Ulimwengu wa kujitambua

Ulimwengu wa kujitambua

Watu ambao hawako huru – kiakili, kiroho au kihisia – mara nyingi hujifungia kwenye ulimwengu wa hisia zao wenyewe. Badala ya kusikiliza kwa moyo ulio wazi, wao huchuja kila kitu kwa kipimo cha “kinanifanya nijisikieje?” badala ya “je, hiki ni cha kweli?”

Wanapokutana na ujumbe wa kweli, lakini usioendana na hisia zao, hulikataa au kupinga. Hii ni kwa sababu ndani yao kuna hofu ya kukabiliana na ukweli usiofurahisha au kubadilika.

Kwa mfano: mtu aliyeumizwa na mapenzi anaweza akakataa kusikia habari yoyote ya msamaha au upendo wa kweli, si kwa sababu si sahihi, bali kwa sababu moyo wake haujapona.

Kwa hiyo mtu ambaye hajaweka uhuru wa ndani, anakuwa tayari kupokea tu yale yanayopendeleza hisia zake – hata kama si ya kweli. Hii ndiyo maana uhuru wa kiakili na kiroho ni muhimu. Unapokuwa huru ndani yako, unaweza kusikiliza ukweli hata kama unauma, unaweza kujifunza kutoka kwa wengine hata kama hawaeleweki kwako, na unaweza kuchagua njia ya ukuaji badala ya kujificha kwenye faraja ya hisia zako.
 
🤏🏾👴🏾PAUSE TAKATIFU...

Kuna nguvu katika utulivu.

Katika wakati wa utulivu kati ya hatua na mawazo, roho yako inazungumza.

Inanong'ona mwongozo, inatoa uwazi, na kukukumbusha ubinafsi wako.

Unapotua, unaupa ulimwengu nafasi kujibu. Unatengeneza nafasi kwa pumzi yako mwenyewe.

Funga macho yako.

+ Vuta polepole, ukihisi kuongezeka kwa kifua chako.

Pumua kwa upole, Kupunguza kelele.

Hapa - katika utulivu huu - uko nyumbani.

Ni lini mara ya mwisho ulijiruhusu kuwa hv?

…‡Utashi huru
 
1. Binadamu kama mpokeaji wa maarifa
Binadamu hapati maarifa kutoka kwao wenyewe moja kwa moja. Wanafumbuliwa, wanafundishwa, wanajifunza kupitia uzoefu, mazingira, roho, au chanzo kikubwa zaidi — iwe ni Mungu, ulimwengu, au “akasha” (sehemu ya hifadhi ya maarifa ya kiroho).

Hii ina maana kwamba:
  • Maarifa hayazaliwi ndani ya binadamu bali yanapokewa.
  • Hili linamweka binadamu kama “chombo” au mteka wa mwanga — yaani anayechukua, kuchakata, na kutumia maarifa aliyopokea.

2. Maarifa yanatoka wapi?
Maarifa yanaweza:
  • Kutoka kwa Chanzo cha Ulimwengu (Mungu, Chanzo Kikuu, Nuru)
  • Kupitia uzoefu wa maisha
  • Kupitia mtiririko wa kiroho (intuition, ndoto, mafunuo)
  • Au hata kupitia viumbe wa mwanga au viumbe vya kiroho.

3. Binadamu ana jukumu gani basi?
  • Kupokea kwa moyo ulio wazi.
  • Kuchuja kwa hekima (sio kila maarifa ni ya mwanga).
  • Kutumia kwa uumbaji, uponyaji, au kujenga.
  • Kushirikisha wengine kwa upendo na kusudi.
MENEMENE TEKERI NA PERESI leo dada To yeye
Ujumbe huu usiponijenga bas mimi sijajua bado dhumuni la kuishi.Mleta mada asante sana 🙏
 
SHERIA YA KUTOA.

Kutoa ni kupokea. Kutoa na kupokea maisha. Kila uhusiano ni wa kutoa na kuchukua.

Sheria ya Utoaji inasema ukitaka kupokea kitu kwanza wape wengine.

Njia bora ya kupata kile unachotaka ni kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka.

Kutoa na kupokea, kwa nia sahihi, huruhusu mtiririko wa nguvu katika Ulimwengu kutoa kwa Mpaji na kwa Mpokeaji.

Kwa muda unaotoa utakuwa unapokea.

…‡Utashi huru
 
🤷🏾‍♂️JE UAMSHO WA KIROHO NI NINI?

Mwamko wa Kiroho ni pale mtu anapofahamu asili yake halisi na utu wake wa kipekee.

Wakati hii itatokea katika maisha yako, utakuwa na hisia mpya ya kuona vitu na ulimwengu unaokuzunguka.

Utaanza kuamini maisha na kutumia sauti yako ya ndani wakati wa kufanya maamuzi.

Utaweza kukubali ⚫ hisia zako na kuzihisi kweli, sio kuzikandamiza kupitia uraibu na mifumo hasi,

Utaachilia mifumo ya zamani ambapo utaguswa katika maisha yako kulingana na kiwewe chako na uzoefu wa zamani.

