Uliniua Gloria

Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
Mtunzi

*NYEMO CHILONGANI*
*ULINIUA GLORIA*

*Sehemu ya 01*

Kelele za shangwe zilikuwa zikisikika kutoka katika nyumba ya mzee Steven. Vigelegele kutoka kwa wakinamama vilikuwa miongoni mwa sauti za shangwe zilizoendelea kusikika kutoka ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imejengwa kisasa katika Mtaa wa Magomeni Kondoa.

Magari kadhaa yalikuwa yamekusanyika ndani ya eneo la nyumba hiyo, idadi kubwa ya magari hayo yalikuwa ya kifahari ambayo wala hakukuwa na mtu ambaye alishangaa kuyaona yakiwa yamepakiwa ndani ya eneo la nyumba hiyo.

Sauti ya muziki ilikuwa juu ingawa wakati mwingine ilikuwa ikipunguzwa kutokana na mtu yeyote ambaye alikuwa akitaka kuongea lake katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza Peter na Gloria ambao walikuwa wakitarajia kufunga ndoa mwezi mmoja baadae ndani ya Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge.

Wote ndani ya nyumba hiyo walionekana katika nyuso zilizokuwa na furaha, walipenda kuwaona watoto wao wakiingia katika maisha ya ndoa, maisha yaliyoonekana kutamaniwa na watu ambao walikuwa nje nayo lakini kuchukiwa na watu ambao tayari walikuwa ndani ya maisha hayo.

Gloria hakuwa mbali na Peter, muda wote alikuwa pembeni yake huku akipigapiga picha kwa kutumia simu yake katika kila tukio lililokuwa likiendelea mahali hapo. Kazi kubwa ya Peter ilikuwa ni kukishika kiuno cha Gloria, kumbusu mara kwa mara huku akimuachia tabasamu pana.

Baba yake Peter, mzee Steven alionekana kuwa mwenye furaha kubwa, muda wote alipokuwa akiongea, alikuwa akitabasamu tu huku akionekana kuzidiwa na furaha ambayo alikuwa nayo kwa kile kitu ambacho kilikuwa kinaendelea.

Katika maisha yake alibahatika kupata watoto wawili tu, wa kwanza alikuwa Rachel ambaye alikuwa amekwishaolewa na wa pili alikuwa Peter ambaye baada ya siku kadhaa nae angeanza maisha ya ndoa na msichana Gloria Michael.

Katika sherehe hiyo, wazazi wake Gloria, mzee Michael Mshama na Bi Justina walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wamekusanyika katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza kwa hatua ile waliyokuwa wameifikia.

Mpaka kufikia katika kipindi hicho, wao pia walionekana kuwa na furaha kubwa, hawakuamini kama binti yao, Gloria alikuwa akitarajiwa kufunga ndoa na baada ya hapo kuitwa mke wa mtu huku ukichukua muda mchache kabla ya kuitwa mama.

Gloria ndiye alikuwa binti yao ambaye walikuwa wakimpenda kupita kawaida, walimthamini na kumpa kila kitu ambacho kama wazazi walitakiwa kumpa binti yao mpendwa. Kwao, Gloria ndiye alikuwa kila kitu, yeye ndiye alikuwa tabasamu nyusoni mwao.

Ukaribu wa Peter na Gloria ulianza tangu walipokuwa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Mwalimu Nyerere huku baada ya kufika kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Benjamini wakaanza kuingia katika uhusiano wa kimapenzi. Ingawa walikuwa na furaha lakini uhusiano wao ulionekana kuwa na vizuizi vingi huku kizuizi kimoja na kikubwa kikiwa ni masomo.

Walitamani kufanya mambo mengi katika maisha yao kwa wakati huo lakini masomo ndio kilikuwa kizuizi kikubwa. Muda mwingi walikuwa wakitamani kusoma pamoja lakini kila walipojaribu kufanya hivyo, walijikuta wakianza kushikanashikana na hatimae kulaliana na kufanya mapenzi.

Kila mmoja kichwani alikuwa na ndoto yake ambayo alikuwa amejiwekea. Peter alikuwa na hamu kubwa ya kuwa Mchumi mkubwa hapo baadae huku Gloria akiwa na hamu ya kuwa Mwanasheria mkubwa hapo baadae. Kila mmoja alikuwa akiishi katika ndoto yake ambayo ilikuwa ikiendelea kukua kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.

Wakamaliza kidato cha nne na kukaa nyumbani kusubiri matokeo, yalipotoka, kila mmoja alikuwa amefaulu vizuri ila kwa wakati huu kila mmoja alikuwa akielekea kusoma tofauti na mwenzake. Peter alichaguliwa kujiunga na shule ya Tambaza huku Gloria akichaguliwa kujiunga na shule ya Zanaki zote zikiwa jijini Dar es Salaam.

Kidogo sana ukaribu wao ukaanza kupungua, mambo yakaanza kubadilika, kila mtu akaanza kuukumbuka ukaribu ambao alikuwa nao kwa mwenzake katika kipindi kile ambacho walikuwa shule moja, tena darasa moja.

Simu ndicho kilikuwa chombo cha mawasiliano ambacho walikuwa wakipenda kukitumia kuwasiliana, ingawa walikuwa mbalimbali lakini simu zikaonekana kuwafanya kuwa karibu sana. Kila siku walikuwa wakiwasiliana usiku, walikuwa wakichukua muda mwingi kuongea simuni, mchana wakiandikiana meseji mbalimbali na wakati mwingine kuonana faragha.

Ingawa walikuwa wakifanya mambo mengi kama wapenzi lakini kamwe hawakusahau kuhusu Elimu, walikuwa wakiendelea kusoma zaidi na zaidi huku upendo wao ukiendelea kukua kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele.

Wakafanikiwa kumaliza kidato cha sita na wote kuchaguliwa chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, wakaanza kusoma huku ukaribu wao ukiwa wazi kabisa na kutambulishana kwa wazazi wao.

Hiyo ilikuwa ni furaha kwao na kwa wazazi wao pia, wakaamua kuanza kufanya vitu kwa wazi kabisa kwani hawakuwa wakihofia kitu chochote kwa wakati huo. Mwaka wa kwanza ukakatika, mwaka wa pili ukaingia na ndipo walipoamua kuwaeleza wazazi juu ya lengo lao la kutaka kufunga ndoa na kuwa pamoja.

