Niliwahi piga beki 3 kimasihara akanasa. Ilikuwa tabu ndani ya nyumba. Kila nikimgusia kuhusu suala la kutoa akawa anakuwa mbogo. Dogo alikuwa kiburi mpaka nikajuta.
Katika harakati za kusugua akili ni jinsi gan ntamaliza msala kuna jamaa akanambia kazi ngumu huwa ni maji na mafuta na mimba changa.
Sasa Kuna shimo lilikuwa pale home limejaa maji nikamwambia wife nahitaji yale maji yatolewe yote kuna ukarabati nataka kulifanyia.
Wife akamu assign beki tatu ile kazi ya kutoa maji kwenye lile shimo. Jioni yake wife ananiambia eti beki 3 analalamika mgongo na kiuno vinamuuma anaomba kesho yake apumzike. Ikabidi niwe mbogo wife akakubali yaishe kesho yake kamwamsha saa kumi na moja asubuhi aendelee na kazi ya kuchota maji.
Moyoni nikajisemea Yes, jioni yake narudi najipitisha pale kwenye shimo kucheki maji hayajaisha. Naingia ndani kutaka kuleta noma wife ananipokea mlangoni na maneno yanayonifanya nijione bonge la bwana "mume wangu, rais wa malofa, mdada ameshindwa kumaliza kazi uliyonambia nimwambie aifanye" kuuliza kwanini nikaambiwa anaumwa tumbo na hapo alipo anatoka damu nyingi saana. Nikazuga zuga pale, moyoni nikajisemea mission accomplished.
Imepita miezi minne na beki tatu bado yupo, siku moja alinitumia sms "sikutaka kutoa mimba yako sababu nilijua wewe ni baba sahihi wa mwanangu, Una akili saana byee."
Mpaka leo sijawahi kuliongelea lile shimo na maji yake. Wife nae yupo amebunda tu hajui nini kilitokea.
Sent using
Jamii Forums mobile app