Ulipata milioni yako ya kwanza ukiwa na umri gani? Ulipataje?

Binafsi miaka 30 sasa ni mtu wa Kujaribu Jaribu vitu vingi ( ideas ) hivyo nikipata laki 2, 3 au 4 najaribu kitu kipya.

Kukusanya Milioni NET nikawa nayo mkononi SIJAWAHI kwasababu siyo muumini wa Saving na sijawahi kupata Deal la kulipwa pesa hiyo.
jifunze kusave mkuu kama huna dili za pesa ndefu, ukipata hizo lakilaki kabla hujapanga chochote toa hata 50 peleka mahali huwezi ichukua kabisa.

Mimi nilikua na lain ya airtel money nilimpa maza aitunze na asinipe under no circumstance, wala nilikua sijui anaitunza wapi. Nikawa nikipata tu hela, kabla sijaitamani na kunua kitu natoa kiasi kadhaa naideposit kwenye lain inayobaki nachafua ninavyojua. Baada ya kila miezi 3 maza alikua ananipa najikuta nna laki nne hadi 8, ndo nakaa nawaza sasa hii hela itanizalishiaje zingine, huku nikihakikisha cashflow inaendelea kuwepo. Mana adui wa akiba ni ukate mrija wa cashflow, utaitumia tu
 
tunafanyaje mzee tushike maana naona tunalingana kwa kila namna
nadhani mtakua nyumbani, step ya kwanza toka nyumbani ujue bills, ujenge discipline ya hela, yani ujue kutafuta na kutumia vizuri pesa,jiweke karibu na watu waliotoka ama wenye michongo weka aibu pembeni. Jitume mtoto wa kiume mana kuna watu watakutegemea siku moja.
 
Umenifanya nicheke sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli mimi nimeshashika pesa nyingi sana, ila less than 40 million. Nilichojifunza ni kuwa sina nidhamu na pesa, nilishazoea kupata pesa kirahisi hivyo huwa sina akiba au ni kidogo sana. Sasa huyu baba lao Corona umeniumbua sana, dili hakuna tena na mfukoni sina kitu, mshahara bado sana. Sijui mwisho wa mwezi ntafikaje, ndugu zangu jifunzeni nidhamu ya pesa. Sasa hivi namiliki shilling 300 yani mia mbili plus mia mbovu niliyoiyokota chumbani. Hahaahahaha hahahahaha unaweza dhani masihara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah kweli nidhamu ya pesa ni muhimu sana, unapata pesa unalipa watu wengine tu hadi inaisha-unamlipa mangi, unalipa bar, unamlipa mwenye nyumba, unalipa maduka ya nguo,s/market, na sehemu zote za bata unalipa. Kasoro unasahau kujilipa wewe kwa kuweka akiba.
Mtu mmoja nilimsikia akisema, you are not rich because of how much you earn, but how much you keep for yourself. Apo ukute mtu hajawai kuearn hata laki tano cash ila ana savings ya laki nane, wakati wewe mwenye uwezo wa kupiga deals za mamilioni kuna siku unaamka huna kitu kabisa
 
Kilitokea nini mkuu, tupe hiyo story tujifunze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuelezee ilikuaje miaka 19 wengine hata hela ya boom hawajashika wewe 17 ushashika kiasi hicho
Maana koments zako zinanipa controversy flni, mara milio 40, mara 6, mara 4, hebu tueleze kinagaubaga

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiwa na miaka 17 nilipewa 4 M kama urithi baada ya baba kufariki. Nilipofikisha miaka 19 nilianza biashara ya kukopesha pesa wakulima wa tumbaku amapo nilipata faida mpaka ya 1.3 M. Pamoja na kuja kishika pesa nyingi baadae lakini sijawahi kuzidi 40 M. Vp hapo umenielewa au niongeze sauti?
 
Tuelezee ilikuaje miaka 19 wengine hata hela ya boom hawajashika wewe 17 ushashika kiasi hicho
Maana koments zako zinanipa controversy flni, mara milio 40, mara 6, mara 4, hebu tueleze kinagaubaga

Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiwa na miaka 17 nilipewa 4 M kama urithi baada ya baba kufariki. Nilipofikisha miaka 19 nilianza biashara ya kukopesha pesa wakulima wa tumbaku amapo nilipata faida mpaka ya 1.3 M. Pamoja na kuja kishika pesa nyingi baadae lakini sijawahi kuzidi 40 M. Vp hapo umenielewa au niongeze sauti?
 
Huu ni ukweli mchungu. Tubadili tabia
 
Niliipata nikiwa chuo ifm ,nilipewa ada na mama wakati mm nilikuwa nalipiwa na serikali (mama hakujua) ,nikanunua vyumba hostel ifm kipindi hicho hostel dili kinoma ,nilinunua vyumba vitatu kwa laki 6 kila chumba kina vitanda vi 4 ,kila kitanda wanalala watu wawili na kila kitanda unapangisha per person
300,00×2 =600,000
600,000×4=2,400,000
2,400,000×3=7,200,000 that was second year
Nikamchimbia kisima mama yangu ,she was able to earn 15,000 kwa siku minimum kwa kuuza kwakuwa alipokuwa anakaa palikuwa na shida ya maji

3rd year ilikuwa hatari ....nilipiga mpaka 10m no one knew niliifanya kwa displine kubwa nikarudi post graduate i did the same

Nikaja shtukiwa na warden nilivyomaliza post nikafanya kwa faida ndogo baadae soko la vyumba chuo likawa sio dili baaada ya wanafunzi wengi kuprefer kigambon na hostl za nje ...nami nikawa nafanya bznes huku naajaliwa ,nikaona upuuuzi nw naendelea na biashara maisha yangu si makubwa saaaana lakini nimaisha ambayo wengi wanayatamani ,napata changu ,napata cha kusomesha ndugu zangu sidaiwi kodi ,nabado nasave hela mara 5 ya mshahara niliokuwa napewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa na miaka 22 moshi Kilimanjaro nilikuwa nafanya kazi za kubeba mizigo milimani, tukawa tunabeba mizigo na kufanya biashara ya t-shirt na bracelet kwa wazungu, nikameki ad ikafika dollar 900.. Million mbili ivi. Nikampatia ujauzito girlfriend wangu akajifungua malezi yakawa makubwa mara dogo aumwe mara kodi mara kazi zikawa ngumu mliman na biashara ikazuiwa tena. Imebaki kama historia ata laki moja nimeimiss now. Inaniuma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ilo jina lako linafurahisha na maelezo yako, ila ya kwanza huwa haidumu mkuu, ila inakupa mwangaza kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…