Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Funga domo lako usinisababishie nafungiwa jf, funga bakuli lako hujui watu tumeumia kiasi gani.
Mimi ni mtu wa kawaida kuna watu humu tunajuana face to face. We mjinga ungekuwa karibu yangu ningekudunda mbaya kwa hasira nilizo nazo.
Mamilion wanalia kwa ajili ya jpm wewe unaongea ujinga, hivi unajua jpm alikuwa muhimu kiasi gani?
Unajua nini maana ya uongozi wewe?

Akili kisoda wewe.
Na mamilioni ni vice/versa R.I.P in advance
 
Alifariki Baba, alifariki Mama nilihuzunika sana tu bila kutoa chozi.
Ila kwa JPM chozi lilinitoka kwa huzuni kubwa huku mapigo ya moyo yakiwa juu sana.
Hadi leo bado ninahuzuni.
Mama,Baba..Mtu baki
 
Kwanza tangu nione Kigogo anaongelea hilo twitter, nilianza kuwa mtazamaji mzuri wa TBC.
Kisha nikadownload ule wimbo wa "hakuna Mungu kama wewe Bwana" nikawa nausikiliza taratibu na ule "Yupo Mungu mbinguni ajibuye maombi yetu".

Siku inatangazwa nilikuwa nimeweka TBC kwa hiyo niliipata pale pale. Nikajikuta naropoka hatimaye. Nikaweka ngoma yangu ya " Hakuna Mungu kama wewe bwana" nilisifu mpaka saa 10 usiku.
Mimi shem wenu alijuta kuniamsha kunipa taarifa. nilimpa show ya hatari, nilimpa yote niliyofundishwa na somo that day...i was happy.
 
Mimi niliacha clouds fm on nikalala kwenye kisita hivi mara nikasikia nyimbo za maombolezo nikastuka sana nikajua kuna kitu nikazima radio ni kaja kuwasha saa nane nikaona bado zinaimba nikabadili tbc mara nikasikia magufuli aliwahi kuwa waziri wa ujenzi nikazima radio, sikulala usiku kucha yaani hamna amani moyo kuuma tu , nilikuja kuwasha tv na radio kesho yake saa kumi baada ya kuona watu wameongea sana nilikuwa natetemeka sana tu sitosahau
 
Usiku kucha nilikuwa napigiwa simu na watu mbalimbali, ila kwa kuwa simu yangu huwa inajiweka don't disturb kila inapofika sa nne usiku hivyo sikuweza kusikia simuzao.

Asubuhi naamka nakuta jirani kafungulia sabufa sauti kubwa,,,. Ule wimbo wa tutaonana tena (Goodluck Gozbert)…..
Kama ilivyo kawaida nikachukua simu nikaanza kupekua mtandaoni......
Dahhh ndo nikakuta taarifa
Aisee sikufichi nililia sana

JPM amehusika kwa namna fulani kunikwamisha kimaisha but alikuwa mzalendo wa kweli kwa nchi yake
He was a Legend for his country but not all of his citizen

Ukweli kama mimi nilishazoea maisha ya ujanjajanja,,,. Sasa JPM alikuja na mifumo yake. Ilinikwamisha sana aisee,,,,,. Atleast now mambo yameshaanza kurudi kama zamani

Rest Easy Legend
 
Watu tunazika watu wetu kwa corona kila siku halafu yeye anasema Tanzania haina corona! Alistahili sana kufa kwa corona hiyo hiyo.
Msipende sifa na kuitajataja corona hiyo unauhakika kweli hao watu walikufa kwa corona???! Furahia sasa magu hayupo ndio muda wako ila ukikuwa kiakili utamkumbuka baada yakuona mazuri yake, r.i.p mwamba kutokea chato
 
Umelala yoooo

Mchana nilikuwa napiga story na mzee flani kitaa tukawa tunasema kwa kauli za samia kweny hotuba ya tanga
Akuna usalama kabsa,.

Usiku nilistuka midaa ya SAA sita hivi nikaingia insta kila page nikakuta RIP

Sikustuka sana maana kwa uvumi ule nilijua tu jiwe kashaendaa ,nikawa nawazoom tuwanafiki kule insta ,waliokuwa wwanawabishia wambea
 
Hiyo siku nilikuwa nimepiga k-vant kubwa nikasema nipumzike nje kidogo ili nisiwasumbue wa ndani, bahati mbaya usingizi ukanipitia.
Nakuja kushituka nakuta wapangaji wapo nje wanalia. Nikajua labda nilizima, walivyoona siamki wakajua nimevuta.
Nikaamua kuamka ili kuonesha mi ni mzima, nikaona hata hawana mpango na mimi. Ndio kuna jamaa akatamka kabisa kuwa Magufuli kafariki.
🤣🤣🤣🤣 Fala wewe
 
Nilihisi ka_relief kamoja kazuri sana rohoni kwangu - niwe mkweli tu... kuna watu wameumizwa sana na huyo jamaa hadi leo bado wanalilia mioyoni mwao.
 
Azoe huko aliko na asirudi tena. Alijaa hamu ya kutoa roho za watu. Ya kwake ikatwaliwa pia...
Msipende sifa na kuitajataja corona hiyo unauhakika kweli hao watu walikufa kwa corona???! Furahia sasa magu hayupo ndio muda wako ila ukikuwa kiakili utamkumbuka baada yakuona mazuri yake, r.i.p mwamba kutokea chato
 
Ilinikuta kama kawaida yangu kuamka 11asubuhi kuomba hasa kumuombea yeye baada ya siku chache kuota ndoto mbaya iliyomuhusu. Nimekaa chumba kingine nisiwapigie kelele waliolala naona meseji inaingia kwenye kisimu cha tochi '' Poleni kwa msiba raisi Magufuli amefariki'' ikabidi nitafute wapi ilipokuwa smartphone yangu naingia facebook nakuta kuna nabii Kasunga karepost ujumbe wa utabiri wa kifo cha Magufuli alioutoa hapo kabla, dah nilichukua dakika kadhaa machozi tu kidume yanatoka, wife akaamka mida hiyo kama 12 akakuta nishawasha na tv kabisa alivyoiona habari machozi yakamtoa japo halikuwa hamkubali kabisa, ilikuwa experience ngumu sana kwangu binafsi.
 
Ile siku sitaisahau, nakumbuka since tarehe 06/03,ulizuka uzushi mkubwa uko jamuhuri ya Tweeter kuhusu afya ya Magufuli.

Basi siku ya tarehe 17, nkatoka jobs, SAA nne usiku nkalala,. Wakati nimelala nilisikia simu inaita Ila kutokana na wenge la usingizi sikuipokea,, baada ya dakika 10, nilipigiwa Tena simu,, na mshikaji wangu mmoja, namnukuu " oya jamaa Meko amefariki"

Ukweli sikumpenda Magufuli Ila nilishtuka hatari, Basi muda huo kuingia Tweeter, nakuta ni sherehe kwa baadhi ya wadau wa Tweeter.

msiba ukinikuta Niko Arusha, nimelala.

Vipi wewe mdau ulipataje habari za msiba huu, na ulikuwa wapi.
Nlikuwa Hostel nasoma Usiku Dah Nkaanza kuamsha masela huku machozi yananitoka
 
Back
Top Bottom