Hakuna sababu yeyote inayo halalisha kuandikiwa dissertation na mtu. Kwangu mimi huu ni upumbavu uliotukuka. Nikiwa supervisor wako au kwenye examination panel yako ujue nitakushika tu. Tukiacha hayo ya kushikana, kuandikiwa au kufanyiwa utafiti na mtu mwingine inaonyesha hujui kile unafanya zaidi ya kutafuta yale makaratasi na hapo kuna tatizo kwenye supervision-supervisor mzuri atajua kinacho endelea.
Wenzetu wana masters ambazo dissertation sio lazima unaweza instead ukafanya courses za ziada kutimiza graduation requirements au internship na kuandika report. Hizi zinawafaa zaidi wale ambao hawana ulazima wa kufanya utafiti kutokana na malengo yao. Bahati mbaya hapa Tz masters zetu karibu zote tunatanguliza dissertation.
Take home: Sifagilii kufanyiwa au kuandikiwa research-hii ni sawa na wizi/udanganyifu wa hali ya juu.