Taarifa hiyo ikaonekana kuwa ya furaha kwa wazazi wao, wakatoa baraka zote na kuwaruhusu kwa moyo mmoja vijana wao kuoana na kuishi pamoja. Siku zilikuwa zimekatika sana, maandalizi ya harusi yalikuwa yamefanyika vya kutosha na katika kipindi hiki zilikuwa zimebakia siku thelathini kabla ya kufungwa kwa harusi hiyo kanisani.

Wazazi waliongea sana katika hafla hiyo fupi isiyokuwa na watu wengi huku kila mmoja akijaribu kuionyesha furaha yake ya waziwazi mahali pale walipokuwa. Kila mmoja alipomaliza kuongea, Peter akatakiwa kuongea kitu chochote alichokuwa nacho moyoni hata kabla ya Gloria nae kuitwa na kuongea.

“Sijui niseme nini. Yaani najiona nimezidiwa na furaha kabisa. Kila ninapomuangalia Gloria nakumbuka kipindi kile alipokuwa mdogo na kuanza kuelekea nae shuleni. Unakumbuka Gloria?” Peter alisema na kumuuliza Gloria.

“Nakumbuka. Ila sikuwa mdogo peke yangu. Sema tulikuwa wadogo,” Gloria alimwambia Peter na kuwafanya watu wote mahali pale kuanza kucheka.
“Nafahamu. Ila si unakumbuka kwamba nilikuwa mtu wa kwanza kukuvusha barabara? Nisingekuwa makini na wewe ungekuwa umekwishagongwa na gari.

Nilianza kukulinda toka zamani sana, japokuwa tulikuwa wadogo lakini bado nilikuwa nikikuonyeshea jinsi gani ninakuthamini na kukulinda, sikutaka uvuke barabara peke yako, nilikuwa nikikushika mkono na kukuvusha barabara. Ulinzi ule ule ambao nilikuwa nikikupa toka utotoni ndiyo ulinzi ule ule ambao nitaendelea kukupa hadi uzeeni,” Peter alisema huku akimwangalia Gloria.

Watu wote waliokuwa wamekaa sebuleni pale wakabaki kimya, maneno ambayo alikuwa akiyaongea Peter yalionekana kuwa maneno mazito ambayo kwa msichana yeyote angeyasikia ni lazima angejiona ni kwa namna gani alikuwa akipendwa na kuthamaniwa.

“Naona siku ya harusi ni mbali sana, acha nianze kukuahidi leo hii hii hata kabla ya harusi yenyewe,” Peter alisema huku akimnyanyua Gloria na kuupitisha mkono katika kiuno cha Gloria na kisha kuendelea.

“Nakuahidi kuwa nawe katika maisha yangu yote, nakuahidi kukupenda katika shida na raha, magonjwa na afya, furaha na maumivu. Naahidi kukupenda katika kila hatua ya maisha ambayo tutayapitia baada ya kuingia katika ndoa,” Peter aliwambia Goria ambaye alibaki kimya huku kwa mbali macho yake yakianza kulengwa na machozi.

Peter akabaki kimya kwa muda, alikuwa akimwangalia Gloria usoni, kwake, Gloria akaonekana kuwa mtu mpya, msichana mpya ambaye alikuwa ameongezewa uzuri zaidi ya ule ambao alikuwa nao kabla.

Lipsi za midomo yake zilikuwa zikichezacheza tu huku akizitamani lipsi za Gloria. Alipoona ameridhika kumwangalia Gloria, akayarudisha macho yake kwa wazazi wa Gloria, mzee Michael na Bi Justina.

“Nimeahidi mengi, nimeahidi kumtunza binti yenu katika njia iliyo njema. Ninawaomba ninyi pia mniruhusu kumchukua binti yenu, muda wenu wa kumlea naona unafikia tamati, sasa hivi nadhani ni muda wangu kumlea binti huyu mrembo, binti huyu aliyeuteka moyo wangu,” Peter aliwaambia mzee Michael na Bi Justina.

Ilipofika zamu ya Gloria kuongea, akashindwa kabisa kuongea kitu chochote kile, akaamua kumkumbatia Peter na kuanza kulia. Maneno ambayo aliyaongea Peter yalikuwa yamemgusa, aliyaona maneno mazito ambayo yalikuwa yakijirudia rudia moyoni mwake.
“Nakupenda Peter. Nakupenda mpenzi,” Gloria alimwambia Peter huku wakiwa wamekumbatiana.
“Nakupenda pia Gloria,” Peter alimwambia Gloria.

Baada ya hapo, wote wakatawanyika na kuyafuata magari yao. Peter hakutaka kumuacha Gloria mikononi mwake, alikuwa amemshikilia vilivyo japokuwa mzee Michael alikuwa akimuita.

Wote wakabaki wakiangaliana tu, mapenzi ambayo waliyokuwa nayo mioyoni mwao yalikuwa yakiendelea kuchipuka.
“Ninakupenda sana Gloria,” Peter alimwambia Gloria.
“Ninakupenda pia.”

Baada ya hapo, Gloria akaingia garini na kuondoka mahali hapo. Muda wote huo Peter alikuwa amesimama tu mpaka pale gari lilipotoka machoni mwake. Akaanza kupiga hatua na kuelekea ndani ambapo akapitiliza hadi chumbani.

Alipofika chumbani, akaanza kuchati na Gloria huku akionekana kuwa na furaha tele. Waliendelea kuchati mpaka saa tisa usiku, muda ambao akapitiwa na usingizi kitandani pale. Ingawa meseji zilikuwa zikiendelea kuingia, Peter alikuwa amekwishalala kitambo kutokana na uchovu mkubwa ambao alikuwa nao siku hiyo.

“Nakupenda mpenzi. Najua umeshalala, ila utakapoamka naomba ujue kwamba ninakupenda sana. Mwaaaaaaaa! Hiyo ni kwa ajili yako peke yako” Hiyo ilikuwa ni meseji ya mwisho ambayo Gloria alikuwa amemuandikia Peter ambaye alikuwa amekwishalala.

*Je, nini kiliendelea?*
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
Jogoo wa shamba11
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
*NYEMO CHILONGANI*
*ULINIUA GLORIA*

*Sehemu ya 02*

Ilikuwa ni taarifa nzuri kwa Peter ambaye alikuwa amefungua barua pepe yake na kukutana na majibu ya barua pepe ambayo alikuwa ameituma miezi miwili iliyopita juu ya kujiunga na chuo cha Biashara cha St’ Victor kilichokuwa jijini Lusaka nchini Zambia.

