Uliponiambia kuwa hawezi kazi niliamini lakini sikujua kuwa hawezi kwa kiwango hiki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uliponiambia kuwa hawezi kazi niliamini lakini sikujua kuwa hawezi kwa kiwango hiki!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dumelambegu, Apr 30, 2011.

 1. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote, zilianza tetesi kuwa amepanga kuchukua fomu. Nilishtuka na kuwaza sana maana nilitambua vizuri utendaji kazi wake tangu akiwa kwenye ngazi ya chama. Kabla fikra hizo hazijanitoka kichwani, nikapata taarifa kupitia kwenye luninga ikionyesha wanafunzi wa UDSM Mlimani wakiwa wamejitokeza kwa wingi wakimtaka achukue fomu agombee kukikalia kiti cha enzi kwani ndiye aliyekuwa tumaini lao.

  Kabla kichwa hakijatulia kutafakari hayo ya wanafunzi wa Mlimani, nikapata habari kupitia kwenye vyombo vyote vya habari kuwa tayari amechukua fomu. Mwili mzima uliishiwa nguvu. Nilijiuliza kuwa imekuwaje nchi hii imefika mahali hata mtu wa aina hii ajisikie kuwa na sifa ya kukalia kiti cha enzi.

  Nilimwita mke wangu ambaye hakuwa na interest ya mambo ya siasa lakini kwa hilo ilibidi nimshirikishe kilichokuwa kinaendelea. Kwanza alicheka halafu akaniuliza kwamba kwa nini hupendi akalie kiti cha enzi? Nilimwambia mke wangu sababu mbili. Kwanza ni uwezo wa kazi yenyewe na pili kwa tabia yake niliyokuwa naifahamu vizuri nilijua fika kuwa haendani na hadhi ya hicho cheo.

  Mke wangu alinitupia swali ambalo angalau jibu lake lilisaidia kuongeza nguvu kwenye mwili wangu. Aliniuliza kwamba nina uhakika gani kwamba atashinda. Mbona kulikuwa na watu wengine waliochukua fomu. Nilifakari swali la mke wangu na hatimaye nilijipa matumaini kuwa kuna uwezekano angeishia njiani.

  Miongoni mwa watu waliochukua fomu alikuwepo mtu ambaye utumishi wake ulikuwa wa kutukuka ndani na nje ya nchi, mzalendo na anayeendana vizuri na hadhi ya hicho cheo. Walikuwepo wengine lakini huyo ndiye aliyeniongezea nguvu na kufufua matumaini yangu kuwa taifa hili lisingeishia kuongozwa na mtu ambaye kwa vigezo vyovyote vile hafai.

  Lakini siku zilivyozidi kusonga mbele, ndivyo nilivyoendelea kusononeka kwani vyombo vya habari viliongeza kasi ya kumsifu asiyestahili na kuwaponda wanaostahili.

  Hatimaye siku ya siku ikawadia ambapo vikao maalum vya chama vilianza kufanya mchujo wa waliochukua fomu. Ilianza Kamati Kuu. Ilipoibuka na majina, akapita asiye na sifa na mwenye sifa. Ikafuata NEC, kwa mara nyingine tena, asiye na sifa na mwenye sifa wote wakapita.

  Ndipo ukaja Mkutano Mkuu, uliouwa tumaini langu. Mwenye sifa na hata wengine ambao angalau walikuwa nazo, walitupwa chini na asiye na sifa ndiye akapewa rasmi kibali cha kupeperusha bendera ya chama chake akiwa mgombea wa nafasi ya kiti cha enzi.

  Tukio la Mkutano Mkuu kumpitisha asiye na sifa halitanitoka kamwe kichwani mwangu. Hakika moyo wangu uliumia. Niliwaza na kuwazua, nilisononeka na kuishiwa nguvu. Yote hiyo ni kwa sababu nilijua bayana kuwa hawezi kazi na mbaya zaidi mwenendo na hulka yake havifanani na hadhi ya kiti cha enzi.

