MUENDELEZOo
KULA KIMASIHARA KULIVYOBADILI HADITHI NZIMA YA MAISHA YANGU....
Tuseme ni part 03........
_ Wakati wote hayo yanaendelea wanda alikuwa ndani akilia huku amezungukwa na wamama kadhaa lakini aliekuwa karibu yake akimtia moyo na kumbembeleza alikuwa ni huyo mama yake mdogo wa sasaivi lakini walikuwa hawajuani na ndio mara ya kwanza wao kukutana..
_ Wakati huo wote hawakujua kama nje kuna taarifa za msiba wa baba.. mda wanda analia wamam kadhaa walikuwa wakimuuliza ilikuaje mpaka yeye atake kumdhuru baba yake kwa kifo cha mama yake.. na wote walihisi labda mzee huyo alimpiga mke wake na kumsababishia kifo. Ila kila walipomuuliza wanda hakujibu alikuwa anaishia kulia kwa kwikwi...
_ wakati hayo yakiendelea ndipo ikasikia sauti ya watu nje ya nyumba wakizungumzia kuwa baba nae kajinyonga wamama wote mle ndani walishangaa kwa kutoa macho na kujiziba mdomo, wakiwa na maswali imekuaje kuaje tena na baadhi yao wakaanza kutoka nje ili kujua zaidi imekuaje, wanda aliposikia hiyo taarifa aliganda yaan kam mtu ambae amepigwa na mshtuko wa moyo hapohapo akakata moto ( Alizimia ).....
_ Wanda akasema alikuja kushtuka nje anapepewa, alizinduka akiwa anajiuliza vipi mbona kazungukwa na watu, kumbukumbu iliporudi tena na kukumbuka akaangua kilio na kuzimia tena.....
Wakati huu alishtuka akiwa zahanati ya kijiji iliyopo nyuma ya jengo la serikali ya kijiji,, alichokuwa anashangaa ni kwamba kila akizimia na kuzinduka wakwanza kumuona ni huyo mama ake mdogo wa sasa ambae alikuwa hamjui ila alikuwa tofauti na wamama wengine akionekana sio wa pale kijijini maan hata mavazi yake hayakuwa ya kijijini na alikuwa mda wote kavalia miwani yenye kioo cheupe ambacho kiliruhusu kuona macho yake.....
.......Kwakua ilikuwa usiku tayari na hakuna ndugu mwingine wakumsubiri miili ilibidi ipumzishwe kesho yake mchana ambapo ilipumzishwa nyuma ya nyumba waliyokuwa wakiishi karibu na sehem walipomkuta mama kafariki....
__Wanda akaniambia kilichomuuma zaid ni kwamba alikuwa hajui baada ya hapo ataishije . Hana ndugu , hajui ataanzia wapi mwaisha ya upweke na kijijini porini kam vile na zaidi ni kupoteza watu watatu ndani ya msiba ule...😬😬😬^^ namimi nilishangaa kama wewe ndugu msomaji watatu kivipi wakati ni wawili baba na mama^^... akaniambia kwamba
..
.... Kuna siku mama yake alimuita na kumuambia kuwa alikuwa na mimba ya mdogo wake ambayo ilikuwa changa Wanda alifurahi akitegemea kupata mdogo. Kwahyo baadhi ya kazi alizokuwa akifanya mama, Wanda ilibidi amsaidie mama maana mimba kadhaa zilishawah kuharibika kutokan na mama kufanya kazi nyingi ngumu so ili hii kuitetea ilibidi Wanda amasaidie mama yake. Ndoman mpka yeye anakua mkubwa hakukuwa na mdogo wake sababu mimba zilikuwa zinaharibika na walivoenda hospitali akashauriwa hivyo....
_Na siku ya tukio wenda Mama aliwah kurudi sababu alikuwa akijiskia vibaya na hofu ya wenda mume wake alipatwa na tatizo njiani akielekea shambani maana wakati wanaamka kwenda shambani mzee alimwambia mama Wanda atangulie yeye atafata baadae lakini haikuwa hivyo, wakati mama kabla hajafariki alikuwa akilalamika na kumlaumu mzee wake kuwa alipanga kufanya ubaya ndomana akamwambia yeye Atangulie.... ndo kurudi kakutana na tukio....