Taarifa ile ilikuwa moja ya taarifa nzuri ambayo ilimpa furaha sana siku hiyo, alichokifanya ni kuichua na kuiweka kwenye laptop yake na kisha kuifunga. Uso wake ukajawa na furaha, akajiona kukamilisha ndoto ambazo alikuwa amejiwekea toka kipindi cha nyuma, ndoto cha kusoma katika moja ya chuo kikubwa Afrika.

Wazazi wake waliporudi nyumbani usiku, akawataarifu juu ya taarifa ile, kila mmoja alionekana kufurahia kupita kawaida, mafanikio ya mtoto wao yalikuwa yakiwapa furaha kupita kawaida. Siku hazikuwa nyingi sana na alikuwa akihitajika chuoni hapo, alikuwa amepewa wiki mbili kwa ajili ya maandalizi tu.

Alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na Gloria na kisha kumwambia kuhusu taarifa ile, Gloria nae akaonyesha furaha na kuahidi kwenda nyumbani kwa mzee Steven kwa ajili ya kuonana na Peter, mpenzi wa maisha yake ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida.

Alipofika ndani ya nyumba hiyo, akapokelewa kwa mabusu mengi na safari yao kuishia chumbani ambako huko wakakaa wakicheza muziki huku wakishikanashikana kama kawaida yao. Kila mmoja kwa wakati huo alionekana kuwa na furaha, mafanikio ya mmoja kati yao yalionekana kuwa mafanikio ya kila mtu.

Siku iliyofuata, Peter akaanza kufanya maandalizi katika maduka mbalimbali huku akiwa pamoja na mpenzi wake, Gloria. Walitumia zaidi ya masaa matatu kutembea katika maduka mbalimbali na ndipo waliporudi nyumbani.
“Na vipi kuhusu harusi yetu?” Gloria aliuliza.

“Tutaoana tu. Hilo halina kipingamizi mpenzi” Peter alimwambia Gloria.
“Najua tutaoana ila je itakuwa muda muafaka uliopangwa?” Gloria aliuliza.

“Yeah! Nitakachokifanya mara baada ya kuelekea chuo, nitakupigia simu na kunifuata kule na kisha tutaoana kulekule” Peter alimwambia Gloria.
“Yaani tuoane hata wazazi wasishiriki ndoa yetu?”

“Kwani tatizo liko wapi? Ila usijali, wao pia watatufuata. Si unajua Zambia si mbali sana” Peter alimwambia Gloria.
“Sawa. Ila inabidi tuoane haraka sana, nina hamu ya kuingia katika ndoa”
“Usijali mpenzi”

Furaha bado kwao iliendelea kama kawaida, walishinda siku nzima chumbani huku wakifanya kila kitu walichokuwa wakitaka kukifanya siku hiyo. Kuanzia hapo, wakazidi kuwa karibu zaidi, ukaribu wao ukaongezeka kiasi ambacho kiliwashangaza hata wazazi wao pia.
Siku ziliendelea kukatika mpaka kufika siku ambayo Peter alitakiwa kuondoka kuelekea nchini Zambia.

Walipofika uwanja wa ndege, Peter akamshika mkono Gloria na kuanza kumuaga. Muda wote huo Gloria alikuwa akilia tu, hakuamini kama mtu ambaye alikuwa akimpenda na kumzoea alikuwa akijiandaa na safari ya kuelekea masomoni nchini Zambia.

“Mbona unalia sasa?” Peter aliuliza.
“Inaniuma mpenzi”
“Usijali. Nitakapofika tu, nitafanya mpango wa wewe kuja huko”
“Najua ila naona kama utachelewa sana”

“Sitochelewa wala kuwahi, nitahakikisha nakuja muda muafaka” Peter alimwambia Gloria.
“Sawa mpenzi” Gloria alijibu na kisha kukumbatiana.

Baada ya hapo, Peter akaanza kuwaaga tena marafiki zake na wazazi wake na kisha kuondoka na ndege ya siku hiyo huku moyo wake ukiwa umegawanyika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ilikuwa ikimtaka kutokuondoka kwa sababu ya Gloria lakini sehemu nyingine ilikuwa ikimtaka kuondoka ili kukamilisha ndoto alizokuwa amejiwekea toka zamani.

Harusi ambayo waliipanga ifanyike baada ya mwezi mmoja ikaonekana kuingia doa, kwa wakati huo Peter alikuwa akiangalia kuhusu masomo yake tu, alijua fika kwamba harusi ingeendelea kuwepo hata kama kingetokea kitu gani, ila kwa wakati huo alijiona kuwa na kila sababu za kuenda nchini Zambia na kujiunga na chuo cha St’ Victor kilichokuwa katikati ya jiji la Lusaka.

Saa 10:17 ndege ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege jijini Lusaka ambako Peter akateremka na kuanza kuelekea ndani ya jengo la uwanja huo. Alipochukua begi lake hasa mara baada ya kuchunguzwa, akachukua teksi ambayo alimtaka dereva kumpeleka katika chuo Kikuu cha St’ Victor.

Saa 10:45 gari ikaanza kuingia katika eneo la uwanja wa chuo kile ambako moja kwa moja akaanza kuelekea katika ofisi za chuo kile na kisha kujitambulisha kwa uongozi wa chuo kile. Akakaribishwa, akafanya ulipaji wa vyumba ambavyo vilikuwa katika chuo kile na maisha yake ya Elimu kuanzia ndani ya chuo hicho.

Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Gloria pamoja na wazazi wake, kila siku walikuwa wakimkumbushia kuhusu harusi ambayo walipanga ifanyike baada ya wiki kadhaa, Peter alionekana kuwa muelewa japokuwa hakutaka kuwaambia wazazi wake kwamba walikubaliana kufungia harusi nchini Zambia katika siku ambayo Gloria angekwenda kule kwa ajili ya kumtembelea.

“Usiwaambie kama nitakuita huku kwa ajili ya kufunga ndoa” Peter alimwambia Gloria.
“Sawa. Ila usichelewe mpenzi, ninatamani kufunga ndoa nawe” Gloria alimwambia Peter.

“Usijali. Ngoja maisha yangu yatulie kidogo, nafikiri siku chache zijazo nitakuita kwanza uje tukae kwa muda na kisha tufunge ndoa takatifu kanisani” Peter alimwambia Gloria.

“Sawa”
Maisha yalikuwa yakiendelea nchini Zambia, kila siku Peter alikuwa akiingia darasani, wanachuo wengi walikuwa wakitamani kuwa karibu na Peter chuoni hapo kwa sababu tu alikuwa Mtanzania, watu ambao walikuwa wakisifiwa kwa kuongea sana nchini Zambia.