Utajua kwamba jambo hilo hilo halitatokea tena kwa sababu unavutia kile unachotaka maishani, na unaweza kuachilia njia za zamani za kufikiria.

Unapopata Uamsho wa Kiroho, maswali mengi yatakuja akilini mwako, na utajiuliza maswali mengi kwa sababu ego yako itajaribu kutafuta visingizio vyote vya kukuweka katika hofu na mifumo ya zamani.
 
ELIMU YA VITO NDANI YA MAANDIKO YA KALE.

Tutaangazia maandiko kutoka kwenye Kitabu cha cha Mafumbo (The Book of Codes) maarufu Biblia.

Bila shaka mnajua kwa nini The Bible ni 'the most authentic book' na nilishasema mara nyingi sana, kwa nini napenda kuirejelea.

Msiojua au mliosahau niulizeni.

This is my favourable book anyway.

Nimefanya Bible Research wakati nafanya Masters ya Theology & Divinity, najua safari ya hiki kitabu, tangu mwaka 325AD.

Tuendelee . . .

Kwenye Biblia (The Book of Laws), wanazuoni, wanaizungumzia milango 12 ya mbinguni, lakini kimsingi (basically) wanazungumzia habari za milango 12 ya Nyota, kwa sababu kule kunakoitwa mbinguni ni kwenye ulimwengu wa kinyota (cosmic/ astral world)

Wanasema kila mlango umetengenezwa kwa VITO VYA THAMANI (gemstones), kila mlango tofauti na mwingine!

Inabidi utumie kichwa (akili/ elimu) badala ya moyo (Imani/ hisia) kufumbua fumbo hili.

Mwandishi anazungumzia Vito vinavyoendana na Nyota lakini katika mkutadha wa kile ambacho yeye alikusudia kukiwasilisha kwa wasomaji wake.

Ni muhimu watu wajue kuwa Biblia si kitabu cha dini fulani, ni kitabu cha mafumbo kwa karne nyingi.
Kina mafumbo (siri) ambayo ukiyafumbua utafanikiwa kwenye haya maisha.

Ndio maana ukienda makanisani utakikuta.

Misikitini utakikuta.

Kwenye mahekalu na masinagogi utakikuta.

Kwenye secret societies kipo pia.

Kwa waganga wa kienyeji utakikuta.

Kwa wachawi kipo.

Kwa wasio na dini utakikuta mpaka wengine wanakitumia kama 'mto' (pillow) kulalia ili wasisumbuliwe na wachawi!🤪

Mimi na wanautambuzi wengine tunakiita THE BOOK OF LAWS (Kitabu cha Sheria/ Kanuni) na ni the most authentic book!

Sasa kwenye hicho kitabu, ukisoma utaona kinawazungumzia wataalam au wabobevu wa masuala ya Nyota (the wisemen) au mamajusi (kiswahili), kuwa walipokuwa huko kwao Mesopotamia (Iran ya sasa), waliiona Nyota ya Simba (Leo) ikiangaza kwenye ulimwengu wa kinyota (cosmic World) na kwa kutumia vifaa vyao vya kazi, kwa mujibu wa teknolojia ya wakati ule, wakaanza kuifuatilia mpaka walipofika Bethlehem ya Uyahudi alipokuwa amezaliwa Yesu Kristo, almaarufu Bwana Yesu!

KUNA AINA TANO ZA KUSOMA NYOTA YA MTU, MIE NAJUA NNE NA UWA NAFUNDISHA MBILI TU.

Kuna dimensions mbalimbali za kinyota, wengine wanasema mtu ana nyota nyingi, ni sawa tu; lakini the accurate ni ile ya sun sign, ambayo inazingatia birth date na hapo ndipo tunapata kile tunachokiita NATAL/ BIRTH CHART.
Wote humu ndani mnaelewa bila shaka, what's all about the Natal Chart!

Tuendelee . . .

Hao the 'wisemen' walifuata utaratibu wa kidiplomasia mpaka wakafika mahali pale alipozaliwa Yesu, wakakaribishwa ndani.

Kabla hawajafanya lolote WALIMSUJUDIA!

Kwa nini?

Ili wasamehewe dhambi?
HAPANA!

Ili waokolewe?
HAPANA!

Ili iweje sasa?

Kwa nini wakisujudie kichanga kilicholala bila kutambua lolote?

JIBU: Hawakuwa wakisujudia kichanga, bali nyota ya utawala (ufalme), ambayo ni Nyota ya Simba (Leo zodiac sign)

Mfalme husujudiwa!

Mtu hawi Mfalme baada ya kuwa Mfalme, anakuwa Mfalme kwa asili yake, yaani kwa kuzaliwa!

Mfalme ni Mtawala, ni kiongozi wa watu, ndivyo ilivyo Nyota ya Simba!

Kwenye dini, Yesu anaitwa Simba wa KABILA la Yuda, yaani Mtawala au Mfalme wa Wayahudi!

Waswahili wamemwimbia nyimbo "Simba wa Yuda anaunguruma" nafikiri walimaanisha Mfalme anatoa amri au maelekezo!

