Afande nilifeli kinoma, kuna bidada mmoja ni homegirl wangu tulipangiwa wote 841kj.
Dogo alikuwa ananikubal wayback tuko o level mie nikawa sina time nae.
Muda umeenda tukaja pangwa wote 841 pale akawa kama manzi angu muda wa kufolen badi hangan mlee na ile barid mie nakula utulivu.
Siku tunamaliza coz nikambook mapema kuwa nitadance nae pale mwamunyange kama sikosei lile hall kubwa la chawote, maana kulikuwa na disco la kuagana.
Basi tumepata msosi, manzi akaja mie nikawa bado nataka zile za kucheza kwanza kiumeni afu badae mida ya wanga ndio nikakamilishe kazi, daaaaah ile nimecheza kiumen nataka nimuendee manzi nakuta yuko na mdau mwingine afu manzi kama vile alimind kuwa na mkwepa ,basi ikashindikana kila nikijaribu peyeza rupia naona jamaa hana time ya kuachia pale, nkamute.
Time imeenda kuja kusanuka saa sijuii saa 8 tunaambiwa disco limeisha ,daaa mie nliwaza kuwa mida ya saa 8 saa 10 ndio mida ya kufanya unyamwela kumbe hesab za kijeshi hazikuwa hivoo bwana.
Tumeondoka pale saa 8 tukaambiwa tukajiandae tuannze kurudisha blanket, shuka na stuffs zingine ambazo zilikuwa bado kukusanywa, ikabidi nimcheki mtoto kwa hewa aje tukumbatiane hadi asubuhi anitoe baridi maana hapo ni saa 9 ,jeshi limechukua blanket godoro na shuka zao hakuna pakulala.
Nilimtafuta yule dogo kwa simu sikumpata sijui alienda gongwa na majamaaa baada ya lile disco daaaah nikikumbuka huwa najilauku sana sema nimemiss sana yale maisha ya palee kwa Cpt Moshi na Maiga