Peter alikuwa muongeaji mkubwa sana chuoni kitu ambacho kilimfanya kupata marafiki wengi sana akiwepo Kaposhoo, mtoto wa tajiri Charles nchini Zambia. Mara kwa mara Kaposhoo alikuwa karibu na Peter jambo ambalo liliwafanya kuwa marafiki wakubwa chuoni hapo.

Kutokana na kuwa na fedha nyingi, Kaposhoo ndiye ambaye alimfundisha Peter kwenda katika kumbi za starehe na kunywa pombe, maisha ambayo Peter hakuwa ameyazoea kabla.

Kazi kubwa ya Kaposhoo ilikuwa ni kutembea na kila msichana ambaye alikuwa akionekana mrembo mbele yake, maisha hayo akawa ameyazoea sana, fedha ambazo alikuwa nazo ziliwafanya wasichana wengi kumpapatikia.

Tangu katika kipindi ambacho Peter alikuwa amezoeana na Kaposhoo, hakukuwa hata na siku moja ambayo Peter alitumia fedha zake, Kaposhoo ndiye ambaye alikuwa akimgawia Peter kiasi kikubwa cha fedha ambacho Peter alikuwa akiendelea kufanyia mambo yake.

Hosteli za chuo zikaonekana kuwabana sana jambo ambalo liliwafanya kupanga nyumba nzima katika mtaa wa Kingstone, mtaa ambao ulikuwa ukikaliwa na matajiri tu nchini Zambia.

Maisha yalionekana kuwa ya furaha, walikuwa wakijiachia kupita kawaida, japokuwa Kaposhoo alikuwa akipenda kulala na wasichana mbalimbali lakini hali ilionekana kuwa tofauti kwa Peter.
Peter hakutaka kuwa na msichana mwingine yeyote, uaminifu wake kwa msichana Gloria bado ulikuwa ukiendelea katika moyo wake.

Kaposhoo hakutaka kumuona rafiki yake akiwa katika lindi la mawazo, kila siku alikuwa akijitahidi sana kumletea wasichana wa aina mbalimbali lakini bado Peter alikuwa akionyesha msimamo wa kulilinda penzi lake na Gloria.

Japokuwa alikuwa amepanga kufunga ndoa na Glory ndani ya mwezi huo lakini mambo yakaonekana kubadilika mara baada ya kuwasiliana na wazazi wake na kuwaambia kwamba alikuwa ameahirisha mpaka katika miezi ijayo.

Hiyo haikuonekana kuwa taarifa nzuri kutokana na mambo mengi kuwa tayari lakini kwa sababu mtoto wao huyo alikuwa masomoni nchini Zambia, wakakubaliana nae.

Mwezi wa kwanza ukakatika, mwezi wa pili ukaingia na ndipo ambapo Peter akaamua kumuita Gloria nchini Zambia. Kwa mara ya kwanza kufika nchini Zambia, Gloria alionekana kuwa mwenye furaha kubwa, mara kwa mara alikuwa karibu na mpenzi wake, Peter.

Ulipita muda mrefu sana bila wawili hao kuonana, walipofika nyumbani, kituo cha kwanza kilikuwa ni chumbani ambako wakaanza kufanya mambo ya kiutu uzima. Tendo lile liliwachukua dakika zaidi ya themanini, kila mmoja akaridhika.
“Umepanga nyumba hii peke yako?” Gloria aliuliza.

“Hapana. Ninakaa na rafiki yangu hapa. Mtoto mmoja wa tajiri hapa Zambia. Yeye ndiye aliyegharamia kila kitu” Peter alimwambia Gloria.
“Sawa” Gloria aliitikia.

Saa 12:18 gari la Kaposhoo likaanza kupaki mahali hapo na moja kwa moja kuteremka. Kiu yake kubwa kwa wakati huo ilikuwa ikitaka kumuona Gloria, msichana ambaye alimfanya Peter kutotaka kumsaliti katika kipindi ambacho alikuwa peke yake nchini Zambia.

Mara baada ya kuingia ndani, akaanza kumuita Peter ambaye akafika sebuleni pale huku akiwa pamoja na Gloria. Macho ya Kaposhoo yalipotua kwa Gloria, kwanza akashtuka, uzuri wa Gloria ukaonekana kumshtua kupita kawaida.

Huku akionekana dhahiri kuchanganyikiwa na uzuri ule, akaanza kumfuata na kumpa mkono kwa lengo la kumsalimia. Aliposhikana mikono na Gloria, akauhisi mwili wake ukipigwa na shoti kali, kwa mbali kijasho kilikuwa kikimtoka.
“Karibu G” Kaposhoo alimkaribisha Gloria.

“Asante” Gloria aliitikia.
Muda wote Kaposhoo alikuwa akimwangalia Gloria, tayari uzuri wake ukaonekana kumchanganya kupita kawaida. Ni kweli alikuwa amekutana na warembo wengi lakini kwa Gloria alionekana kuwa na urembo wa tofauti sana, urembo ule ulikuwa ukimtetemesha moyo wake kila alipokuwa akimwangalia.
“Inabidi nifanye kitu. Ni mrembo sana.

Inabidi nifanye mapenzi pamoja nae kwa gharama yoyote ile, nilikuwa natamani kukutana na wasichana wa Kitanzania, kwa huyu, simuachi, hata kama urafiki na Peter utakufa, poa tu” Kaposhoo alikuwa akijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akimwangalia Gloria ambaye alikuwa amelala mapajani mwa Peter kochini.

*Je, nini kitaendelea?*
 
macho 4

macho 4

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2017
Messages
432
Likes
271
Points
80
macho 4

macho 4

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2017
432 271 80
Mtunzi

*NYEMO CHILONGANI*
*ULINIUA GLORIA*

*Sehemu ya 01*

Kelele za shangwe zilikuwa zikisikika kutoka katika nyumba ya mzee Steven. Vigelegele kutoka kwa wakinamama vilikuwa miongoni mwa sauti za shangwe zilizoendelea kusikika kutoka ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imejengwa kisasa katika Mtaa wa Magomeni Kondoa.

Magari kadhaa yalikuwa yamekusanyika ndani ya eneo la nyumba hiyo, idadi kubwa ya magari hayo yalikuwa ya kifahari ambayo wala hakukuwa na mtu ambaye alishangaa kuyaona yakiwa yamepakiwa ndani ya eneo la nyumba hiyo.

