Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu.

Ulimwengu Wa Plastiki Au Dunia Ya Watu.
1551810998800-png.1038843


Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba aliwai kusema “Ndugu zangu sina budi kuwa kumbusha kuwa siku hizi kuna Wakimbizi wa Mazingira, watu wanaharibu mazingira katika maeneo yao na kuhamia maeneo mengine, jitihada za maendeleo zote hazitakuwa na maana kama hatutatunza Mazingira yetu”.

Raisi wa Awamu ya Pili Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi alisema “Umaskini na uharibifu wa Mazingira ni watoto mapacha na mama yao ni Ujinga.”

Mwanadamu ndio chanzo cha uharibifu wa Mazingira na uharibifu huo unasababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utupaji wa taka ovyo zikiwemo taka za plastiki.

Plastiki utengenezwa kwa kiasi kikubwa na malighafi aina ya organic polymers. Polyethylene na nylon ni mfano mzuri wa organic polymers. Kauli mbiu ya mazingira ya mwaka 2018 duniani kote ilisema "Kupiga vita uchafuzi wa plastiki" (Beat Plastic Pollution) na kilele cha kuadhimisha siku hiyo ya mazingira kilifanyika nchini India. Huku kauli mbiu ya mazingira mwaka 2018 Nchini Tanzania ikisema "Nitunze Nikutunze" ikilenga kusisitiza utumiaji wa nishati mbadala na watu kuachana na matumizi ya mkaa.

Kwa nini Plastiki? (Tuangalie Historia): Watafiti wanasema kuanzia mwaka 1950 mpaka 1970 asilimia ndogo sana ya plastiki ilikuwa ikizalishwa duniani kote. Kwa sababu hiyo waliweza kusimamia vizuri na kuzuia madhara yatokanayo na plastiki katika mazingira asilia. Lakini kuanzia mwaka 1990 mpaka hivi sasa, uchafu wa plastiki ambao umezalishwa ni mara tatu ya miongo miwili kutoka mwaka 1950 mpaka mwaka 1960 na kutoka mwaka 1960 mpaka mwaka 1970. Watafiti wamekadiria zaidi ya tani bilioni 8.3 za plastiki zimezalishwa kuanzia mwaka 1950 mpaka sasa. Asilimia 60 kati ya hizo zimeishia katika mazingira asilia. Pia kuanzia mwaka 1950 mpaka hivi sasa kiwango cha uzalishaji wa plastiki kimekuwa kwa kiasi kubwa hapa duniani.


Uchafu wa Plastiki kwa sasa umezagaa karibu kila sehemu ya Dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa ni zama za Mwanadamu (Anthropocene era) na nimatokeo ya kuongezeka kwa shughuli za mwanadamu katika Dunia. Leo hii Mwanadamu uzalisha Tani milioni 300 za uchafu wa Plastiki kwa mwaka duniani, huku ikikadiriwa kuwa sawa na idadi ya uzito wa watu Duniani. Chupa za Plastiki milioni 1 ununuliwa kila baada ya dakika moja Duniani. Huku mifuko ya Plastiki trilioni 5 utumika mara moja tu kabla ya kutupwa kila mwaka (single-use plastic bags). Huku nusu ya plastiki zote zinazotengenezwa duniani zinatengenezwa kwa madhumuni ya kutumika mara moja tu, Ni Asilimia 9 tu ya uchafu wote wa Plastiki ambao unazalishwa unakuwa recycled. Huku asilimia 12 uchomwa moto, wakati asilimia 79 kati ya hizo ubakia katika mazingira yetu ya asili.

Mito 10 inayobeba zaidi ya asilimia 90 ya uchafu wa plastiki na kupeleka baharini.
1. Chang Jiang (Yangtze River) 1,469,481 tani
2. Indus 164,332 tani
3. Huang He (Yellow River) 124,249 tani
4. Hai He 91,858 tani
5. Nile 84,792 tani
6. Meghna, Brahmaputra, Ganges 72,845 tani
7. Zhujiang (Pearl River) 52,958 tani
8. Amur 38,267 tani
9. Niger 35,196 tani
10. Mekong 33,431 tani

Source: Data from “Export of Plastic Debris by Rivers into the Sea” by Christian Schmidt, Tobias Krauth, and Stephan Wagner, published in Environmental Science & Technology (2017)