..... Baada ya mazishi mida ya jion kam saa 10 au 11 hivi watu wakiwa wamepukutika wakibakia wachache hasa viongozi wa serikali ya kijiji maana hakukuwa na ndugu,, wanda alifatwa na mwenyekiti wa serikali ya kijiji na kuambiwa kuwa aingie ndan achukue nguo zake kadhaa na aingie chumbani kwa wazazi wake akachukue vitu vya kumbukumbu na vya muhimu then waongozane ofisi ya serikali ya kijiji kuna kitu cha kuzungumza...
... Wanda aliingia akachukua nguo zake nzuri nzuri alizozipenda kuzivaa unaweza kusema nguo za sikukuu zilikuwa chache tu akaingia chumban kwa wazazi wake akachukua nguo kadhaa za mama yake,, alikuta fedha kiasi kadhaa ambazo anasema hakuziheasabu alibeba hivohivo. Kitu cha kumbukumbuk alichoweza kukibeba ni album ya picha (zile za karatasi za zamani sijui nimepatia) ambayo hapo kabla hakuwahi kuiona
.... kulikuwa kuna redio ndogo zile za zaman na baadh ya vtu ambavyo havikuwa na umuhimu sana akaviacha akijua atakaa siku za kuomboleza msiba kwa mwenyekiti ila atarudi tena nyumbani kukaa.... alivyotoka nje akaongozana na viongozi wa kijiji mpaka ofisi,, anakwambia njiani alikuwa akipewa pole na kila mtu aliekutana nae njiani mkasa wake ulimfanya kuwa maarufu pale kijijini..
....Walivyofika mazungumzo yalianza yakihusisha watu wanne wazee wakiume wawili, wanda pamoja na huyo mama yake mdogo wa sasa .....
Aliambiwa kwamba huyo mmama unaemuona pembeni yako alikuja hapa kijijini tangu wiki iliopita ni mtu wa jeshi kitengo maalumu cha madawa ya kulevya;;
Alikuja hapa kijijini kutoa elimu kwa vijana kuhusu madawa ya kulevya akiwa na wenzake ambao washatangulia kurudi Dar es salam. Na walianza elimu hii mda mrefu wakizunguka vijiji vyote katika wilaya yetu ....
na sababu iiyomfanya yeye abaki mpaka hapa leo baada ya wenzake kuondoka ni siku ambayo alikuwa anaagana na uongozi wa kijiji alifika baba yako na kutuomba twende huko kwake kuna tatizo mke wake anatoka mapovu mdomoni....
Alivosikia kauli ya mapovu mdomoni na Kwakua yeye ni mtaalamu wa madawa na ni dharura ikabidi aongozane nasi kuja kwenu ili kuona kama ataweza kutoa msaada... ila ikawa tumechelewa sana...
Kusema ukweli ameguswa na mkasa wako hasa hali ya maisha yako kuanzia sasa hauna ndugu na hauna mtu wa kukuangalia na familia nyingi za hapa kijijini ni za uwezo wa chini kumpata mtu wa kukulea ngumu;; hivyo ameomba akuchukue uende nae Dar es salaam ukaishi nae huko na atakusomesha.......
__Kimoyo moyo wanda alifurahi sana hadi kutoa tabasamu kuonesha kufurahishwa na jambo hilo licha y kuwa amepata mlezi bali anaenda kuishi Dar jiji ambalo amekuwa akisiki wenzake wakiadisia tu kuwa kuna maghorofa na mambo mengi .. ilihali yeye hata morogoro mjini hajawah kufik na hata gari alipanda mara kadhaa tu ....
__ Baada ya Wanda kuridhia.. mama mdogo akamwambia wanda kua asijali kuhusu malezi atamlea vyema na yeye anamtoto mmoj tu wakiume basi Wanda atageuka kuwa kama binti yake wakike.. pia kuhusu nyumbani akamwambia asijali maana ashaongea na mwenyekiti na ametaftwa kijana atalinda eneo hilo na atalala pale kwao ila ile ardhi itasajiliwa rasmi kwa Jina lake wanda na kumbukumbu ya wazazi wake isipotee...
