Ulipata milioni yako ya kwanza ukiwa na umri gani? Ulipataje?

Harry singo

JF-Expert Member
Apr 24, 2016
352
437
Habari zenu jamani,

Bila kupoteza muda nijikite kwenye mada.

Mada hii nimeiweka hapa ili tujadili kwa ajili ya kuhamasishana na kujifunza pia. Sio kwa ajili ya kusema mambo ya kufikirika yasiyo na tija ambayo hayatamsaidia mwanajamvi yoyote kuokota kitu.

Niwaombe unapo comment, tuelezee kidogo ili uzi uchangamke na watu wajifunze hasa vijana ambao bado wapo kwenye hustle pamoja na kuwatia moyo wale waliokata tamaa.

Mimi binafsi ni moja kati ya watu ambao hawakuwa na bahati ya kuishi maisha ya ushuani, nilizaliwa na kukulia naweza kusema uswahilini tu japo sio kwenye uswahili ule tunaoujua wa sasa.

Sikubahatika kusomeshwa na wazazi hadi Chuo Kikuu, walinisomesha hadi form 4, nikaingia mtaani kupambana nikajiendeleza mwenyewe nina BA ya fani fulani kwa sasa.

Baada ya kumaliza Form four niliingia mtaani na kujichanganya na mafundi wa ujenzi nikiwa bado naishi nyumbani kwahiyo niliweza kujinunulia mahitaji yangu tangu hapo, nikashika kila kibarua kilichoingiza pesa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi viwandani kwa posho ya kuanzia 2900 kwa siku, nilipoacha kazi za viwandani nilikua nimefikia kwenye posho ya 7000 kwa siku. Hizi zilikuwa kazi ngumu sana. Ila zilinijenga na nikajua kwamba hakuna kinachotokea bila sababu.

Kwanini nimesema hivyo, kwa sababu kila kiwanda nilichopitia niliondoka na ujuzi fulani ambao ulinifanya baadae nije kuanzisha miradi mbalimbali.

Baada ya kuchuma kwenye jua la saa sita kwa muda mrefu nikapata kibarua kwenye kampuni ya wahindi ambao walinipenda sana, (tofauti na msemo wa kusema wahindi watu wabaya, mimi nilikutana na wazuri)

Nikapanda chati kidogo nikawa napokea 200,000 kwa mwezi na kutokana na uchapa kazi nikaongezewa ikawa 250,000 pamoja na nauli na chakula pembeni. Ni wakati huu ndipo nilipojichanga nikajilipia VETA kusoma kozi fulani ya viwandani.

Alipoona nia yangu ya kusoma Mr. *** Bosi wangu alinipa mkopo isio na riba ili nijiendeleze hivyo nikaenda DP.

Tukio hili ni kwamba siku moja nilisahau begi langu kazini, na kwa hisia za kibinadamu akalifungua kuangalia ndipo alipokuta vitabu pamoja na makaratasi mengine ndio akaniuliza nini hiki, nikamwambia ukweli bosi mimi nasoma na ndio maana nilikuomba ruhusa niwe nawahi kutoka mchana, mwqnzo alikua na hisia zingine ila baada ya tukio hili alikaa kama wiki ndio akaniambia atanikopesha na atanipa likizo. Japo hatanilipa.

Kipindi cha kusoma nilihangaika sana. Nasoma narudi nyumbani nakula mzee akiwa hayupo narudi geto, kodi ikiisha nilikuwa nahangaika sana ila hiyo ni story nyingine.

Bahati mbaya yule Mhindi alikuja kufariki nikiwa nakaribia kumaliza na ndipo ndugu wa familia (watoto) wakanilazimisha nilipe mkopo ama nifanye kazi bila malipo kufidia.

Nashukuru Mungu nilivuka hicho kikwazo baada ya hapo nikahangaika sana kupata ajira sikupata pamoja na dp yangu. Nikatumia ujuzi niliopata kwenye moja ya kiwanda nikakopa kwa watu kama wanne nikapata laki 4 nikaanza kutengeneza bidhaa nazungusha madukani. Hii ilidumu kwa muda sana kama miaka miwili hivi nikawa na mtaji wa kama 800,000 hivi.

Nikaenda Manyara maeneo fulani yanaitwa Maole, ndanindani ya mbuyu wa Mjerumani nikalima mahindi heka moja nikapata gunia 7, na soko halikua zuri soko. Ile hela ni kama nikaizika.

Nikarudi mjiji nikafanya kila kilichingiza hela halali (ni story ndefu) lakini siku navunja boksi nilipata kama 368,000 kisha nikaomba mkopo wa 400,000 kwa rafiki yngu ambaye alikuwa Vicoba (alikopa akanikatia kiasi hicho) kisha nikarudi shamba safari hii nilipata 1,500,000

Hiyo ikawa milioni yangu ya kwanza.

Siku nyingine tutaongelea maisha baada ya milioni ya kwanza (usidhani ilidumu)

Nawakaribisha kujadili
Ni mimi Mfalme (ni jina tu)

(Angalizo: Unaposema kwa kifupi inapoteza maana ya uzi. Tuelezee kidogo. Ilikuwaje, ulikuwa na umri gani)
 
Nilipata nikiwa na miaka 22 biashara ikiwa dagaa nyasa..na vijiwe vya hapa na pale hiyo siku iliyotimia ilikua 27/1/2018 niliztandaza juu ya kitanda nikazilalia kwa furaha nikapiga picha nyingi sana baada ya miezi 3 ikafika 1.6M nikanunua boksa baada ya hapo kilichotokea sitaki kukumbuka kamwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipata mwaka jana mwezi wa 9 mwishoni. Hiyo ni baada ya form six watu kwenda jeshini nami najijua nilivyo kapuku jeshi nikapiga chini.
Nilipiga kazi mpaka nikakonda, mwendo wa kuamka saa kumi na kurudi nyumbani saa mbili usiku. Kazi zenyewe unasimama tu kasoro kupumzika saa moja tu.
Hiyo hela nilinunua vitu kadhaa maana sikuwa natafuta mtaji wala nini.
Kati ya hiyo milioni nilitoa kitu kama 80k pekee kwa ajili ya bata. Inaniuma sana sikuiwekeza sahivi naishi kwa mawazo.
 
Nilipata mwaka jana mwezi wa 9 mwishoni. Hiyo ni baada ya form six watu kwenda jeshini nami najijua nilivyo kapuku jeshi nikapiga chini.
Nilipiga kazi mpaka nikakonda, mwendo wa kuamka saa kumi na kurudi nyumbani saa mbili usiku. Kazi zenyewe unasimama tu kasoro kupumzika saa moja tu.
Hiyo hela nilinunua vitu kadhaa maana sikuwa natafuta mtaji wala nini.
Kati ya hiyo milioni nilitoa kitu kama 80k pekee kwa ajili ya bata. Inaniuma sana sikuiwekeza sahivi naishi kwa mawazo.


Rudi tena upige kazi mkuu
 
Tupe kisa, ilikuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Haina kisa insuch...bt nililigundua hili zao linahela kipindi cha kampeni 2015...watu walikua wanauza kienyeji tu ile kilocal local...nikaopt kuwatembelea wakulima nikanunua mashamba .2016 nikaamua kujitangaza kupitia social medias!nikapata ka tender kupeleka mikumi national parks kwa wazungu fulan...!
Nimeuza mno mno mno strawberies...had leo napigiwa simu ila niliacha nilipata ajali!
Kwa wanaouza sasa hv sidhan km wanapata faida ile ya shilling kwa shiling!..maana mikoa yote ya baridi nimeuza sana mbegu..!
 
Back
Top Bottom