Ulipwaji wa bima baada ya kupata ajali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulipwaji wa bima baada ya kupata ajali

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Lusyonja, Oct 20, 2009.

 1. L

  Lusyonja Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 21, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Salaam wana jamii.Naombeni ushauri tunawezaje kupata malipo ya bima baada ya kuumia katika ajali ya barabarani hapa dsm.sie tulikuwa katika basi, lilikuja loli lilioshehana pamba likagonga kwa nyuma basi letu na kuendelea kugonga magari mengine hadi matano.
  ajali ilipimwa, vielelezo vyote vya magari yaliyohusika katika ajali vipo tayari na jarada lipo osterbay polisi tayari kupelekwa mahakamani , lile loli lililotugonga lilikuwa na comprehensive hai ya Jubilei insurance.Tajiri wa gari hataki kutujazia MOTOR ACCIDENT REPORT FORM, alipeleka polisi insurance cover note tu bila risiti. cha kushangaza katika mashtaka ya dereva wa loli limeongezwa kosa la kuendesha bila bima wakati sio kweli!.
  1. Je wanajamii tulioathirika na ajali hiyo tunawezachukue hatua gani ?
  2. Yawezekana kuna ufisadi kati ya mwenye gari na Jubilei insurance ili
  tusilipwe haki zetu.je tunaweza kufanya nini ili haki itendeke.
  3. Kama huyo mwenye loli lilisababisha ajali hataki na hataweza kujaza MOTO
  ACCIDENT REPORT FORM , ni jinsi gani ya kumlazimisha mmiliki wa Jubilei
  insurance aweze kutulipa Bima zetu pamoja na magari yaliyogogwa?

  Asanteni kwa ushauri wa kawaida na kisheria kwani naona kuna harufu kali ya RUSHWA!
  Lusyonja
   
 2. October

  October JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kweli yule mwenye Lori alikua hana Bima, kitu ambacho kinathibitishwa na kushindwa kwake kuwakilisha Receipt ya Bima. Kuna baadhi ya matapeli kuiba Covernote za Kampuni fulani ya Bima na kuwauzia wateja, wanaweka Hela mfukoni huku wakiomba mungu ajali isitokee. Pale inapotokea ajali ndo wanapogundulika kwamba walikua hawana Insurance ya kweli.

  Hata hivyo hata kama gari iliyowagonga haikuwa na bima bado mna haki ya kulipwa Ingwawa itachukua muda kidogo. Utaratibu ni kwamba lazima lazima Kesi iende mahakamani na mahakama itoe hukumu kwa mkosaji kupewa adhabu anayostahili. Baada ya hukumu mnaweza kufungua kesi ya madai mkiambatanisha na nakala ya hukumu ili kufungua kesi ya madai ili mlipwe fidia.

  Kama mwenye gari hakuwa na bima hiyo ni shauri yake kwa sababu mahakama itamwamuru kulipa kutoka mfukoni mwake, kama alikua na bima halali basi bima yake italipa.
   
 3. L

  Lusyonja Member

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 21, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana October, kwa jinsi hiyo inatubidi tuwe wapole tusubiri mwenendo wa kesi , nadhani wiki hii haitapita.Nitaku-PM baada ya kesi kwisha ili utushauri ni wapi tunapata wakili wa kesi za traffic na tunafungulia mahakama gani.

  Mwanajamii sheria inabidi tuzijue na haki zetu tuzijue laa sivyo itakula kwetu siku zote.

  Thanx
   
Loading...