^-- Safari ilianza jioni hyohyo na kuna sehemu walisimama kwa rafiki yake mamdogo wakalala kisha safari iliendelea kesho yake na kufika dar mchana ambapo walifikia katika ile nyumba ya mbagala ( ambapo tulikimbilia mim na wanda baada ya kutoka mpirani)..
___ kama unavyojua wakishua yaani ile wamezama ndan ya geti tu wakakutana na watu wengi ila sio sana ndani ya fence wamevaa vzur huku wengi wao suti na wameshika vnywaji wanaongea kwa makundi makundi. yaani kam party hivi.. mama mdogo alishangaa hakujua kinachoendelea nin ila alivyozama ndani akakutana na taarifa ya kuwa mumewe amechaguliwa ni moja kwati ya watu ambao wataenda kufanya kazi katika ubalozi wa Tanzania nchi flani......
Baada ya chakula na nin watu kuondoka na shereh kuisha ndipo mama akamtambulisha wanda kwa wanafamilia na hawakuonekan kumshangaa sababu walikuwa na taarifa na ujio wake....
...__ Maisha ya Dar yalianza vzuri huku wanda akiwa mgeni na anashangaa kila kitu yale mambo ya profesa jay viatu kwenye friji hayo mambo ndo alikuwa nayo 😂😂 huu mfano alinipa mwenyew naukumbuka hadi leo nlicheka sana😂😂...... Lakini baada ya mda baba mwenye nyumba aliondoka kwenda uko ughaibuni na aliondoka na mtoto wakiume wa huyo mama. Hivyo mama mdogo alibaki na Wanda pamoja na house girl pamoja na ndugu baadhi ya familia hyo waliokuwa wakiishi pale ambao sio muhimu kuwataja 😂😂 infact nmewasahau 🥴🥴......
^___ Maisha yalikuwa mazuri sana na nlipomuuliza kuhusu kunyanyaswa au kuteswa kuchukiwa na ndugu wa mamdogo.. alisema haikuwah kutokea.. ndo nikaamini. manyanyaso huwaga kwa familia za kimaskini, ambao hatuna uwakika wa kula ndipo chuki hukuwepo.....
^..... Mambo yote mam mkubwa aliyafanya kama alivyoahidi kasoro kitu kimoja tu .... nikamuuliza kipi akasema """ELIMU""" ,,, Tangu afike dar hakuwah sikia kuhusu shule wala chochote licha ya mama mdogo alikuwa nanuwezo wa kumsomesha na hcho kitu Wanda alaikuwa akimsumbua sana mama mdogo amabe alikuwa akimjibu tu kuwa nasubira nakutaftia kitu kizuri.....
""_ Tangu watoke morogoro alikaa dar kwa miaka mi3 huku mda mwingi akishinda nyumbani tu basi bila ya hata ya kufanya kitu wala kwenda shule na mama alikuwa sio mkaaji . Akikaa kidogo then anasafiri kwa mume wake.. akipata likizo hata iwe ya wiki mbili mama anakwea pipa.... 😂😂 mama alikuwa anautaka sana🙌🏽🙌🏽
..._ Baada ya miaka mitatu kupita mama kuna siku alimfata Wanda na kumwambia anataka ampeleke jeshi. Wanda alikubali bila kipingamizi kutokan na kuchoka kukaa nyumbani. Alihisi pia jesh itakuwa rahisi ukizingatia yeye ni mtoto wakike alafu alikuwa na hasira na wanaume wenye tabia kama za baba ake na aliapa akiwa polisi atakamata wabakaji wote na kuwafunga yeye mwenyew 😁😁 akili za kitoto bhna 😂
Alienda jeshini maisha aliyakuta ni magumu na ukakamavu sana hakutegemea na akasema huko ndo aliwachukia kabisa wanaume maan makamanda walikuwa wanapigisha mazoez na adhabu sio poa yaani ndo alizidi kutuchukia.... Akasema Jeshini ile ya kujitolea alikaa miaka yote miwili na mamdogo alitaka Wanda akomae kweli maana hata likizo wakati wa kujitolea wenzake walipopata yeye alinyimwa ...... so alishinda tena kambini kigoma huko porini kwa miaka miwili ya kujitolea ndipo akarudi tena Mjini akiwa kakomaa mpaka ugoko.....