Sauti ya muziki ilikuwa juu ingawa wakati mwingine ilikuwa ikipunguzwa kutokana na mtu yeyote ambaye alikuwa akitaka kuongea lake katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza Peter na Gloria ambao walikuwa wakitarajia kufunga ndoa mwezi mmoja baadae ndani ya Kanisa la Praise and Worship lililokuwa Mwenge.

Wote ndani ya nyumba hiyo walionekana katika nyuso zilizokuwa na furaha, walipenda kuwaona watoto wao wakiingia katika maisha ya ndoa, maisha yaliyoonekana kutamaniwa na watu ambao walikuwa nje nayo lakini kuchukiwa na watu ambao tayari walikuwa ndani ya maisha hayo.

Gloria hakuwa mbali na Peter, muda wote alikuwa pembeni yake huku akipigapiga picha kwa kutumia simu yake katika kila tukio lililokuwa likiendelea mahali hapo. Kazi kubwa ya Peter ilikuwa ni kukishika kiuno cha Gloria, kumbusu mara kwa mara huku akimuachia tabasamu pana.

Baba yake Peter, mzee Steven alionekana kuwa mwenye furaha kubwa, muda wote alipokuwa akiongea, alikuwa akitabasamu tu huku akionekana kuzidiwa na furaha ambayo alikuwa nayo kwa kile kitu ambacho kilikuwa kinaendelea.

Katika maisha yake alibahatika kupata watoto wawili tu, wa kwanza alikuwa Rachel ambaye alikuwa amekwishaolewa na wa pili alikuwa Peter ambaye baada ya siku kadhaa nae angeanza maisha ya ndoa na msichana Gloria Michael.

Katika sherehe hiyo, wazazi wake Gloria, mzee Michael Mshama na Bi Justina walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wamekusanyika katika hafla hiyo fupi ya kuwapongeza kwa hatua ile waliyokuwa wameifikia.

Mpaka kufikia katika kipindi hicho, wao pia walionekana kuwa na furaha kubwa, hawakuamini kama binti yao, Gloria alikuwa akitarajiwa kufunga ndoa na baada ya hapo kuitwa mke wa mtu huku ukichukua muda mchache kabla ya kuitwa mama.

Gloria ndiye alikuwa binti yao ambaye walikuwa wakimpenda kupita kawaida, walimthamini na kumpa kila kitu ambacho kama wazazi walitakiwa kumpa binti yao mpendwa. Kwao, Gloria ndiye alikuwa kila kitu, yeye ndiye alikuwa tabasamu nyusoni mwao.

Ukaribu wa Peter na Gloria ulianza tangu walipokuwa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Mwalimu Nyerere huku baada ya kufika kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Benjamini wakaanza kuingia katika uhusiano wa kimapenzi. Ingawa walikuwa na furaha lakini uhusiano wao ulionekana kuwa na vizuizi vingi huku kizuizi kimoja na kikubwa kikiwa ni masomo.

Walitamani kufanya mambo mengi katika maisha yao kwa wakati huo lakini masomo ndio kilikuwa kizuizi kikubwa. Muda mwingi walikuwa wakitamani kusoma pamoja lakini kila walipojaribu kufanya hivyo, walijikuta wakianza kushikanashikana na hatimae kulaliana na kufanya mapenzi.

Kila mmoja kichwani alikuwa na ndoto yake ambayo alikuwa amejiwekea. Peter alikuwa na hamu kubwa ya kuwa Mchumi mkubwa hapo baadae huku Gloria akiwa na hamu ya kuwa Mwanasheria mkubwa hapo baadae. Kila mmoja alikuwa akiishi katika ndoto yake ambayo ilikuwa ikiendelea kukua kadri siku zilivyozidi kwenda mbele.

Wakamaliza kidato cha nne na kukaa nyumbani kusubiri matokeo, yalipotoka, kila mmoja alikuwa amefaulu vizuri ila kwa wakati huu kila mmoja alikuwa akielekea kusoma tofauti na mwenzake. Peter alichaguliwa kujiunga na shule ya Tambaza huku Gloria akichaguliwa kujiunga na shule ya Zanaki zote zikiwa jijini Dar es Salaam.

Kidogo sana ukaribu wao ukaanza kupungua, mambo yakaanza kubadilika, kila mtu akaanza kuukumbuka ukaribu ambao alikuwa nao kwa mwenzake katika kipindi kile ambacho walikuwa shule moja, tena darasa moja.

Simu ndicho kilikuwa chombo cha mawasiliano ambacho walikuwa wakipenda kukitumia kuwasiliana, ingawa walikuwa mbalimbali lakini simu zikaonekana kuwafanya kuwa karibu sana. Kila siku walikuwa wakiwasiliana usiku, walikuwa wakichukua muda mwingi kuongea simuni, mchana wakiandikiana meseji mbalimbali na wakati mwingine kuonana faragha.

Ingawa walikuwa wakifanya mambo mengi kama wapenzi lakini kamwe hawakusahau kuhusu Elimu, walikuwa wakiendelea kusoma zaidi na zaidi huku upendo wao ukiendelea kukua kadri siku zilivyokuwa zikizidi kusonga mbele.

Wakafanikiwa kumaliza kidato cha sita na wote kuchaguliwa chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Walionekana kuwa na furaha kupita kawaida, wakaanza kusoma huku ukaribu wao ukiwa wazi kabisa na kutambulishana kwa wazazi wao.

Hiyo ilikuwa ni furaha kwao na kwa wazazi wao pia, wakaamua kuanza kufanya vitu kwa wazi kabisa kwani hawakuwa wakihofia kitu chochote kwa wakati huo. Mwaka wa kwanza ukakatika, mwaka wa pili ukaingia na ndipo walipoamua kuwaeleza wazazi juu ya lengo lao la kutaka kufunga ndoa na kuwa pamoja.

Taarifa hiyo ikaonekana kuwa ya furaha kwa wazazi wao, wakatoa baraka zote na kuwaruhusu kwa moyo mmoja vijana wao kuoana na kuishi pamoja. Siku zilikuwa zimekatika sana, maandalizi ya harusi yalikuwa yamefanyika vya kutosha na katika kipindi hiki zilikuwa zimebakia siku thelathini kabla ya kufungwa kwa harusi hiyo kanisani.

Wazazi waliongea sana katika hafla hiyo fupi isiyokuwa na watu wengi huku kila mmoja akijaribu kuionyesha furaha yake ya waziwazi mahali pale walipokuwa. Kila mmoja alipomaliza kuongea, Peter akatakiwa kuongea kitu chochote alichokuwa nacho moyoni hata kabla ya Gloria nae kuitwa na kuongea.

“Sijui niseme nini. Yaani najiona nimezidiwa na furaha kabisa. Kila ninapomuangalia Gloria nakumbuka kipindi kile alipokuwa mdogo na kuanza kuelekea nae shuleni. Unakumbuka Gloria?” Peter alisema na kumuuliza Gloria.

“Nakumbuka. Ila sikuwa mdogo peke yangu. Sema tulikuwa wadogo,” Gloria alimwambia Peter na kuwafanya watu wote mahali pale kuanza kucheka.
“Nafahamu. Ila si unakumbuka kwamba nilikuwa mtu wa kwanza kukuvusha barabara? Nisingekuwa makini na wewe ungekuwa umekwishagongwa na gari.

Nilianza kukulinda toka zamani sana, japokuwa tulikuwa wadogo lakini bado nilikuwa nikikuonyeshea jinsi gani ninakuthamini na kukulinda, sikutaka uvuke barabara peke yako, nilikuwa nikikushika mkono na kukuvusha barabara. Ulinzi ule ule ambao nilikuwa nikikupa toka utotoni ndiyo ulinzi ule ule ambao nitaendelea kukupa hadi uzeeni,” Peter alisema huku akimwangalia Gloria.

Watu wote waliokuwa wamekaa sebuleni pale wakabaki kimya, maneno ambayo alikuwa akiyaongea Peter yalionekana kuwa maneno mazito ambayo kwa msichana yeyote angeyasikia ni lazima angejiona ni kwa namna gani alikuwa akipendwa na kuthamaniwa.

“Naona siku ya harusi ni mbali sana, acha nianze kukuahidi leo hii hii hata kabla ya harusi yenyewe,” Peter alisema huku akimnyanyua Gloria na kuupitisha mkono katika kiuno cha Gloria na kisha kuendelea.

“Nakuahidi kuwa nawe katika maisha yangu yote, nakuahidi kukupenda katika shida na raha, magonjwa na afya, furaha na maumivu. Naahidi kukupenda katika kila hatua ya maisha ambayo tutayapitia baada ya kuingia katika ndoa,” Peter aliwambia Goria ambaye alibaki kimya huku kwa mbali macho yake yakianza kulengwa na machozi.

Peter akabaki kimya kwa muda, alikuwa akimwangalia Gloria usoni, kwake, Gloria akaonekana kuwa mtu mpya, msichana mpya ambaye alikuwa ameongezewa uzuri zaidi ya ule ambao alikuwa nao kabla.

Lipsi za midomo yake zilikuwa zikichezacheza tu huku akizitamani lipsi za Gloria. Alipoona ameridhika kumwangalia Gloria, akayarudisha macho yake kwa wazazi wa Gloria, mzee Michael na Bi Justina.

“Nimeahidi mengi, nimeahidi kumtunza binti yenu katika njia iliyo njema. Ninawaomba ninyi pia mniruhusu kumchukua binti yenu, muda wenu wa kumlea naona unafikia tamati, sasa hivi nadhani ni muda wangu kumlea binti huyu mrembo, binti huyu aliyeuteka moyo wangu,” Peter aliwaambia mzee Michael na Bi Justina.

Ilipofika zamu ya Gloria kuongea, akashindwa kabisa kuongea kitu chochote kile, akaamua kumkumbatia Peter na kuanza kulia. Maneno ambayo aliyaongea Peter yalikuwa yamemgusa, aliyaona maneno mazito ambayo yalikuwa yakijirudia rudia moyoni mwake.
“Nakupenda Peter. Nakupenda mpenzi,” Gloria alimwambia Peter huku wakiwa wamekumbatiana.
“Nakupenda pia Gloria,” Peter alimwambia Gloria.

Baada ya hapo, wote wakatawanyika na kuyafuata magari yao. Peter hakutaka kumuacha Gloria mikononi mwake, alikuwa amemshikilia vilivyo japokuwa mzee Michael alikuwa akimuita.

Wote wakabaki wakiangaliana tu, mapenzi ambayo waliyokuwa nayo mioyoni mwao yalikuwa yakiendelea kuchipuka.
“Ninakupenda sana Gloria,” Peter alimwambia Gloria.
“Ninakupenda pia.”

Baada ya hapo, Gloria akaingia garini na kuondoka mahali hapo. Muda wote huo Peter alikuwa amesimama tu mpaka pale gari lilipotoka machoni mwake. Akaanza kupiga hatua na kuelekea ndani ambapo akapitiliza hadi chumbani.

Alipofika chumbani, akaanza kuchati na Gloria huku akionekana kuwa na furaha tele. Waliendelea kuchati mpaka saa tisa usiku, muda ambao akapitiwa na usingizi kitandani pale. Ingawa meseji zilikuwa zikiendelea kuingia, Peter alikuwa amekwishalala kitambo kutokana na uchovu mkubwa ambao alikuwa nao siku hiyo.

“Nakupenda mpenzi. Najua umeshalala, ila utakapoamka naomba ujue kwamba ninakupenda sana. Mwaaaaaaaa! Hiyo ni kwa ajili yako peke yako” Hiyo ilikuwa ni meseji ya mwisho ambayo Gloria alikuwa amemuandikia Peter ambaye alikuwa amekwishalala.

*Je, nini kiliendelea?*
Na mm nipo nakwenda nao mdogo mdogo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
104,185
Likes
294,432
Points
280
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
104,185 294,432 280
*Sehemu ya 03*

Gloria alionekana kuwa tofauti kwa Kaposhoo, muda wote alikuwa akimwangalia kwa macho ya matamanio, macho ambayo yalionyesha dhahiri kwamba alikuwa akitaka kulala nae tu.
Uzuri wa Gloria ulikuwa ukiutetemesha moyo wa Kaposhoo, kila alipokuwa akimwangalia aliuhisi mwili wake ukiwa kwenye dimbwi zito la mapenzi, dimbwi ambalo alishindwa kabisa kuogelea na alijiona kama alikuwa akikaribia kuzama.

Kitu alichokuwa akikitaka ni kulala na Gloria tu, hakuangalia kuhusu urafiki mkubwa ambao alikuwa nao kwa Peter, kitu ambacho alikuwa akikiangalia kwa wakati huo ni kukidhi tamaa za mwili wake tu. Kila siku alipokuwa akimwangalia Gloria alizidi kuwa mrembo kiasi ambacho Kaposhoo akaona ilikuwa heri kugombana na Peter lakini si kumuacha Gloria ambaye kila siku alizidi kuonekana mrembo.

Alichokijua yeye ni kwamba alikutanana Peter chuoni, hakuwa amekua nae toka utotoni jambo ambalo lilimfanya kutokuhisi uzito wowote kama angeamua kutembea na Gloria, asingejisikia hukumu yoyote moyoni mwake.

Hapo ndipo ambapo Kaposhoo akaamini kwamba wanawake wengi wa Kitanzania walikuwa warembo waliokuwa na figa nzuri ambazo kwa mwanaume yeyote anayejua kutamani basi ni lazima angeingiwa na pepo la uzinzi mara amuaonapo mwanamke kutoka nchini Tanzania.

“Anazidi kunawili tu” Kaposho alijisemea moyoni katika kipindi ambacho alikuwa akimwangalia Gloria ambaye alikuwa akimvutia kupita kawaida.

Kaposhoo hakujua ni mahali gani ambapo alitakiwa kuanzia ili kumteka Gloria, kila siku ndoto zake zilikuwa juu ya Gloria tu. Hakutaka kujihusisha tena na wanawake wa hapo Zambia kwa kuona kwamba hawakuwa wanawake wazuri kama alivyokuwa Gloria.

Kuhusu kuchukua wanawake wa Kizambia, Kaposhoo akaiacha tabia hiyo, hakutaka kuonekana machoni mwa Gloria kwamba alikuwa mtu wa wanawake, alitaka aonekane mtu mwema jambo ambalo alifanikiwa kwa asilimia kubwa.

Hata katika kipindi ambacho alikuwa akitafuta mazoea kwa Gloria, Peter hakuonekna kuhofia kitu chochote kile kwani kwake watu hao wawili walionekana kuwa waaminifu sana, kwa Gloria, Peter hakudhania kama msichana huyo angeweza kumsaliti na kumfuata mwanaume mwingine zaidi yake huku kwa Kaposhoo, alimuona kuwa rafiki yake mkubwa ambaye wala asingeweza kutembea na msichana ambaye alijua fika kwamba alikuwa msichana wake.

Kujiamini huko kukaonekana kuwa kosa kubwa sana kwani kitendo cha Peter kuwaacha mara kwa mara peke yao sebuleni, Kaposhoo akaanza kupiga ndogondogo ambazo zilikuwa zikimfanya Gloria kuchekacheka tu.

Kaposhoo hakuonekana kujali, alijua fika kwamba kwa mwanaume yeyote ambaye unamtaka msichana fulani, haukutakiwa kuwa na haraka, ulitakiwa kufanya mambo yako taratibu sana na mwisho wa siku msichana huyo anakuwa wako.

Fedha kwake zikaonekana kuwa silaha kubwa kwa kila msichana ambaye alikuwa akimtaka. Kwa sababu alikuwa akimtaka sana Gloria, fimbo yake kubwa ilikuwa ni fedha ambazo kwa kiasi fulani zilionekana kumchanganya Gloria.

Kaposhoo hakuona hasara kutumia zaidi ya kwacha laki moja kwa siku, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kumchanganya Gloria na mwisho wa siku anakuja kuwa wake na kuanza kutanua nae kama kawaida yake.

“Unanawili sana siku hizi. Nini siri ya mafanikio yako?” Kaposhoo alimuuliza Gloria huku akitoa tabaamu pana.
“Kula vizuri tu” Gloria alijibu huku akionekana kusikia aibu.

Kaposhoo hakutaka kukaa kochini hapo tu, alichokifanya ni kuinuka na kisha kumsogelea Gloria ambaye alikuwa katika kochi jingine na kumuinamia kwa nyuma.

Pumzi yake ikaanza kumpiga Gloria shingoni mwake, kutokana na kiyoyozi kilichokuwa ndani ya nyumba kile kilivyokuwa kikitoa kijiubaridi, Gloria akaanza kujisikia hali ya utofauti.
“Leo tunakula nini?” Kaposhoo alimuuliza Gloria.
“Sijui. Wewe unataka tule nini?” Gloria alimuuliza.

“Chochote tu utakachopenda” Kaposhoo alimwambia Gloria.
“Ngoja niandae chakula kizuri” Gloria alimwambia Kaposhoo na kisha kuinuka kochini hapo.

Akaanza kupiga hatua kuelekea jikoni. Kaposhoo akatulia kochini pale, tayari alijiona kwenda kushinda kile alichokuwa akikitaka. Hakuonekana kuogopa, ndani ya nyumba walikuwa wawili tu huku Peter akiwa chuoni.

Alichokifanya Kaposhoo ni kusimama na kisha kuelekea kule kule jikoni ambapo akamkuta Gloria akikata kata nyanya huku akiwa amesimama na kuupa mgongo mlango.

Kaposhoo alivyoona hivyo, akaanza kupiga hatua ndogondogo, alipomfikia Gloria, akaipeleka mikono yake kiunoni mwa Gloria.

Mategemeo yake yote alifikiri kwamba angepata upinzani kutoka kwa Gloria, kilichomshangaza, hakukuwa na upinzani wowote ule. Hiyo ikaonekana kuwa nafasi kwake, akaanza kuusogeza mdomo wake mpaka katika shingo ya Gloria na kisha kumbusu.

Katika kila hatua ambayo alikuwa akiipiga mwilini mwa Gloria, msichana huyo alikuwa akitulia, hakuonyesha kipingamizi chochote kile. Mpaka kufikia hatua hiyo, tayari Kaposhoo akajiona kuwa mshindi ambaye alitakiwa kufanya kitu chochote kile.

Mikono yake haikutulia, alichokifanya ni kuanza kuipeleka kwa juu mpaka kufikia sehemu iliyokuwa na matiti ya Gloria na kisha kuanza kuyashikashika.

Hali ile ikamfanya Gloria kuanza kuunyonganyonga mwili wake huku akikiachia kisu alichokishika na kisha kuishika mikono ya Kaposhoo ambaye tayari alionekana kuchanganyikiwa na kuingiwa na mzuka wa kufanya ngono tu.

“Niacheeeee.....” Gloria alimwambia kaposhoo kwa sauti ya mahaba huku akijaribu kuitoa mikono ya Kaposhoo ambayo ilikuwa ikiendelea kuchezea matiti yake.

“Tatizo nini? Wewe si uendelee kukata nyanya tu” Kaposhoo alimwambia Gloria.
“Niacheeee” Gloria alimwambia Kaposhoo katika sauti ambayo ilimwambia kuendelea kufanya vile.

