kelao
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 8,132
- 5,785
Siku ile alikuja alshabibi tuu harafu alikuwa tayari kitaa maana alifurushwa chuo wakati wa kunji la alshababu 2011
Ulivaa kanzu?Ili uwe FFU unatakiwa uwe yatima kisha kichwa chako kiwe na bangi ya asili kabisa pia uwe na uchizi Kama asilimia hamsini halafu sifa zingine za uaskari zinafuata. Nakumbuka siku moja nipo Town kariakoo nanunua bidhaa nikasikia king'ola chao kinajamba kama Lori kisha kuna mdada anatangaza kuwa watu wote waliokuwa pale watawanyike .Mara wakaruka mijamaa imejifunika usoni maski ikasema kikosi cha virungu shambulia Yaani Nilipigwa rungu ya bega kisha tumbo .Nikaona nyota kisha giza totoro ile nashifuka najikuta nipo mnazimoja hospitali na pingu mkononi imeunganishwa kwenye kitanda na polisi wa kirai amekaa pembeni yangu. Nolipozinduka yule polisi akamwambia nesi nimepona .Yaani nilibebwa mzobe mzobe mpaka msimbazi polisi bahati nzuri akaja mkubwa wao akasema tuachiwe kwa dhamana . Naona mpaka leo bega langu halijaponaga. .NIKIONA KOFIA NYEKUNDU NAPITA MBALI SANA WALE SIYO WATU NI MICHIZI SANA YAANI SIKUWA NAJUA KINACHOENDELEA LAKINI WAKANISHAMBULIA. BAADAE NILIGUNDUA KUMBE HARAKATI ZA WAISLAM NA SHEKHE PONDA.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahah ulidhani ni mwisho wa dunia sio,hahah daahMwaka 2004/2005 kama sikosei, jamaa waliamsha dude furahisha mwanza. Kawaida ilikuwa miezi fulani hasa ya likizo ya june kunakuwa na mkutano wa Askofu wa kanisa la EAGT Moses Kulola (RIP) Waislamu nao walikuwa na mkutano wa hadhara palepale wakati maandalizi ya mkutano wa injili yanaendelea. Walokole wanajenga jukwaa, waislam wanabomoa. Kumbe ilisemekana waislam hawakuomba kibali na hawatakiwi kuwepo pale. Basi jamaa wakakaza vichwa (nafikiri hapa ndipo watu huhusisha uislamu na fujo ama ugaidi). Mpaka zimesalia siku kadhaa mkutano wa Kulola uanze, jamaa hawaelewi somo. Wakaanza kuandikwa vibaya na magazeti (hasa msanii africa) wakaanzisha vichambo kwa gazeti tajwa. Siku ya tukio nadhani kila upande ulishindwa kumvumilia mwenzie (walokole vs waislam) wakaanzisha vurugu, polisi wakaitwa kutoka kirumba wakashindwa. Zikamiminwa defender za kufa mtu. Nadhani yale mabomu huwa hayabagui, ni kama mvua tu inawanyeshea wema na waovu. Watu walilia,, fikiria kutoka uwanja wa furahisha mpaka milima ya isamilo (wenyeji wa mwanza mnanielewa) tulikipata cha mtema kuni. Ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupata madhara ya mabomu ya machozi, kwahiyo kutokana na akili za kijima nikajua ndio mwisho wa dunia😁😁. Nusu nizime ndipo watu wazima wakatukusanya madogo wote tukaambiwa tunawe kwa maji safi ndio ikawa salimika. Waliokuwa uwanjani walipigika kipigo cha Madagascar. Huwa sitaki mchezo kabisa hata wa traffic.
Kabisa mkuu. Kwanza hewa ilikuwa tofauti sana na kuna muda unahisi kama kuanguka. Isitoshe ilikuwa vita ya dini mbili tofauti nikajua ndio Mungu kafanya yaje. Nilisubiri tu kusikia parapandaHahah ulidhani ni mwisho wa dunia sio,hahah daah
kwani zile bunduki zina ishu gani mkuu,zile ni za machozi hazina ishu.Mnawatukuza sana,bila shaka wakisoma uzi huu wanajiona wa maana,km kweli wapo vzr waje bila Bunduki ndo watajua Kwanini kuku hakojoi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha pale mtwara (mnarani),, jamaa walikuwa wanatumia fimbo afu wamakonde walikuwa wanatumia mawe,, mechi ilipigwa karibia nusu saa, majaa wakakimbia wakaacha gari, gari lilipigwa mawe sana,,wanajeshi wakaja wakawa wanapita nyumba baada ya nyumba,,Ila jamaa hawa ni waoga sana nakumbuka
Mtwara vurugu ya gesi kati yao wamakonde zilipigwa uso kwa uso
Walivyozidiwa wakakimbia wakaenda kuitwa wanajeshi zikapigwa hatari hadi vifaru vilipelekwa ilikuwa zaidi ya hatari
Sent using Jamii Forums mobile app
HahahaMgomo wa machinga mbeya siji sahau mara ya Kwanza nashuhudia mtu anapigwa risasi live, yalipigwa mabomu ya machozi uoni mbele wala nyuma nilikimbia peku sijui viatu vilivulika saa ngapi.
Onyo ukiwaona hao kaa mbali sana kama huelewi jalibu siku kuwasogelea.
Akili za kijimaHahah ulidhani ni mwisho wa dunia sio,hahah daah
nomaNov 10 ,2017
At St. Pauls Liuli High School Nyasa
Tuligoma bwana. Sio kwa kile kisago. Tuliamka kila mtu kavaa ndala au kiatu dongea