^___ Aliporudi alishangaa safari ya kwenda nyumbani inakuwa fupi ghafla na kutahamaki sio mbagala tena bali mamdogo kajenga nyumba nyingine tena maeneo ya Mbezi. Nyumba ni kubwa na yakisas zaidi kuliko ile ya mbagala na alipouliza kule kabaki nani wakasema wanakaa wafanyakazi wakufanya usafi na mambo mengine mchana na ikifika usiku nyumba inafungwa...
Lakini alipofika nyumbani hakumaliza hata mwezi mama akampeleka tena kambi nyingine amabyo iko pwani maarufu sana huko pia akakaa kwa mwaka mmoja bila likizo ndipo aliorudi tena nyumbani sas rasmi tena akiwa na ajira kama ya kitengo cha mama....
Ila wakati yeye anatoka kambini alikuta mama nae ametoka kozi... kwa wasioelewa... kunabaadhi ya vitengo vya jeshi na baadhi ya idara ukitaka upande cheo lazima ukasomee kozi ili uendane na cheo katika hyo idara....sas hapo yeye anarudi anakutana na mama nae ametoka kozi sio mda mrefu yeye na wenzake kadhaa......
....Kwa alivyosema Wanda Sas ukimaliza kozi kutoka na hivyo vitengo na idara unakuwa tu hupandishwi cheo hivihivi inabidi uendlee kazini kupambania uapisho wako ukizembea kwenye utendaji wenzako wataapishwa wew jina lako halipo....
So kama njia ya kufanya kuaminika na wakuu wao ili wapandishwe vyeo mamdogo na wenzake amabo kapiga nao kozi. wakaja na idea ya kukamata wauzaji wa madawa wakubwa so ili kuwafaham ikabidi itengenezwe mission ya mtu ajifanye anatumia madawa aingie kitaani kupitia watumiaji wadogo wadogo na wauzaji wadog atapata info zote za wauzaji wakubwa... mwisho atoe taarifa idarani ili hao wauzaji wakamatwe.. hivyo baada ya mission kukamilika wangepewa mahongera kwa kazi nzuri na vyeo vyao juu na mishahara kupanda...
__ Mamdogo akaona hii mission aifanye wanda sababu hawezi akawauza pia katoka kambini bado wamoto alafu wanaume wengi wakiona mwanawake hawawatilii maanani kabisa (hawampi attention kama ni tatizo kwao)😂😂 hii kweli 👍🏼👍🏼 Mwisho mamdogo alijua Wanda ni mwanae so mission ikikamilika hata wanda atapanda kutoka chini mpka cheo flan hv japo ni kidg na heshima atapewa mamdogo sababu ni kumpika dog (wanda) vzur.....
__jeshin hain kukubali wal kukataa hasa wakuu zako wakishafanya maamuzi. So Wanda akageuka kuwa Tom boy akapewa na mavazi, wakatafta location nzuri ya mtaa. Wakapanga geto na kuweka kila kitu awe kama kitoto flani chakishua tom boy ambacho kimeshindikana kwao hvyo anakaa mtaani... alilipiwa hadi Gym kila sku alfajiri anaenda mazoezin ili kutopoteza fitness yake japo ilibidi iwe siri watu wasije mshtukia .....
^___ Na mpaka mim naenda pale alikuwa na miezi kama 8 kwenye mission na walifikia hatua nzuri maan wanda alishawajua baadhi ya wauzaji wakubwa ilibaki location na mitego tu hvyo walikuwa wanawasikilizia tu...
.................................................
