Silas Haki
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 368
- 39
Hapa mzee umegusa penyewe kabisa, mimi nilikuwa nagombana na makatibu wa CCM wa kata yangu kwa kuwaambia kuwa mtu waliyeweka agombee alikuwa kimeo kama siyo kimeta.
Wewe nani alikuambia haya yote? Kama huwezi kufuatilia ukalale au ukaandamane kuwaunga mkono CCM kujivua magamba.TIP:
this is forum, usionyese ufundi wa kuandika, hapa mtu akifungua post anataka aone point moja kwa moja, be STRAIGHT, mtu hawezi kufatilia para hadi ya tatu bado kabla ya kuelewa point yako
Mkuu umenikumbusha mbali sana...wakati wakimteua hiyo 2005,nakumbuka tulibishana sana na rafiiki yangu mmoja,nikamwambia MOYO WANGU NI MZITO SANA KAMA HUYU JAMAA ANAWEZA..sababu: nikamwambia naona kama vyombo vya habari vinatumia nguvu nyingi mno kumtangaza,methali isemayo chema chajiuza,kibaya..inagonga mara kwa mara kichwani mwangu....tukajaribu kutathmini nini jamaa amekifanya cha kumfanya akiweze kiti kikubwa hicho,tukatapatapa huku na kule-wapi!ubaya ni kuwa rafiki yangu alikuwa tayari ameshaleweshwa na vyombo vya habari-hatukufanikiwa!...umenikumbusha tena kuwa ile Octoba watu walipoenda Diamond,nilikuwa department moja pale UDSM ambapo vijana wengi walipewa t-shirts na kofia,nilkuwa mmoja kati ya watu tuliopinga sana 'kutumika kwa vijana wasomi kwa kiasi hicho,lakini kilichotokea,sikukiamini hadi leo-maana walikuwepo watu nawamini sana katika uwezo wa kuhoji na kuchambua maamuzi-walikuwepo kwenye mkumbo ule wa kwenda Diamond bila kuhoji kama tulivyowazoea. Wachache tuliobaki na kukataa kile kitu tulionekana watu fulani mataahira!(nashukuru leo hii tunajivunia maamuzi yetu).
Nafikiri tuendelee kutafakari na kuchukua hatua..historia imetuhukumu..ni funzo kubwa..muda mwingine labda makosa haya hayatarudiwa...
Mimi nilijua tu kuwa hawezi. Baada ya kuwa nimewahi kukaa naye maraka kadhaa vikaoni wakati akiwa bado anafukuzia wasichana kule Sinza nilijua kuwa jamaa yule alikuwa ni sifuri kabisa kichwani. Sikutegemea kuwa angeweza kuwa hata waziri ila nikashangaa kuwa aliwahi kutuwakilisha kama diplomat mkuu wa nchi kwa miaka kumi kabla hajawa mfalme wetu. Kwa jumla ya miaka 20, yeye ndiye anakuwa image ya watanzania nje ya nchi; yaani wababaishaji wasiojua kuchambua mambo kwa kina!!
Nikikumbuka inauma sana ijapokuwa hakuambulia kura yangu lakani the way vijana wa rika langu kipindi hicho walivyokuwa wakimshabikia kwa kweli nilinyongonyea kwa kuona Tanzania yetu ikidumbukia shimoni pasipo kuwa na msaada wowote.
Nakumbuka huyu jamaa kipindi hicho alikuwa na kashfa tayari ya IPTL, sikupata picha akipewa madaraka makubwa kama haya atafanya ufisadi kiasi gani lakini leo kila kitu kipo wazi. Nakumbuka siku jina lake linapitishwa dodoma ilikuwa ni jioni nikiwa na collegues ofisini tukipiga simu kwa jamaa zetu waliopo dodoma kutueleza kinachoendelea. Taarifa ilivyokuja kuwa amepitishwa niliugua ghafla na wiki nzima sikuwa kwenye mood ya kufanya kazi. Sio siri ni vibaya kumuombea mtu kifo ila kwa uchungu niliokuwa nao niliomba lolote litokee huyu jamaa asiwepo kwenye uchaguzi 2005.
Inauma sana kila ninapokumbuka kwamba tulifanya maamuzi ya kukurupuka wakati chaguo sahihi tulikuwa nalo. Natumai sasa Watanzania tumejifunza kutokana na makosa hatutarajii kurudia kosa kubwa kama hili linalogharimu uhai wa watanzania wengi hv sasa na wengi wetu kukosa matumaini maana hatuna pakushika wala kuegema. Ni hatari kwa kweli.
Mkuu: Nakukumbusha pia kuwa CCM ya Mwalimu si kama ile ya Mwinyi na si kama ya Mkapa wala hii ya magamba ya Kikwete!
TIP:
this is forum, usionyese ufundi wa kuandika, hapa mtu akifungua post anataka aone point moja kwa moja, be STRAIGHT, mtu hawezi kufatilia para hadi ya tatu bado kabla ya kuelewa point yako
</p>Hakika hili liwe fundisho kubwa kwetu na tusirudie makosa.
TIP:
this is forum, usionyese ufundi wa kuandika, hapa mtu akifungua post anataka aone point moja kwa moja, be STRAIGHT, mtu hawezi kufatilia para hadi ya tatu bado kabla ya kuelewa point yako
Wewe ndio Mtikila?TIP:
this is forum, usionyese ufundi wa kuandika, hapa mtu akifungua post anataka aone point moja kwa moja, be STRAIGHT, mtu hawezi kufatilia para hadi ya tatu bado kabla ya kuelewa point yako