Kaposhoo hakuonekana kukubaliana nae, alichokifanya ni kuendelea kuyachezea matiti ya Gloria ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi.

Gloria akaonekana kuchoka, hatua ambayo alifikia Kaposhoo ikaonekana kumchosha hali iliyompelekea kumwachia mwanaume huyo afanye chochote kile alichokuwa akitaka kukifanya mwilini mwake.

Hiyo ikaonekana kuwa nafasi zaidi kwa Kaposhoo, alichokifanya ni kuanza kuifungua blauzi aliyokuwa ameivaa Gloria na kisha kuyaacha matiti yake ya saa sita kuwa wazi.

Kaposhoo akaona kutokufaidi, akamgeuza Gloria na kisha kuanza kuangaliana nae. Tayari Gloria akaonekana kuchanganyikiwa, macho yake yalikuwa yamelegea kupita kawaida, macho ambayo yalionyesha kwamba alikuwa tayari kwa kila kitu mahali hapo.

Huku wakiwa wanaangaliana tu, ghafla mlio wa gari ukaanza kusikika kutoka nje, gari ambalo alikuwa akilitumia Peter. Kwa haraka sana Kaposhoo akachomoka jikoni pale na kisha kuelekea chumbani huku Gloria akianza kufunga vifungo vya blauzi yake na kuendelea kukata nyanya.

Wala hazikupita sekunde nyingi, Peter akatokea mahali hapo, alipokwenda jikoni na macho yake kumuona Gloria, tabasamu pana likatawala usoni mwake, akaanza kumsogelea na kisha kumbusu.

“Nilikumiss sana mpenzi” Peter alimwambia Gloria huku akiachia tabasamu pana.
“Hata mimi. Nilikumiss pia” Gloria alimwambia Peter na kisha kubusiana.

Hayo ndio maisha ambayo yalikuwa yakiendelea ndani ya nyumba hiyo, Peter alikuwa akinyeshewa unafiki wa mapenzi ya dhati kutokwa kwa Gloria lakini ukweli ni kwamba katika kipindi hicho msichana huyo akaonekana kubadilika, mapenzi ambayo alikuwa nayo juu ya Peter yakaonekana kuhamia kwa mwanaume ambaye alikutana nae kwa mara ya kwanza hapo Zambia, Kaposhoo.

Gloria hakuonekana kufikiria kwamba alikuwa na mpenzi wake, Peter ambaye alikuwa tayari kufunga nae ndoa, kitu ambacho alikuwa akikifikiria ni kuwa na Kaposhoo tu ambaye alionekana kuwa na fedha kupita kawaida.

Ingawa Peter alikuwa akielekea chuoni kila siku lakini hali ilikuwa tofauti kwa kaposhoo, ratiba yake ya kwenda chuoni ikaonekana kupungua kabisa, alikuwa akitumia muda mwingi kukaa nyumbani jambo ambalo lilimchanganya Peter.

“Siku hizi huendi kabisa chuo” Peter alimwambia Kaposhoo.
“Nadhani kuna mchezo wa kishirikina nachezewa siku hizi” Kaposhoo alimwambia peter.
“Kwa nini?”

“Ninaumwa sana. Naweza kusema kwamba kesho nakwenda chuo, nitasoma sana ila hiyo kesho ikifika tu, naumwa mpaka siwezi kuamka” Kaposhoo alimwambia Peter.
“Pole sana”
“Asante sana” Kaposhoo alimshukuru Peter.

Hiyo ndio ilikuwa kazi yake, hakutaka kwenda chuoni, tayari Gloria akaonekana kumchanganya kupita kawaida. Kila siku akawa mtu wa kuuchezea mwili wa Gloria lakini kufanya ngono kikawa ni kitu ambacho Gloria alikuwa akikipinga sana.

Kaposhoo hakutaka kuonekana kuwa na haraka, kila siku aliamini kwamba Gloria asingeweza kuchomoka katika mikono yake, kama alikuwa akikaza sana, aliamini kwamba kuna siku angechoka kukaza na hatimae kufanya kile alichokuwa akikitaka, kuivua sketi ya Gloria na kufanya nae mapenzi.

Kushikwashikwa na Kaposhoo kila siku kukaonekana kuzidi kumpagawisha Gloria, kila alipokuwa akimuona Kaposhoo, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda sana.

Japokuwa alijua fka kwamba alikuwa na mpenzi wake, Peter lakini hakuacha kumfikiria Kaposhoo, mwili wake ukaonekana kuanza kuwashwa na hakuona mwanaume yeyote ambaye angeweza kuukuna zaidi ya Kaposhoo ambaye tayari alikuwa ameingia ndani ya moyo wake na kuvuta kiti.

Hali hiyo ndio ambayo ilimfanya Gloria kumvulia sketi Kaposhoo na kwa mara ya kwanza kumsaliti Peter kwa mwanaume huyo ambaye kwake alimuona kuwa mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati. Siku hiyo wakalala chumbani mchana wakifanya mapenzi tu.

Gloria hakuonekana kujutia kile kilichokuwa kikiendelea kutokea, kwake, Kaposhoo alionekana kuwa mwanaume sahihi ambaye alistahili kumvulia sketi yake na hatimae kumsaliti Kaposhoo.

Kwa Gloria wala hakujisikia hukumu hata mara moja, kitu ambacho alikuwa akikifanya alikiona kuwa sahihi kufanywa na mtu kama yeye, mtu ambaye alikuwa ameangukia katika mikono ya mwanaume mwingine, mwanaume ambaye alionekana kumjali zaidi ya kitu chochote kile, MOYO WAKE UKAMSAHAU PETER.

*Je, nini kitaendelea?*
 
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
4,131
Likes
9,326
Points
280
Age
27
moneytalk

moneytalk

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
4,131 9,326 280

Aiii gloria jaman

Sent using Jamii Forums mobile app
 
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Messages
4,104
Likes
1,533
Points
280
K

kisukari

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2010
4,104 1,533 280
Nakuaminia shunie asante
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
22,190
Likes
20,631
Points
280
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
22,190 20,631 280
Gloria analiwa mapema hivyo...

Kapashoo nae siyo kabisa atakulaje mwanamke wa rafiki yake...

Peter ana makosa makubwa sana, kumuamini Peter mbele ya mwanamke wake...

Cc: mahondaw
 
Forum statistics

Threads 1,249,945
Members 481,161
Posts 29,715,396