzengo wao hawaamini kuwa sikuwahi mtafuna huyo mama.
 
Hapo uliokokaa...!!
 
Itakua mlikua mnagombania Bwana
 
Sitakaa nisahau kipindi hicho nipo chuo nilipigiwa simu asubuhi sana saa 12 nikapokea hapo nipo na hangover mara naanza kuambiwa na mama kuwa mimi kazi yangu huko chuo ni kula bata tu na wala class siendi kuna mtu amemuhire ananifuatilia kila nachofanya.........aisee nilikuwa na hangover nikaona sielewi kitu kwanza nikamwambia nitamcheck baadae nikaendelea zangu kulala


Baadae nakuja kupiga simu home wakaniambia kuanzia sasa hivi mama ameamua kunipunguzia hela na sitakuwa napewa hela kuanzia alhamisi mpaka jumapili (maaana hizi siku ndo nilikuwa naomba sana hela home) na hapo nina boom ila walikuwa hawajali kuhusu hizo hela.........mi nikaawambia hizo habari hazina ukweli but huyo mtu wao waliomtuma amewadanganya sema hawakuniamini though ni kweli nilikuwa napenda sana bata ila mengine nilisingiziwa hasa la kutoingia kabisa class


Kiukweli aliyeenda kuwaambia kwetu aliniletea matatizo sana maana kuanzia hapo kwa muda wa miezi kama mitatu niliishi kwa shida jamani (sema kuna mtu alikuwa anajitahidi kunipa backup) halafu nilikuwa najifanya kiburi kutokuwaomba hela na my mum wala alikuwa haniambii chochote na home wakawa hawanipigii simu na mimi nikawa siwatafuti


Nashukuru Mungu kuna siku huyo anaenipa backup akaniambia curious acha ujinga hapo hauna hela kabisa mpigie simu your mum najua lazima atakupa hela na kweli kuanzia hapo flow yangu ya kupewa hela ikarudi kama kawaida tena nilikuwa nakomesha kwa kulipizia maumivu ya nyuma


Nilimlaani kwa kila aina ya maneno aliyeenda kuwaambia kwetu maneno ya uongo na bahati nzuri nilipomaliza chuo my mum alikuja kuniambia mtu aliyesema hayo maneno........kuanzia hapo sitaki kusema nilichomfanyia huyo shiwaladu


Kusingiziwa ni kubaya sana omba yasikukute
 
Haa ha ha...ila wew hukusingiziwa jamaa alikushilawaduu...!! Maana unapigwa simu still una hang over...balaa
 
Haa ha ha...ila wew hukusingiziwa jamaa alikushilawaduu...!! Maana unapigwa simu still una hang over...balaa
Hahahahahahaaaaa hiyo kawaida maana home wanajua kama nakunywa sema huyo shilawadu aliwaambia hata class siingii kabisa kitu ambacho si cha kweli
 
Hahahahahahaaaaa hiyo kawaida maana home wanajua kama nakunywa sema huyo shilawadu aliwaambia hata class siingii kabisa kitu ambacho si cha kweli
Hapo kwenye class bhasi ndo alikuchomaa..!!
 
Nmewahi kusingizia mtu kitu na nimewahi kusingiziwa vitu.
 
JF hapa watu wenyewe wananisingizia mengi kweli... Ila ukweli naujua mimi
Tatizo humu mtu mmoja akikujua mambo yako basi umekwisha.......atafungua na ID yake ya zamani huko aje akudhalilishe na vitu vyake vya uongo ili uonekane una tabia mbaya


Sio kila unaejuana nae humu atakuwa mtu mzuri kwako...........ili nimejifunza through JF
 
Uko sahihi, usipende watu wakujue sana kihivyo sometimes ndio haohao wanakuja kukuzushia mambo mengine ambayo hata hujayafanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…