Ulipokeaje na ulikuwa wapi siku ya tarehe 17 Machi, kifo cha Dkt. Magufuli

Mimi sitaniii nilikua na demu ' mchepuko' ambaye si CCM damu damu!

Tena nilimuomba simu yake niangalie Instagram ( yangu ilikata moto).

Ile nafungua data na kwenda instagram nikamuona Mama anatangaza!!! Kwakweli yule mchepuka alinishangaa sana namna nilivyo fanya ( sidhubutu kuandika hapo naweza fuatiliwa) kwa yeye ni mataga og mimi ni mpinzani sio siri niliharibu bajeti ya wiki mbili ndani ya masaaa matatu
 
Me nilikuwa v lounge, moshi town, nakula vyombo na mchuchu, sina hili wala lile, mara simu inaita, na mziki, nikasema bro ni nn usiku usiku na misimu.
...
Next day mbuzi wangu nilipeleka ahera madukani

IMG_20210604_171944.jpg
 
Nilikuwa Mkoa fulani nafanya task fulani ya wizara fulani, ule usiku nilikuwa hotelini nimelala ndipo nilopopokea simu kutoka kwa mtu wangu wa karibu.

Vile nilikuwa nimetoka usingizini siikuelewa na yeye alikuwa ameshakata simu na kila Nikimpigia tena simpati ghafla nikasikia kilio Kikubwa cha mwanamke kwenye ile hotel ndipo nilipotoka kuuliza kwani kuna nini?

Hapo ndio nilipata taarifa rasmi kwa upana na kwa mstuko ule wa taarifa nilijikuta hadi nimepata na Period..
 
Nilikuwa Longido kikazi. Nataka nilale nikatumiwa sms kwamba mzee amefariki. Sikuamini basi nikabidi nimpgie jamaa yangu nimuulize, nikajibiwa ndio nisubiri Habari tbc...
Na leo ww ip mob umetangulia pumzika kwa amani mkuu
 
Nilikuwa Chanika. Nililala Chanika siku Ile. Asubuhi nikamfuata jirani yangu nikamuuliza," (excuse me)Hii I Tel yangu inasema nini sijui! Ati una habari gani kuhusu Magufuli. Ni kweli kwamba amekufa?"

Akaniambia hizo habari zimetangazwa jana saà tano usiku.
 
Nilikuwa Chanika. Nililala Chanika siku Ile. Asubuhi nikamfuata jirani yangu nikamuuliza," (excuse me)Hii I Tel yangu inasema nini sijui! Ati una habari gani kuhusu Magufuli. Ni kweli kwamba amekufa?"
Akaniambia hizo habari zimetangazwa jana saà tano usiku.
Mimi nilikuwa zangu Rwanda king kazi, by SAA tano usiku kwa SAA za kule Mara mfanyakazi mwenzangu anapiga simu room kwangu namuuliza vipi eti alikuwa analia namuliza Bob vipi ooh JIWE LIMEPASUKA. Nikakata simu nikalala zangu.Ahahaahhaa..
 
Hiyo siku nilikuwa nimepiga k-vant kubwa nikasema nipumzike nje kidogo ili nisiwasumbue wa ndani, bahati mbaya usingizi ukanipitia.
Nakuja kushituka nakuta wapangaji wapo nje wanalia. Nikajua labda nilizima, walivyoona siamki wakajua nimevuta.
Nikaamua kuamka ili kuonesha mi ni mzima, nikaona hata hawana mpango na mimi. Ndio kuna jamaa akatamka kabisa kuwa Magufuli kafariki.
Nimecheka
 
Marehemu alikuwa jiwe kweli kweli maana sio kwa Sokomoko lile..
Apumzike anapostahili
 
Nilikuwa zangu ghetto, mara status zikaanza kufurika RIP ikiambatana na picha ya Magufuli. Niliumia sana, hadi nilitokwa machozi. I had never known nilimpenda Magufuli kiasi kile.
 
Nilikuwa Longido kikazi. Nataka nilale nikatumiwa sms kwamba mzee amefariki. Sikuamini basi nikabidi nimpgie jamaa yangu nimuulize, nikajibiwa ndio nisubiri Habari tbc.
Baada ya hapo nilienda kulala mida ya saa 4 kasoro usiku, ila niliweweseka kwa mawazo (sikutaka kuamini kabisa) mpaka saa 6 ndio nikapata usingizi.
Asubuhi naenda field karibia kila mtu hakuwa na furaha hata wale wakosoaji.
Rip mdau daah nawewe umemfata magu😭😭
 
Nilikuwa Mkoa fulani nafanya task fulani ya wizara fulani, ule usiku nilikuwa hotelini nimelala ndipo nilopopokea simu kutoka kwa mtu wangu wa karibu. Vile nilikuwa nimetoka usingizini siikuelewa na yeye alikuwa ameshakata simu na kila Nikimpigia tena simpati ghafla nikasikia kilio Kikubwa cha mwanamke kwenye ile hotel ndipo nilipotoka kuuliza kwani kuna nini!? Hapo ndio nilipata taarifa rasmi kwa upana na kwa mstuko ule wa taarifa nilijikuta hadi nimepata na Period..
na period juu
 
Hivi nyie mnaoshangiria kifo cha Magufuli, Mshajiuliza kwa nini reply zenu zinapata like chache? Kuliko zile reply za wanaonesha kuhuzunika kutokana na kuondokewa jemedari Magufuli.
 
1629834583808.png
Japo wapo watakaochukia picha na wazo hili, pia wapo watakaofurahia kumbukizi hili. Jamaa alilaumiwa kwa mengi pamoja na kufanya mengi.

Sasa hayupo na mengi yanasemwa kuhusiana na waliomrithi. Je wewe kama mtanzania usawa huu wa tozo na kesi za ugaidi usio kichwa wala miguu, unammiss huyu mwamba au la?

Nashauri mchangie kwa staha na si matusi wanangu. Hebu tujikumbushe enzi zile na hizi tuweze kutafuta majibu ya maswali ambayo hadi sasa hayajapatiwa majibu. Kila la heri wanangu.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom