Ulinisaliti Juliet

Qumanina zao mkule kiboga huyo jamaa na Juliet umle pia
 


Kweli mke wa mtu sumu... jamaa anataka kulipiza...


Cc: mahondaw
 
Dawa ya moto ni moto
 
Mimi sintosahau demu niliyempenda alipewa mimba na mtu mwngne mpk Leo sipendi wanawake
 
SEHEMU YA 23

“Nimekumisi pia, nakuja.”
Siku hiyo sikutaka kurudi nyumbani mapema, nilichokifanya ni kuunganisha mpaka baa ambapo nikaagiza kleti moja ya pombe na kuwaita warembo waje kunywa tani yao huku mziki mkubwa ukisikika.

“Kunyweni mpaka muache, mkichoka, niambieni niwaongezee,” niliwaambia wanawake wale.

“Asante sana, wewe ndiye mtu saa achana na wale wazee wenye mikono ya birika,” aliniambia msichana mmoja na kuanza kunywa, walikuwa kama watano hivi.

Unywaji wao ulikuwa ni wa harakaharaka, kila walipomaliza kreti moja, niliagiza nyingine, nilitaka wanywe tu mpaka wachanganyikiwe.

“Hahah! Kwa hiyo baby tukuite nani sasa manake hii ofa ni funga mwaka,” aliniuliza msichana mmoja kwa sauti ya kilevi, alikuwa amelewa mno.

“Niite Pedeshee Steve au Papaa Steve,” nilimwambia msichana yule.

“Hivi unafanya kazi wapi?” aliuliza msichana mwingine, naye alikuwa amelewa tu.

“Mimi ni Mkurugenzi hapo TRA. Hebu kunyweni kwanza, maswali mengine baadaye,” niliwaambia na kuagiza kreti nyingine.

Usiku huo ilikuwa ni kunywa tu. Sikuwa mlevi wa pombe, nilichokuwa nikinywa ilikuwa ni soda tu. Wanawake wale nisiowajua walikuwa wakipiga kelele kila wakati kiasi kwamba ikaonekana kama fujo pale tulipokuwa tumekaa.

Utulivu wao haukuwa mkubwa kabisa, kila wakati walikuwa wakinishikashika maeneo ya zipu huku wengine wakitaka kuifungua na kuana mchezo wao, nilikuwa makini sana.

Kwa muda mwingi, Juliet alikuwa akinipigia simu lakini sikutaka kupokea kabisa, nilikuwa naiangalia simu na kisha kuichunia.

Hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu na mwisho wa siku kuamua kuipokea. Kitu cha kwanza kabisa kukisikia ilikuwa ni sauti ya wanawake wale, nahisi alichanganyikiwa.

“Upo wapi?” aliniuliza, sauti za wanawake zilikuwa zimemchanganya.
“Nipo kazini.”
“Kazini?”
“Ndiyo.”

“Mbona nasikia kelele za wanawake mpenzi na muziki?” aliniuliza, sikutaka kulijibu swali hilo, nikakata simu.
 
SEHEMU YA 24

Mwanamke, hebu jifikirie, unampigia simu mumeo arudi nyumbani, anakwambia yupo kazini, unapompigia simu saa saba, anakwambia yupo kazini lakini unasikia sauti za wanawake wakicheka, unapomuuliza, anakwambia yupo kazini, ila unapouliza kama ni kweli yupo kazini, anakata simu. Utajisikiaje? Utaweza kuvumilia na wakakati wewe ni mjauzito?

Hakika aliumia, lakini haikuwa na jinsi, alitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba nilikuwa nikilipiza kisasi bila kujua, kama alivyoniumiza, na mimi nilitaka kumuumiza.

Siku hiyo sikurudi nyumbani, nilipotoka hapo baa nikaelekea hotelini na kulala, siku iliyofuata, nikaenda ofisini na kurudi nyumbani.

“Mume wangu! Ulikuwa wapi usiku wa jana?” aliniuliza, alionekana kutia huruma, machozi yalikuwa yakimlenga.
“Nilikuwa kazini mpenzi.”
“Pole sana na kazi, nahisi zilikuwa nyingi sana.

Ila naomba unionee huruma na hali niliyokuwa nayo mpenzi,” aliniambia kwa sauti ya upole. Japokuwa nilitakiwa kumuonea huruma, wakati huo ulikuwa ni kuonyesha sura ya mbuzi tu au kuvaa miwani ya bati.

“Samahani mke wangu.”
Sikutaka kuongea sana, nilichokifanya ni kuvua nguo zangu na kuelekea bafuni kuoga.

Kesho yake, nikajiandaa na kuelekea kazini huku ile nguo niliyokuwa nimeivaa nikiacha pakti tano za kondomu, tena pakti nne zilikuwa zimetumika zote na pakti moja zilikuwa zimebaki mbili tu.
 
SEHEMU YA 25

Niliporudi nyumbani usiku, kondomu zile sikuzikuta na wakati nguo zilikuwa zimefuliwa. Nilipomwangalia, macho yake yalikuwa mekundu hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amelia sana.

“Kuna nini mke wangu?” nilimuuliza.
“Hakuna kitu mpenzi. Pumzika tu.”
“Hapana, siwezi kupumzika na wakati upo kwenye hai hii.”
“Naomba upumzike.”
Sawa.”

Wakati yeye akiwa na uchungu wa moyo, kwangu ilikuwa ni furaha tele. Ilipofika saa sita na nusu usiku, simu yangu ikaanza kuita, alikuwa amelala ila kwa sababu nilipanga kuipokea simu hiyo, hivyo sikutaka kulala japokuwa nami nilijifanya kulala.

Alipoisikia simu yangu inaita, akashtuka, nikaipokea na kuanza kuongea. Ilisikika sauti ya mwanamke upande wa pili, alikuwa ni Getrude, msichana aliyekuwa mfanyakazi wangu. Aliongea kwa kulalamika kwamba alikuwa amenimisi na alitaka kuniona, nilichokifanya ni kuinuka na kwenda kuoga.

Wakati nipo huko, meseji ikaingia simuni mwangu, nilisikia mlio huo na nilimpanga kwamba baada ya kuongea naye ilikuwa ni lazima atume meseji ambayo iliandikwa hivi ‘Baby, naomba uje, mwili unaniwasha, nahisi kuna vijidudu vinanitembelea mwilini.

Njoo uupoze moyo wangu kama jana na juzi ulivyonikuna vilivyo. Achana na huyo mjauzito, hawezi kukuridhisha, njoo kwangu nikupe mahaba motomoto mpaka uchanganyikiwe na kuona kwamba watoto wa kitanga tunayajua mapenzi. Kama unanipenda zaidi ya mke wako, njoo, ila kama mke wako ni zaidi yangu, usije’.
Nilipomaliza kuoga, nikarudi chumbani.

Alikuwa akilia sana kwani aliusoma huo ujumbe, nikajifanya kutokujali na wala sikumuuliza kulikuwa na nini, nikavaa na kuondoka zangu huku nikimuacha akilia kama mtoto.
Nilichokuwa nikitaka ni kumuumiza tu.
*
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…