huu uzi ulinivunjia mahusiano yangu, sitakuja kusahau, nilitoa ushuhuda mwaka mmoja uliopita, nikasimulia visa vyangu vinne nilivokula tunda kimasihara.
siku ya siku kulikua na ubatizo kwa jirani, baada ya sherehe za ubatizo za nyumban kumalizika, yule jiran akaomba nimsindikize kuwapeleka nduguze waliokuja ubatizoni, nikaona sio kesi, nikasepa nae mida kama ya saa sita usiku, nikaacha simu kwa huyo girlfriend wangu niliekua nimepanga kumuoa,
bila wasiwasi nikajua tutawah kurudi lakn jiran alinipitisha maeneo mengine mengi mengi na kurudi home mida ya sa nane,
kumbe huku home wife anapekua sim yangu, alipita kilaaa kona ya sim, alikuta mauchafu yangu yotee kwenye sim, ikiwa shuhuda za kula kimasihara, chatting zangu chafu za wasap na girls wengine, emails zangu na makorokoro mengine mengi sanaaa.
nilivorudi usiku ule hakusema kitu ila kesho yake kesi ilianza, na nilishindwa kesi mana sikua na mahala pakuchomoka,
baada ya wiki mbili nlitakiwa kwenda course mahali flan ambayo ingeniweka mbali nae na yeye ikampasa kwenda mkoani kwao, baada ya kufika kwao na mm kianza kujiandaa na kwenda course, ndipo akanipa taarifa rasmi kua hawezi kuendelea na mm tena.
sikumlaum, maana ni mara nyingi kanikuta na madudu kibao lakn amekua binti wa kusamehe sana.
ile ya mwisho ilikua funga kazi, akaridhia kusepa, aliniuma, ananiuma na ataniuma kwa sababu alikua mtu sahihi kwangu japo mm sikua mtu sahihi kwake.
kwa wenzangu wote tuliopi kwenye mahusiano, jali mahusiano yako, mjali mwenzio.
huu uzi nausoma sanaaaa lakn ulinipotezea njiwa wangu mzuri sana.
nakumis "E" wangu, stay good popote ulipo.
soon nitarejea japo nije hata nikusalimie tu.