  Mke wangu alijaribu kunipoza kwa maneno mbalimbali kama vile 'you never know, he might change and do wonders beyond your expectations' lakini wapi nilijua nchi imeliwa.

  Leo hii, akiwa ametimiza miaka takriban sita tangu akalie kiti cha enzi, hakuna mwananchi hata mmoja asiyejua kuwa nchi imeyumba katika nyanja zote za maisha. Mambo yanaendeshwa kana kwamba nchi haina kiongozi.

  Hatimaye, juzi tukiwa tumetulia tunaangalia luninga, mke wangu alitamka maneno ambayo nimeyaweka kama kichwa cha thread hii kwamba ''uliponiambia kuwa hawezi kazi niliamini, lakini sikujua kuwa hawezi kwa kiwango hiki'.

  Tafakari.
   
 2. Mkenazi

  Mkenazi Senior Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mti mbaya huzaa matunda mabaya na mti mwema huzaa matunda mema, CCM ndiyo mti wenyewe (Ni system).
  Hata awe nani, akitokea hicho chama ni balaa.

  DR. Slaa alisema kuichagua CCM ni kuchagua balaa. Na kwa sababu system yao ni mbovu tutaishia kuongozwa na personal character na si vinginevyo.

  Dawa ya Tanzania sasa hivi si kubadili sura kutoka chama kilekile kilichodumu miaka 50, tunataka tubadilishe Chama cha kutawala.

  All things must change to something new, to something strange.
  Henry Wadsworth Longfellow (1807 - 1882)
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Dume unatukumbusha mbali sana,maana kama mtu uwezo wake wa kuongoza wizara ni mdogo inakuwaje anapewa litaifa likubwa hivi?

  Hivi ni vigezo gani hasa sisi watanzania tunatumia kumpima mgombea? Marekani wanatumia IQ ya mtu na uwezo wake wa kuelewa mambo.
   
 4. U

  Uswe JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  TIP:
  this is forum, usionyese ufundi wa kuandika, hapa mtu akifungua post anataka aone point moja kwa moja, be STRAIGHT, mtu hawezi kufatilia para hadi ya tatu bado kabla ya kuelewa point yako
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  si kazi yangu kumsemea mtu lkn kauli yako ina walakini. Mleta mada kaeleweka. Back to topic. Hata mi nilishangaa kina mbowe wanagombea ili iweje wakati jk anakubalika kuliko maelezo. Japo nilimpa cdm, nilikuwa na imani fulani juu ya jk. Now i wish angekuwa japo salim
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tulikamata kimeo meeen.sasa inakula kwetu meeen.
  sikio la kufa halina dawa meeen.
  nashauri kama taifa tukae tujiulize nani walitusababishia hili,tujipange upya ni sawa na familia mnasubiri mtoto azaliwe sasa anazaliwa mwenye utindio wa ubongo.mtamwua? hilo haliwezekani.
  tusubiri mimba nyingine tuwe makini tusilewe ndipo tutunge mimba.
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Natilia shaka uwezo wako wa kufikiri... siwezi kukutofautisha na mhusika mkuu katika uzi huu...
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu nakukumbusha kuwaa Dr Slaa alitokea CCM!!!!
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Wengi tunajuta mwanaaaa. Mimi ni mmoja wa watu wa UDSM walioandamana na kufurika pale Diamond Jubileee na Ma t shirt ya ccm kumshangilia jamaa. Tulibeba mabango tukiomba tuongezewe boom kutoka 2500/= hadi 5000/= tukiimba nyimbo za chama lakini tulichoambulia baadae ni kupigwa virungu na mabomu ya machozi kule maeneo ya Survey tukidai kuongezewa boom. Lakini hadi naondoka pale hatukupata kitu. Tumshukuru Mungu kwamba ndugu zetu sasa hivi wana nafuu japokuwa ni kama vilevile maana % zimezidi. Ndugu yanguuuu tunajutaaaaaaa. Nikaja kugundua kuwa hata msomi anaweza kuchagua embe bovu sababu ya njaaaaa. Sasa hivi nikimuona nakasirikaaaaaaaaaaaaaa alfu natulia mwenyewe najinywea viroba siku ziende fasta aghhhhhh. Njaa sometimes inapelekea wasomi kutoa maamuzi ya ajabu. Mie nilichapa makala kule Tazama Tanzania kumsifu jamaa na kuwaponda wengine ila sasa natubu!!! Sikujua kama niliingia mkenge. Sasa hivi magwanda nsha vua. Mapinduzi halisi tunayetegemea kutoka nje ya ccm. Alichoniudhi ni kukaa kimyaa na aliponichefua ni kusema kuwa haijui Dowans.!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Josephine