Madhara ya Uchafu wa Plastiki katika Mazingira ya Viumbe hai
Uchafu wa plastiki una madhara makubwa sana kwa viumbe hai wote, wakubwa na wadogo. Sumu ipatikanayo kwenye uchafu plastiki kwa mfano Diethylhexyl Phthalate usababisha kansa kwa viumbe hai.
Plastiki inaweza kuharibu mfumo wa chakula na kusababisha vifo kwa samaki na wanyama wakubwa kwa kumeza kimakosa, kwa mfano Kasa (Sea Turtle), Nyangumi na Papa.
Uchafu wa plastiki unapochomwa kama utavuta moshi wake kwa muda mrefu au mara kwa mara, basi kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha madhara katika mfumo wa upumuaji na kuharibu utendaji kazi wa mfumo wa Homoni kwa Binadamu. Kemikali aina ya BPA (Bisphenol A) inayopatikana kwenye plastiki uharibu utendaji kazi wa Thyroid Hormone na Sex Hormone kwa Binadamu.


Njia mbadala za kupunguza na kuzuia uchafuzi wa plastiki.
👉
Kutoa elimu na athari za uchafu wa plastiki kwa mazingira.
👉 Kuweka njia nzuri na salama za kurecycle uchafu wa plastiki.
👉 Kuweka faini na sheria za kuzuia aina za bidhaa za plastiki ambazo hutumika mara moja tu na zinamadhara makubwa katika mazingira yetu, mfano mzuri mifuko ya nylon na chupa za plastiki
👉 Kuweka sera ya mazingira ambayo itawabana watengenezaji na watumiaji wa bidhaa za plastiki ambao watakiuka maadili ya utupaji, utengenezaji na uhifadhi wa taka za plastiki.

Mazingira ni yetu sote ni haki yetu tuyalinde, tuyatunze na kuyahifadhi kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae. Mazingira ni Uhai.
Inaonyesha umebobea kwenye maswala ya mazingira. Hongera sana mate
 
Ahsante sana mate, I'm waiting for your general reply about this issue of plastic pollution.
I hope you can add something about this issue.
Mkuu sina elimu sana na maswala ya mazingira. Ila napenda na kuthamini Uhai wa kila kiumbe kuanzia wanyama,mimea na wadudu. Hivyo basi hua najitahidi kuweka mazingira wezeshi ya kila kiumbe kiweze kuishi vyema bila bugudha. Nipo radhi nisitoe buibui ukutani ili waishi vyema.
Btw napenda sana nature, napenda kutembea kwenye miti
 
Mkuu sina elimu sana na maswala ya mazingira. Ila napenda na kuthamini Uhai wa kila kiumbe kuanzia wanyama,mimea na wadudu. Hivyo basi hua najitahidi kuweka mazingira wezeshi ya kila kiumbe kiweze kuishi vyema bila bugudha. Nipo radhi nisitoe buibui ukutani ili waishi vyema.
Btw napenda sana nature, napenda kutembea kwenye miti
Ni jambo jema kupenda mazingira yetu yanayotuzunguka kwanzia Viumbe hai na visivyohai, kwa sababu kila kimoja kinafanya kazi yake kulingana na nafasi yake kwenye Mazingira. Hili kutengeneza chain ya mtegemeano au muunganiko kwenye mazingira (Ecosystem). Thats why, when you define environment you have to include two things:-
(1) Living Things
(2)Non-Living Things

So interaction between Living things and Non-living things = Environment.
 
Ni jambo jema kupenda mazingira yetu yanayotuzunguka kwanzia Viumbe hai na visivyohai, kwa sababu kila kimoja kinafanya kazi yake kulingana na nafasi yake kwenye Mazingira. Hili kutengeneza chain ya mtegemeano au muunganiko kwenye mazingira (Ecosystem). Thats why, when you define environment you have to include two things:-
(1) Living Things
(2)Non-Living Things

So interaction between Living things and Non-living things = Environment.
Naam kila kiumbe kinahaki ya kuishi katika dunia hii kwa kuzingatia ecosystem yake. Kma unapenda kusaidia watu/kuifanya dunia iwe mahali salama kwa viumbe basi tutunze mazingira maana ndio urithi wetu kwa ajili ya existence ya viumbe.
 
Back
Top Bottom