Wale mamajusi (the wisemen) baada ya kukaa kwa siku kadhaa, kabla hawajaondoka, walifungua mizigo (hazina) yao wakachukua DHAHABU pamoja na UVUMBA na MANEMANE, wakawakabidhi wazazi wa Yesu kisha wakaondoka.

Kwa nini Dhahabu na si madini mengine?

Kwa sababu DHAHABU pamoja na mambo mengine, hutumika kufyonza nishati hasi (nguvu mbaya) kwa watu wa nyota ya Simba, lakini pia huvuta nguvu ya kifalme kutoka kwa Mfalme Jua ambaye ndiye Mtawala wa Nyota ya Simba!
Kwa hiyo watu wenye nyota ya Simba wakivaa miilini mwao vitu vya madini ya Dhahabu kama Pete, Cheni, Bracelets nk, wanakuwa wanajikinga na mambo mengi mabaya, lakini pia inawasaidia kung'arisha nyota zao kama Jua na kuwafanya wawe na mvuto usio wa kawaida..

UVUMBA na MANEMANE ni mafusho ambayo huchomwa ili kuondoa nuksi, mikosi, mabalaa na mambo mabaya mabaya kwa watu wa nyota ya Simba.
Kwenye mafusho ya Nyota ya Simba, uwa ni lazima tutie ndani uvumba na manemane, kwa sababu ndani yake kuna energy ya utakaso wa nyota husika.

Ndio maana the wisemen (mamajusi) waliacha hizo bidhaa kwa ajili ya Yesu, ili atimize kusudi lake.

Tafuta Biblia usome Matthew 2:1-9,11

Imeandikwa;
"Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,
"Yuko wapi yeye aliyezaliwa MFALME WA WAYAHUDI?
Kwa maana TULIIONA NYOTA YAKE MASHARIKI, nasi tumekuja kumsujudia."
Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.
Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii kusema;
"Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa KWAKO ATATOKA MTAWALA Atakayewachunga watu wangu Israeli."
Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, "Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie."

Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; DHAHABU na UVUMBA na MANEMANE."

Soma kwa utulivu utaelewa kwa nini kila mtu anawakilishwa na Nyota fulani!

Wewe unapokuwa ndipo na nyota yako inapokuwa.
Wewe na Nyota yako ni UMOJA, you're inseparable.
Kwa lugha rahisi nyota yako ni wewe na wewe ni nyota yako.

Ili mtu mbaya akuharibie, hahitaji mambo mengi, bali kuijua nyota yako na kucheza nayo, maana Nyota ikifanyiwa 'ulozi' ni wewe unakuwa umelogwa.

Ndio maana wale wanaosema tutakuombea nyota yako irudi, ni waongo wakubwa!

Wale pia wanaosema watakupa hirizi ili nyota yako ing'are ni matapeli kama matapeli wengine. Wote hao ni wapigaji!

Kwa nini?

1. Hakuna maombi ya kurejesha nyota.

2. Hakuna hirizi au dawa za aina moja zinazosafisha nyota zote.

Nyota haiibiwi kabisa wala haichukuliwi; isipokuwa inaweza kufunikwa, kuzibwa na kuchafuliwa.

Kama itaibiwa au kuchukuliwa, basi mtu atakuwa chizi, zezeta au msukule (namaanisha machoni kama mtu, lakini kiuhalisia anakuwa sio mtu)

ELEWA HILO, WALA USIJE UKADANGANYWA!

Pia Kila Nyota husafishwa na aina tofauti ya visafishaji au vitakasaji (zodiac cleansers), ingawa baadhi ya Nyota kwa sbb za 'mfanano' wake kwa namna moja au nyingine, zinaweza kutakaswa, kuoshwa, kusafishwa kwa madini/ mawe/ Vito vya aina fulani na au mafusho yanayofanana, kama vile Nyota za Ng'ombe (Taurus) na Mapacha (Gemini) hung'arishwa na madini ya ZUMARIDI (Emerald)

Ngoja niwaletee na maandiko mengine yanayozungumzia mawe au vito muone umuhimu au faida ya kuwa navyo.

VITO NA MADINI MAARUFU AMBAVYO BIBLIA INADAI NDIVYO VIMETUMIKA KUUJENGA MJI MTAKATIFU WA MBINGUNI:

1. Kuna Gold (Dhahabu)

2. Diamond (Almasi)

3. Jasper (Yaspi),

4. Sapphire (Yakuti),

5. Chalcedony (Kalkedoni),

6. Emerald (Zumaridi),

7. Sardonyx (Sadoniki),

8. Sardius (Sardio),

9. Chrysolite (Krizolite),

10. Beryl (Berili),

11. Topaz (Topaz),

12. Chrysoprasus (Krisopraso),

13. Jacinth (Yakintho)

na

14. Amethyst (Amethisto)

Ni kwa mujibu wa Kitabu cha Ufunuo (Revelation 21:10-22)

"Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu;
wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa KITO CHENYE THAMANI NYINGI kama kito cha YASPI, safi kama bilauri;
ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli.
Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu.

Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.
Na yeye aliyesema nami alikuwa na mwanzi wa dhahabu, apate kuupima huo mji, na milango yake, na ukuta wake.
Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Akaupima ukuta wake, ukapata dhiraa mia na arobaini na nne, kwa kipimo cha kibinadamu, maana yake, cha malaika.
Na majenzi ya ule ukuta wake yalikuwa ya YASPI, na mji ule ulikuwa wa DHAHABU safi, mfano wa kioo safi.
Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa VITO VYA THAMANI vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa YASPI; wa pili YAKUTI SAMAWI; wa tatu KALKEDONI; wa nne ZUMARIDI;
wa tano SARDONIKI; wa sita AKIKI; wa saba KRISOLITHO; wa nane ZABARAJADI; wa kenda YAKUTI YA MANJANO; wa kumi KRISOPRASO; wa kumi na moja HIAKINTHO; wa kumi na mbili AMETHISTO.

Na ile milango kumi na miwili ni LULU kumi na mbili; kila mlango ni lulu moja. Na njia ya mji ni DHAHABU safi kama kioo kiangavu.

Kuna kitu mmekielewa?

Kitu gani hicho)

Tueleze kwa ufupi.

Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

DOGOLI KINYAMKELA ☠️ 💀 (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
IMG-20250926-WA0287(2).jpg
 
📚 MWENDELEZO WA ELIMU ZA SIRI 📚
NAMBA, MAUMBO NA ISHARA
sehemu ya 1️⃣


Kwa wiki tatu mfululizo tumekuwa tukijifunza Elimu ya Namba, tukiona jinsi namba zinavyobeba mitetemo, siri za maisha, na nguvu za roho. Lakini safari hii hatuaishii pale: namba peke yake hazitoshi.

Ili kuelewa lugha ya ulimwengu kwa kina, tunapaswa kuunganisha:

▪️Namba .....vibration na mtiririko wa maisha.

▪️Maumbo .... muundo wa nishati na nguvu zinavyopangwa.

▪️Ishara ..... alama na ujumbe wa roho kutoka ndoto, maono, na historia.

👉Kauli kuu ... Namba + Maumbo + Ishara = Lugha kamili ya Ulimwengu/universla language

Hii ndiyo sababu ndoto, maono, na ramani za kale zimetengenezwa kwa alama na mifano. Ukiunganisha hizi tatu, unapata ufahamu wa ndani wa roho, siri za maisha, na mwelekeo wa kweli wa ulimwengu.

Kwa maneno mengine, sasa tunaanza kuona chini ya uso wa mambo, kugundua mchoro wa kweli wa maisha na roho, si tu idadi au matukio. Huu ni mwanzo wa safari ya ndani ya roho kupitia elimu ya siri.

⚫ ELIMU YA ISHARA NA NGUVU ZAKE 📖

Nakupa Dondoo Kuu

▪️1. Kila ishara ni lugha ya ulimwengu wa roho
Kabla ya maneno na maandiko, ulimwengu uliwasiliana kwa alama na vibration.
Ndiyo maana mtu akiona ndoto mara nyingi huona alama (mfano nyoka, maji, mlango) kuliko kusikia sentensi ndefu. Ishara ndiyo lugha ya asili ya roho.

▪️2. Ishara ni daraja kati ya roho na mwili
Akili ya kibinadamu ina mipaka; haiwezi kushusha moja kwa moja taarifa za kiroho.
Roho inashusha ujumbe kupitia alama ambazo ubongo unaweza kuzitafsiri.
Mfano: ukiona namba fulani ikijirudia mara kwa mara (11:11, 7:7:7), hiyo si ajali ...ni roho inakutumia daraja la ishara.

▪️3. Nguvu ya ishara iko kwenye mtetemo wake
Kila umbo lina frequency yake.
mfano 👇

✝️ Msalaba = Namba 4 ikimaanisha uimara, misingi, dunia yenye pande nne.

⭕ Duara = umilele, cycle isiyo na mwanzo wala mwisho ...ishara ya Mungu wa milele.

🔺 Pembetatu = nguvu tatu kuu (mwili, nafsi, roho / Baba, Mwana, Rohomtakatifu) Trinity

Kadri unavyotumia ishara fulani, unajiunganisha na mtetemo wake.

▪️4. Ishara hufungua milango ya fahamu ya ndani
Kila mtu ana akili ya ndani (subconscious mind). Ishara zikiliwa na kuonekana mara kwa mara, zinaingia huko na kufungua nguvu zilizolala.

Mfano: ✡ Nyota ya pembe sita = mbingu ↔ dunia. Ukitazama mara nyingi hujifungulia daraja la ndani la kuunganisha vitu vya rohoni na vya kimwili.

▪️5. Kila dini na tamaduni hutumia ishara
Hakuna dini wala tamaduni isiyo na ishara — zote zinatambua kuwa ishara ni lugha ya ulimwengu wa roho.

Ukristo .... ✝️ Msalaba = daraja la kifo na uzima, ulimwengu wa chini na wa juu.

Uislamu ....🌙 Mwezi na ⭐ Nyota = mwongozo wa mwanga gizani, cycle ya roho.

Uhindu .... ॐ (Om) = sauti ya uumbaji, vibration ya mwanzo wa ulimwengu.

Misri ya kale .... 👁 Jicho la Horus = kinga, kuona yasiyoonekana, ulinzi wa kiroho.

👆Hizi zote si mapambo tu, bali codes za siri ambazo zimebeba frequency na ujumbe wa rohoni.

✍️ukweli ni kwamba,Ishara si mapambo bali ni lugha ya Mungu, lugha ya roho, na njia ya kuwasiliana na nafsi ya ndani.
Utakapozielewa na kuzitumia, utajua mambo makubwa kabla hayajatokea na utajifunza kuishi kwa mwongozo wa juu zaidi.

🟢 ISHARA KUU NA TAFASIRI ZAKE 📖

👉1. Duara ⭕

Umilele, ukamilifu, cycle isiyo na mwanzo wala mwisho.
Umoja wa roho, nafsi, na mwili.
Pia huwakilisha mzunguko wa maisha (kuzaliwa, kukua, kufa, kuzaliwa upya).
Ndio maana pete ya ndoa ni duara ... ishara ya ahadi isiyo na kikomo.

👉2. Mstari/ ─

Ni njia, mwendo na uelekeo.
Huwakilisha nidhamu, sheria na kusogea kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Mstari ulionyooka = uthabiti na ukweli.
Mstari ulioinama au kuvunjika = changamoto, dhiki, au safari yenye mizunguko.

👉3. Msalaba ✝️ / +

Muunganiko wa juu...chini (mbingu na dunia) na kulia....kushoto (mambo ya wakati huu).
Namba 4, misingi ya dunia, pande nne, upepo wa dunia.
Ni ishara ya transition.... kupita hatua moja kwenda nyingine.

Ndiyo maana msalaba hutumika kwenye kaburi (kupita maisha ya kimwili ... ya kiroho).

👉4. Pembetatu 🔺 🔻

Ni ishara ya nguvu tatu (Trinity).

🔺 Pembetatu juu = mwanaume, chanya, moto, jua, kupanda.kwenye freemasonry huwakilishwa na bikali

🔻 Pembetatu chini = mwanamke, hasi, maji, mwezi, kupokea, tumbo la uzazi.katika masonic huwakilishwa na kipima pembe

Zikikutana 🔺+🔻= ✡ Nyota ya Daudi (umoja wa mbingu na dunia, chanya na hasi).

katika Alama kuu ya Masonic

bikali + kipima pembe vikeshikana, kisha katikati kuna herufi "G" kuwakilisha kizazi(Generation) kwani ulimwengu huundwa na Nguvu mbili,uwepo wa hizi nguvu ndio hufanya maisha kuwepo...umeelewa hapo❓

👉5. Spiral 🌀

Ukuaji, mageuzi, nguvu ya kuzunguka ya uhai.
Huwakilisha safari ya nafsi inayopanda ngazi kwa ngazi (ascension).
Ni ishara ya DNA ya mwanadamu na pia ya galaksi zinazozunguka.

Inatufundisha kuwa maisha si mstari wa moja kwa moja bali ni mizunguko inayopanda juu zaidi.

👉6. Jicho 👁

Ufahamu (consciousness), kuona yasiyoonekana.
Kinga ya kiroho, uwezo wa kutambua hatari kabla haijatokea.
Jicho la tatu (third eye) = kuona ukweli wa kiroho bila pazia.

🗣️Fumbo la Adamu na Hawa/Eva: walipokula tunda, walijua wako uchi .... walifunguliwa jicho la ndani, yaani waliona ukweli wa hali yao. hilo ni fumbo kuhusu kufungua jicho lako la 3 kupitia meditation,mfungo ,nguvu zako za mdani pale zinapopanda juu kuzunguka mti wa katikati/utiwa mgongo kwa mfano wa umbile la nyoka( nyoka wa bustani ni hizi nguvu ,mti ni uti wako wa mgongo,shamba ni mwili wako,kula tunda ni kufanya ibada ya meditation,kufunga,maombi n.k, hii mzungu hataki ufanye a.k.a bwana Mungu...umeelewa?

zamani liliitwa Jicho la Horus (Misri ya kale) = ulinzi, hekima na kuona ndani zaidi.

👉7. Nyota ⭐ / ✡

Safari ya nafsi, mwongozo wa nyota angani.

⭐ Nyota yenye pembe 5 = usawa wa nafsi, mwili, roho, akili na hisia.

✡ Nyota ya pembe 6 = muunganiko wa mbingu na dunia.

Nyota 7 = ngazi 7 za uumbaji, sayari 7 za jadi, na hatua 7 za mwanga.

Ndiyo maana manabii na wachawi wa kale walitumia nyota kwa ramani ya maisha.

👉8. Mwezi 🌙

Hisia, siri na subconscious mind.
Mwezi huongoza ndoto, maono na mizunguko ya kiroho.
Pia ni cycle ya uzazi (mwanamke ana mzunguko wa siku 28 kama mwezi).

Mwezi mpya = mwanzo mpya.

Mwezi mpevu (full moon) = ukamilifu na nguvu ya juu ya hisia.

👉9. Jua ☀️

Chanzo cha uhai, fahamu, mwanga na ubunifu.

Jua ndilo linalotoa maisha kwa mimea, wanyama na binadamu.
Pia huashiria uongozi, nguvu ya kiume na ubunifu wa ndani.

👇Ishara zingine za Jua:

🔘 Duara lenye nukta katikati (☉) ... ishara ya kale ya Jua. mfano kwenye uwanja wa mpira ile ni alama ya jua

Mandala za rangi ya manjano/zahabu pia mara nyingi huwakilisha jua.

👉10. Mandala

-Neno Mandala linatoka lugha ya Kisanskrit, likimaanisha “duara takatifu”.

-Ni mchoro wa duara wenye michoro ndani yake, unaowakilisha ramani ya roho na ulimwengu.

-Kila mandala hubeba vibration maalum kwa meditation au kuamsha fahamu.

Msamiati mwingine unaweza kutumia ni “Nguzo ya Duara” au “Alama ya Roho”. mfano nguzo za duara za kulia na kushoto kwenye kibaraza cha mahekalu,makanisa,majumba ya ibada n.k

Mfano 👉mandala yenye maua 8 huashiria usawa wa vipengele 8 vya maisha (mwili, roho, hisia, akili, jamii, kazi, mapumziko, uhusiano).

🔴 NGUVU ZA ISHARA.....

▪️Hulinda

Ishara zinaweza kuwa kama kinga.
Mfano: mtu akivaa msalaba, pete, au hirizi, si mapambo tu bali anaamini kuna nguvu ya kumlinda.
Ni kama kuweka alama ya “usinikaribie” kwa nguvu hasi.

▪️Hufungua akili ya tatu (Third Eye) 👁️
Ukijua ishara na kuzielewa, unafungua jicho la ndani linalokuonyesha zaidi ya kinachoonekana kwa macho.
Unaweza kuelewa ndoto zako, au kuona mtu ana mawazo gani hata kabla hajayasema.

▪️Huunganisha na nguvu za juu ✨
Ishara ni kama antena za redio.
Zinaunganisha roho yako na nyota, sayari au hata nguvu ya Mungu.
Mfano: mtu akitazama jua, au akitumia mandala, anahisi nguvu ya kuunganishwa na ulimwengu mzima.

▪️Lakini pia zinaweza kufunga mtu ⛓️
Ukibaki kwenye tafsiri ya juu juu, unakosea.
Mfano: mtu akidhani msalaba ni chuma tu, au mwezi ni mapambo tu angani, atabaki kwenye mwili bila kugusa roho yake halisi.
Ishara ni kama milango ... unaweza kuingia ndani (roho), au ukabaki mlangoni (kimwili).

HIVYO

👉Ishara ni lugha ya muumba na ulimwengu.
Ni alama za siri ambazo zinabeba ujumbe wa roho.
Ukiunganisha Ishara + Namba, unapata msimbo kamili wa maisha.

👉Mtu anayejua kusoma na kutafsiri ishara:
Anaweza kutambua mambo yatakayotokea kabla hayajatokea.
Anaweza kuona siri ambazo macho ya kawaida hayaoni.
Anaishi maisha ya ndani yenye mwanga na uelewa mkubwa.

👉Kwa kifupi: Ishara = Vifunguo vya roho kuelekea milango ya ukweli.

Umeelewa..❓
downloadfile-1.jpg
 
katika vitabu vya kidini imeandikwa kila nafsi itaonja mauti

wakati huo ukifika macho yatafunga pumzi zitasimama na Ruh itaondoka kwenye mwili

lakini nini kitatokea baada ya? Roho inaenda wapi?

baada ya kifo roho hupanda hadi mbingu 7 ambako huvumbua siri za ulimwengu

katika kila mbingu huona ulimwengu na ulimwengu tofauti mwishoni

roho inamfikia M/Mungu kisha inatumwa kwenye eneo la siri la barzakh

huko wanakula, vinywaji, kuongea na kusubiri sio dunia na sio akhera, bali mwelekeo tofauti, mahali pa siri na kanuni zake.

Ni halisi kuliko ulimwengu huu wa dunia.

🥸LEO UTAONA SAFARI YA ROHO KUPITIA MBINGU 7 KISHA KWENDA BARZAKH...

tunaendelea na mfululizo wetu kuhusu Ulimwengu Zilizofichwa

kama uko tayari tuanze hadi karne ya 19

watu waliamini kuwa dunia iko katikati ya jua mwezi na nyota zote zinazunguka dunia.

kulikuwa na mfumo mmoja tu wa marejeleo duniani, lakini Kitabu kimoja cha kidini kilikuwa imeandikwa...

Imeandikwa kuwa kuna mbingu 7, mifumo 7 tofauti mwaka 1838 ugunduzi ulifanywa

ilithibitishwa kwamba dunia inazunguka jua kwa mara ya kwanza ukweli huu ulionekana

kadiri miaka ilivyopita wanasayansi waligundua zaidi walitangaza ulimwengu ina muundo wa tabaka 7,

Kwenye vitabu vya kidini imeandikwa kwamba aliumba mbingu 7 kwa tabaka.

sasa wakati umefika wa kuzungumza juu ya kifo hivi karibuni roho itaanza safari yake hivi karibuni we kuwa tayari tu Kwa kuyaona maisha ya kweli

Tunaendelelea

kupitia mbingu 7 lakini kabla ya hapo roho itakutana na malaika wa mauti

na kuondolewa katika (gereza)kifungo cha mwili kwa ajili ya mwamini aliemuamini M/mungu wakati huu ni rahisi sana kwake

malaika wa mauti humtokea muumini katika umbo zuri na kuvuta roho (nafsi) kwa upole Sana kutoka ktk mwili wake.

kutoka kwa mwili na kusema oh roho safi (nafsi) toka na habari njema Leo kwako

katika rehema na uzuri wa M/Mungu, na Malaika warudishe roho kwa Mola wako Mlezi, Malaika wenye nyuso zinazo ng'aa kama jua☀️.

kubeba harufu nzuri ya paradise/peponi na Malaika kuzunguka roho(nafsi), inasemekana kuwa Enock/Idris (AS) alipowaona malaika hawa akishangazwa na uzuri wao ulimwengu sasa umeachwa nyuma🌎

kwa Roho huu ni wakati wa kukutana na M/Mungu(Chanzo) lakini kwa wale waliompuuza Mwenyezi Mungu na maamrisho yake kipindi wako hai wakihema hapa duniani ni tofauti sana Kwa upande wao, malaika wa giza na wakali wanawazunguka roho chafu kwa sanda za moto

Malaika wa mauti aseme roho yenye uovu njoo kwa hasira ya bwana wako aliekuumba

☝🏾👴🏾Moja ya mtume wa M/mungu Kwa wanadamu alisema kwamba kutoka kwa Roho na maumivu yake ni kama ngozi ichunwe kutoka ktk mwili wa mwanadamu hali ya kuwa bado ni mzima

ni kama kung'oa miiba kutoka kwa pamba inayorarua, yenye maumivu na mateso yasiyovumilika

utengano huu unachukua muda mrefu lakini ni mwanzo tu wa mateso Kwa waovu na msamaha Kwa watenda wema Kwa wanadamu wenzao na wanyama n.k

wakati huo macho yanakaribia kuuacha ulimwengu huu unaoonekana🌎 lakini ulimwengu wa Siri/ghaibu🌀 unafunguka.

_*Insha hii ya kimetafizikia*
By Dr
IMG-20251010-WA0298(2).jpg
matenyula herbalist 🌳🌱 Ali maalufu Dr dogoli kinyamkela ☠️💀
 
FOOLMOON IN TAURUS
Leo usikose kufanya ibada hii,

Mwezi Mkubwa (Supermoon) unakaribia.

Jiandaeni.

kuanzia leo tarehe 5/11, Mwezi Mkubwa utawasili utakuwa mwezi wa duara mkubwa na wenye mwanga zaidi wa mwaka kwa sababu utakuwa karibu zaidi na dunia, ukiwa mkubwa kwa hadi asilimia 14% na mkali kwa hadi asilimia 30% zaidi ya mwezi wa kawaida. Tayari tunaanza kuhisi nguvu zake zikijikusanya. Baadhi watauita “Beaver Moon.”

Mwezi huu utaleta mvutano kati ya kutaka kushikilia usalama na kukubali mabadiliko, hasa kwa kuwa utakuwa na uhusiano wa mvutano na sayari za Jupiter na Pluto hali itakayowasukuma watu katika matamanio ya kupitiliza, kutaka kujumuika na kufurahia maisha, lakini pia inaweza kusababisha mabadiliko makubwa katika mahusiano mengine ya muda mfupi, na mengine yakibadilisha kabisa uhusiano hadi yasirekebishike tena.

Siku chache zijazo zitakuwa na mchanganyiko wa utulivu na msisimko.
Wakati nguvu ya “faraja” inapogongana na nguvu ya “mabadiliko,” kunazuka mvutano nyumbani, kazini, au hata kwenye makundi ya kijamii. Watu wanaweza kujikuta wakijitumbukiza katika matendo ya kupitiliza ili kujifariji kama kutumia pesa hovyo, kula au kunywa kupita kiasi, au kutafuta starehe za haraka kisha baadaye kujikuta wakiwa wamechoka au wamevurugwa kihisia.

Hivyo basi, huu ni wakati wa kujizuia na kujitawala kihisia.
Usifanye jambo lolote wiki hii ambalo utalijutia kesho.
Kaa mtulivu au ondoka kwa amani.

Nguvu za mamlaka na udhibiti zitaanzag kuonekana wazi iwe ni kwa ushindani kati ya marafiki, migongano ya nguvu katika uhusiano, au malalamiko yaliyofichwa ambayo sasa yako tayari kulipuka kwa kisingizio kidogo tu. Kile kinachoanza kama mazungumzo ya kirafiki kinaweza haraka kubadilika kuwa jaribio la mipaka, hasa wakati vivuli vilivyofichwa vya kihisia vinapoibuka ghafla.

Kwa hiyo, kuwa mwangalifu usiahidi kupita uwezo wako, usitumie pesa hovyo, wala usilazimishe watu wakidhi mahitaji yako ya kihisia.
Epuka jaribu la kutaka kudhibiti matokeo au kutumia mvuto wako kuficha ukweli mgumu.

Kihisia na kisaikolojia, miezi mikubwa kama hii huamsha hisia kwa kiwango kikubwa wengi watasumbuliwa na kukosa usingizi na ndoto zenye nguvu.
Lakini upande chanya ni kwamba mwanga huu wa mwezi unaweza kufungua ubunifu wa ajabu, nguvu za kiroho, na uwezo wa kiintuisho (intuition). Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa wengi, hii itakuwa wiki yenye nguvu nzito sana.

Kumbuka, ulimwengu mzima kwa sasa unapitia mabadiliko makubwa, hata katika miili ya watu kimwili.
Kwa wale wanaopitia changamoto za kiakili au kihisia, tafuta msaada usiwe peke yako.
Na kwa wote wanaohisi nishati ni nzito sana wiki hii kumbuka, kuna mwanga mwishoni mwa handaki.
Hii ni kipindi kifupi tu.
Kivumilie. Kwa upendo.

Aliyeonywa mapema, amejiandaa.


Dr DOGOLI
IMG-20251105-WA0000.jpg
✍🏻
 
KUTOKA KATIKA KITABU CHA WAFU

thoth, kwa Kimisri “Tchehuti” au “Tehuti,” ambayetayari ametajwa kama mwandishi wa kitabu chenye maandishi yanayounda PER-T EM HRU, au Kitabu cha wafu,aliaminiwa na Wamisri kuwa wlalikuwa na moyo na akili ya Muumba, ambaye alikuwepo katika nyakati za mapema sana huko Misri

wenyeji walimuita “Pautti,” na wageni walimuita “Ra.”

Thoth pia ulikuwa “ulimi” wa Muumba,

Kuwa ulimi wa muumba inamaana Kuwa kila alichotamka nyakati zote yalikuwa ni mapenzi ya mungu mkuu, na kusema maneno ambayo aliamuru kila kiumbe na kilicho mbinguni na duniani kuwepo.

Maneno yake yalikuwa yenye nguvu na, anapotamka TU lazima hayo maneno yalete athari au madhara .

alitunga sheria ambazo kwazo mbingu, nchi na vitu vyote vya mbinguni vilitii;

aliamuru mwendo wa jua, mwezi, na nyota; aligunduauchoraji, ubunifu na sanaa; herufi za alfabeti na sanaa ya uandishi; na sayansi yahisabati.

Katika kipindi cha mwanzoni aliitwa"mwandishi (au katibu) wa Kampuni Kubwa yaMiungu,” na alipokuwa akiweka kumbukumbu ya kimbingu yamaneno na matendo ya wanadamu, alifahamika na vizazi vingi vya Wamisri kama “Malaika mtunza kumbukumbu.”

Alikuwa mvumbuzi wa kimwili na sheria za kimaadili

Alikuwa ni mtu wa HAKI;

Ndio maana Mashirika ya Miungu wa Mbinguni, naDunia, na Ulimwengu Mwingine ulimteua
“apime maneno na matendo” ya wanadamu.

Hukumu zake hazikuweza kubadilika, na akawa na nguvu zaidikatika Ulimwengu Mwingine kuliko Osiris mwenyewe.

Osiris alipata ushindi wake na Kuwekwa katika Jumba Kuu la Hukumu la Miungu kwa ustadi wa Thoth “mwenye hekima kinywani” kama Wakili, na kwa ushawishi wake kwa miungu mingine mbinguni.

Na kila mfuasi wa Osiris alitegemea utetezi wa Thoth ILI aweze kuachiliwa Siku ya Kiyama, na kumruzuku makao ya milele katika Ufalme wa Osiris.

.........ITAENDELEA........
MENEMENE TEKERI NA PERESI
 
"ANGALIZO :

Kama huna ukomavu wa Akili - Hizi Makala zinazopostiwa humu usisome, Hizi Elimu ni kwaajili ya wachache wenye Ukomavu wa Fikra. Waliyo huru kufikiri bila mipaka ya Kiimani.

Haya maarifa tangu zamani - hayakufundishwa kwa kila mtu walifundishwa wachache wenye ukomavu wa kifikra - na baadae haya Maarifa yalipigwa Marufuku kwa lengo la kuzima Fikra huru - watu wasijijue wao ni nani hasa.

-Na kisha yakabaki kwa watawala wa Ulimwengu wakajibinafisishia kwa lengo la kutawala wasio na ufahamu wa Kina.

Hivyo basi - kama mafundisho haya yanakukwaza na pengine yanatishia kuvunja imani yako uliyorithi tangu utoto wako nawewe hauko tayari kuwa huru.

{Ushauri Wangu Usisome }-Au Unfollow Page.

🙏🏿 Tukutane Kwa Makala zijazo:

© To Dr dogoli kinyamkela ☠️ 💀
 
Back
Top Bottom