  Josephine Verified User

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 787
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Umenigusa sana, nakumbuka pia 2005.
  Thx.
   
 11. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hiyo nimeipenda.
   
 12. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Usikurupuke ndugu yangu. Hivi hujui kuwa kabla ya 1992 hakukuwa na chama chochote cha siasa hapa nchini zaidi ya CCM?
  Shida hapa ni kwamba walikimbia mfumo mbaya wa uendeshaji wa nchi ndani ya CCM na kujaribu kuja na plan B.
   
 13. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Watanzania tunajijengea uvivu wa kusoma kwa kasi ya kusikitisha.
  Ndio maana rais wetu alikamatishwa hundi feki na EXIM bank kwa sababu ya uvivu wa kusoma.
  Pia hatupendi kabisa tupewe jambo kwa namna ambayo inatufanya tufikirishe bongo zetu.Kila jambo eti liwe straight.
   
 14. n

  nguluvisonzo JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 511
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtangulizi hakupenda aende Magogoni ni wazee wa heshima ndani ya chama walisimamia hilo. Mmoja wapo ni huyu wa Kilimanjaro ndio wenye nguvu ndani ya chama kwa kuwa ni kipenzi cha watu.

  Sasa hivi wametulia kimya hawawezi hata kusema neno, mambo yanazidi kuharibika, sasa hata mimi nimejua ni kwa kiwango gani mtangulizi aligundua hawezi kazi.
   
 15. g

  gepema Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dume la mbegu hii kitu inanikumbusha mbali sana maana nakumbuka enzi hizi na mimi nilikuwa undergraduate jamaa yangu mmoja akawa anamponda sana mwenye kiti cha enzi huku akisema ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya lakini hatuambii kama ni kwenda mbele au kurudi nyuma so tuwe makini isije kuwa ikawa ni kurudi nyuma kwa ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya!
  Game lilipoanza tu nikaona yale maneno yanaanza kutimia leo tuko wapi mbele zaidi au nyuma zaidi?? Changanya na za kwako
   
 16. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  -Uswe, usituzungumzie wote, wengine hupende kusoma-ni sehemu ya hobby- kama mwenzetu ni mvivu kwenye hilo, pole sana.

  -Dumelambegu, nimetafuta kile kitufe cha 'like' na cha 'thank' sijaviona, nilitaka nikugongee kwani hii nimeipenda
   
 17. Greek

  Greek Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenikumbusha mbali sana mkuu, siku nilipojua kuwa hicho chama kimekufa rasmi walipompoteza salim wakamchagua mtu kwa kufuata ushabiki, na sasa wenye akili wanaelewa na kujuta, naam na bado watajuta sana tu. Coz its too late.
   
 18. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Baada ya kuiona si ile aliyoiamini kama wengine wengi walivyo na wanavyoendelea kutoka CCM..
   
 19. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Majuto ni Mjukuu, tuangalie mbele, aluta continua!!!!

  Hata na akina RACHEL wanajuta kumfahamu huyu jamaa. Kotekote sasa kaharibu.
   
 20. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  EEEE!
  MKOME KUFUATA MIKUMBO!
  ATI OOH, CHAMA CHA BABA NA MAMA YANGU SIWEZI KUKIACHA!
  HATA JULIUS ALIWAHI SEMA "CCM SIO MAMA YANGU" :smile-big: HA HA!
   
Loading...