_-' Wakuu nilishusha pumzi nzitoo hyo baada ya hyo story. Wanda akanambia wale wakuu wake hasa mamdogo itakuwa washanishtukia so ili nisitoe siri watajaribu kuja kunikamata wanaweza wakaniuliza maswali na kuhojiwa lakin alinambia nisikubali kitu niseme sijui na sjasikia kitu.. na wakinipa sharti lolote nikubali kufanya kwasababu nikienda kinyume na wakiona hatari ya kuharbika mission yao wanaweza wakanifanya kitu kibaya watu wanataka wapewe vyeo vyao kwahyo nisifanye masihara washatumia gharama kubwa kwahyo nifate masharti...
Akaniahidi kwamba atanisaidia kwa kila ntakapo pata tatzo na atawashawishi wasinifanye kitu kibaya.... Tulikaa kimya huku wanda akiwa kifuani kwangu kwa mda wa kama dakika 10 hivi kila mtu akitafakari cha kwake. Ndipo akanigeukia na kuniuliza vip kuhusu wew hadithi yako ??!!! ^^ nikamuomba niende kwanza nikajisaidie alafu nikirudi ntamuhadthia.....
Nikivyofika chooni wakuu kama mnavojua kurupushani ya siku nzima ikanibidi nichukue nafasi ile kukata gogo, nikaoga na nilikaa nje kama dakik nyingine amabzo sikuzihesabu kupata hewa safi kwenye kigiza watu wasinione na nivyorudi ndani nikamkuta wanda anasinzia.... nikajifunika nae huku nimemkumbatia nikalala....
--^ Nikiwa nimezama kwenye usingizi mzito naskia naamshwa na Wanda huku akinishika shika usoni. Nafumbua macho namuona kavaa nguo zake zakitom boy. Namuuliza anasema saa 11 kasoro anawahi Gym ambayo ipo mbali sana na pale mtaani ( nahisi ni ya Jeshi maana location aliyontajia).... na alibeba begi na humo aliweka nguo ambazo angezivaa akifika huko zakufanyia mazoezi.
nilimind kinoma yaan hata usingizi haujanikamata vzuri.. nikaamka nikataka niforce anipe morning glory lakin alikataa katakata akasema tutakutana usiku saiv niwe naenda kulala kwake🔥🔥🔥....
Basi nikajikokota mpka home 🏡. Bro huwa anaondokaga asubuh saa 11 hvy mpka mda huo alikuwa ashasepa si unajua wasaka tonge mishe mishe. Hata mlango ulikuwa haujafungwa kwa funguo sababu bro akiondoka ili asisumbue watu alikuwa haufungagi anaurudisha tu. Mim na shem tukiamka tunakuta uko wazi na saa 11 hakuna wezi .... niliingia ndani mpak chumbani nikajitupa mzima mzima kitandani nikiwaza asubuh nikiamka chakwanza nkatafte simu yangu then nikalala....
Nipo usingizin yaan sio mda mrefu toka nimeingia kulala naskia sauti ya shemeji ikiniita kutokea sebuleni " shemeji , shemeji " unajua hawez kuingia chumbani ananiitia kutoka sebuleni na saut za wanawake sauti kubwa kalii. Nilishikwa na hasira sababu yaani kila nkipata usingizi na siku yenyewe ndo kama hvyo nakuta naamshwa... nikajibu kwa hasirq "" nini tenaa""... nae akanijibu "" kuna wageni wako"". Nami nikajibu kwa hasira """Aaaah wageni gani tena saiv kwan wangekuja baadae shida ingekuwa wapi aaah"""......
Nikaamka kuchungulia dirishan bado hakujapapambazuka vzur yaani ni kama saa 12 hiv kasoro.. shemu alivoniita alirudi chumbani kwake nahisi nayeye aliamshwa na hodi za watu hao... kufungua mlango nilivyotak nje nakutana na zile njemba mbili za jana usiku walionikita likibao.....
Nilitamani kulia wanangu nikatoa macho nikajiuliza nimeharibu nin tena. Ndipo wakanambia vaa ndala hizo twende.. wakiashiria ndala flan ambazo walizikuta pale chini....
Walinibeba mkukumkuku wanangu mpka kwenye gari yao.........
INAENDELEA HIV PUNDE........
Wazee story ndo imefika pazuri ....... asubuhi imefika ngoja niwape huu muendelezo huku nikiendelea kutype......
Leo niko off nikuandika tu......