Kabla ya yote nataka ifahamike kuwa bandiko hili halina nia ya kukejeli wanawake tajwa hapo juu bali najaribu kuelezea uhalisia wa sehemu ya mapito yangu.
Fuatana nami[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Kama mkataba wa kazi yangu ulivyonitaka niwe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Tanzania na ndivyo ilivyotokea nikajikuta nipo bandarini kusubiria boti ya kuelekea zanzibar kufanya kazi huko kwa muda wa miezi sita. Ilikua ni mara yangu ya kwanza kwenda zanzibar na pia mara ya kwanza kutoka nje ya kituo kikuu cha kazi yangu hapa dar es salaam na kupangiwa kituo kingine tangu nipate mkataba wa miaka mitatu kwenye kampuni hii iliyokua na makao makuu yake ndani ya bandari ya dar es salaam. Sehemu zetu za kazi ambazo mtu angepaswa kwenda kama angehamishwa kutoka hapa makao makuu ni mtwara, tanga, unguja, pemba, mafia na bagamoyo.
Safari ilianza saa 11 jioni, nikiwa na begi langu nikaingia kwenye boti na kwenda kukaa kwenye daraja la tiketi yangu ambalo ni silver class. Sehemu niliyokaa kando yangu kulikua na msichana wa kati ya miaka 22+ ambapo yeye alitangulia kuingia kabla yangu na nilimkuta yuko bize na simu yake ya tochi, nikamsalimia na hatukua na maongezi tena kati yetu kwa muda huo. Baada ya safari kuanza na kila kitu kutulia nami nikaona nitoe simu yangu japo niperuzi. Simu yangu ilikua ni iphone 5s kwa wakati huo na ilikua siku nzuri haswa. Sasa bwana, baada ya kuitoa ile simu nikaona yule msichana amemakinika kidogo kuikazia macho, na baada ya muda akaanza kunisemesha na kuuliza ile ni simu gani, nilipomjibu akafungua mkoba wake akatoa simu kama ile ikiwa mpya kabisa akasema alitumiwa na ndugu yake kutoka canada na ametoka kuichukua lakini hawezi kuitumia na hata alipojaribu kuweka line hakuona majina. Basi nikamfanyia setting pale ikiwa ni pamoja na kumtengenezea apple id ili aweze kutumia na baada ya hapo tukawa kama watu tuliofahamiana kitambo, nikapata mpaka namba. Katika kufahamiana nikagundua kuwa yule msichana kwao mombasa lakini anaishi unguja, na akaniambia kama mipango itaenda sawa anatarajia kwenda kuishi canada miezi mitatu mpaka sita ijayo.
Baada ya kushuka pale bandarini (znz) kila mmoja (kati yetu) akashika njia yake huku tukipeana ahadi za kuwasiliana, lakini haikua hivyo kwani yule bint aliamua kunipotezea. Ni mara moja tu alipokea simu yangu baada ya kuachana pale bandarini tena ni pale nilipompigia ili kumuuliza kama amefika salama, baada hapo hakupokea tena simu wala kujibu sms. Kidume nilijaribu kwa njia zote kufanya ushawishi labda nitajibiwa lakini ikawa kinyume chake, nikakata tamaa lakini sikufuta namba. Nikapotezea kwa muda.
Baada ya wiki kama tatu hivi za kuwa busy weekend moja nikiwa mahali ninapoishi nimeshika simu yangu nikamkumbuka yule bint, nikasema wacha nijaribu leo nikatuma sms ya salamu, mara baada ya kutuma sms tu punde akanipigia. Ile kupokea bint ananiuliza mimi ni nani nikajisemea duh mpaka namba kafuta!, hata hivyo nikajitambulisha, ajabu bint akaanza kufurahi na kunilaumu kwa nini nilikua simtafuti nikashangaa!
Ktk kuendelea kuongea ndipo akaniambia mdogo wake amei restore ile simu yake (iphone) kwa bahati mbaya, na ameenda kwa fundi ameambiwa hawezi kuitumia mpaka aweke apple id iliyokuwepo awali lkn yeye anaikumbuka apple id pekee passwords amezisahau hivyo akataka kujua kama naweza kuzikumbuka, na kweli zilikua kichwani maana nilimuwekea passwords ninazotumia kwenye simu yangu.
Hata hivyo nikamwambia aje ninapoishi na hiyo simu kama anaweza, akaja.
Alivyokuja akanikuta napika sasa ili mimi nifanye kazi yake akaniambia jiko nimuachie yeye. Kazi kwangu haikua ngumu ila ikabidi nijicheleweshe ili nipikiwe kila kitu na pia nipate kuzoeana na yule bint. Akapika vikaiva na tukala pamoja, baada ya muda kdg ndipo nikampa simu yake ikiwa sawa. Yule bint aliiangalia simu mara moja tu na mara nikashtuka akiwa amenivaa mwilini huku akiwa amefurahi ajabu, akanikumbatia kwa nguvu huku napigwa mabusu hapo mzee sikulaza damu, japo nilipata usumbufu ule wa sitaki nataka lkn hatimae nilimla yule bint siku ile ile.
Rasmi sasa tukawa wapenzi baada ya lile game na ikafikia point mpaka nikawa naonewa wivu, ajabu ni kwamba hakuwahi kunionyesha kwao na hakutaka hata nipajue, sikujali. Baada ya miezi miwili ya uhusiano akaondoka kwenda mombasa na akasema anaenda kukamilisha taratibu za safari na alisafiri kweli. Kwa sasa yupo canada na hatuwasiliani baada ya kurudia zile tabia zake za kunata.
Baada ya mwezi kupita nikapata mwanamke mwingine, huyu kwao pemba ila alikua anafanya field pale bandarin unguja. Bint mweusi wa kipemba, mzur wa sura na asiekua na mambo mengi akameza ndoano yangu. Uhusiano ukaanza na ukashamiri, huyu nilimkuta bado bikra, nikampenda haswa huku nikijiwazia "huyu ndie mke".
Tulale kwanza....