Habarini za jumapili ndugu zanguni, Leo ni jumapili ya kwanza ya kwaresma, hakika neno la leo lilikua zuri sana,
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu hii ya leo, ni jambo la kushangaza lakini pia la kifikirisha sana, baada ya kuongea nao kwa nyakati tofauti tofauti, nimegundua rafiki zangu wote niliosoma nao hakuna aliyepata nafasi(kazi) kwa bahati wote walifanyiwa mchongo(walishikwa mkono), nimefikiria sana
Nimewaza hivi wale watoto wa maskini ambao huomba kazi kwa dua mamia kwa maelfu wao hupataje kazi, hasa kazi za kueleweka, au wao huongozwa na bahati, ama kweli mwenye nacho ndiye huongezewa
Rafiki zangu hawa wapo waliosoma hapo Loyola, Alpha, Feza na wachache shule za serikali(Advanced level) n.k
Yaani kuna mmoja alisoma uboyzini shule moja ya kibabe alivyomaliza direct akapata kazi nzuri sana na kwenda nje ya nchi, nikajua zali, la haula kumbe naye kulikua na mkono wa mkubwa anayeishi pale mbweni, aliniambia mwenyewe, nikastaajabu. Kuna siku nilikutana na mzee mmoja mzito sana tukawa tunapata moja moto moja baridi, maongezi yalivyokolea akaniambia sasa hivi zimerudi tena zile zama za simu moja, unamjua nani, yaani huko unapotaka kuajiriwa una mtu, hata wale waendao kule Moshi, Monduli, bagamoyo si kwa bahati tena, lazima ushikwe mkono.
sasa najiuliza circle ya uongozi na watendaji inakua ya watu wanojuana tu, je wale watoto walioko huko Nkasi, Namanyeri, Nanjilinji n.k ambao wazazi wao wanawasubiri wamalize waajiriwe wawasaidie (dhana) itakuaje..? wanajua kama huku mjini ni weka kitu upate kitu,
Na wewe ndugu msomaji unayesoma hapa, hebu sema ukweli kutoka rohoni mwako, kama ulibahatika kupata kazi(kuajiriwa) iwe government au private, hiyo kazi uliipata kwa njia gani..?
May this Lent be a season of grace for you and your loved ones!