Ulimwengu wa FTA Satellite TVs

Wapendwa msaada namna ya kuipata sport 24 maana nimeiangaikia kwa wiki mbili sasa bila mafanikio japo nilikua nazisaka Nss 12 channel ni nazo kutana nazo ni T-chad,Bfbs,bbc one,bbc two,bfbs extra,sky sport 1 uk na zingine nyingi bila hii sport 24 kuingia,pia naombeni kujua hivi kuna C band yenye nguvu kuliko hizi nilizo zizoea kama Galf star na Star gold?ahsanteni

Hapo upo kwenye signal yake kabisa jaribu kupandisha signal strength hiyo sky sport isome hata 80 hapo sport 24 itaingia bila shida ila km unatumia dish 6ft inabidi liwe orginal na lina vipimo kamili make mengine yanapunua ft6
 
Ahsante sana kiongozi.
Lakini unaweza kunisaidia pia uelekeo wa dishi hilo ili kupata arabsat 5A 30.5 East?
Na nawezaje kupata hiyo decoder ya str na ni kwa bei gani?
Mkuu umeuliza swali zuri kwa kifupi umeona angle inayotumika kukamata local chanel za itv,eatv na capital ni nyuzi 64 East ukiwa umesimama nyuma ya dish unapo lirudisha kushoto ndivyo nyuzi zinavyozidi kupungua 63, 60, 58, 45, 36, 30 mpaka nyuzi 0, na unapopeleka ungo kwenda kulia nyuzi huongezeka 65, 67, 70, 83, 84, 89, 90.... ,
kwa kukurahisishia kazi unatakiwa uwe na ujuzi au idea hata kidogo ya kukujulisha nini unataka,
Na endapo una risiva nzuri za kupandisha signal haraka utaenda mpaka kwenye kipengele cha instalation hapo utakuta orodha ya sat na utachagua hiyo sat unayoitaka halafu utaenda katika transponder zake , tafuta transponder yenye signal level kubwa kuliko zote eg 70%, 69%, au 72 % then anza kutafuta nyuzi ya satelite husika kama nllivyokuelekeza awali ila macho yako yawe kwenye tv uangalie msitari wa signal level kadri utakapo zungusha dish kwa mfumo wa anti clockwise utaona ukifikia angle flani signal level inapanda mpaka 70 au zaidi , acha kuzungusha dish nenda nyuma ya pipe ya dish ishushe na uipandishe im sure lazia utafanikiwa, Thanks.
 
Star TV sasa inapatikana katika satellite ya ABS 2 @75E Frequency 3821 V DVB-S SR 2400.Hii satellite iko pale ilipo Ting ila Star Tv iko kwenye C band tofauti na Ting ambayo iko Ku Band ila satellite ni ileile.

Imeongezeka channel ya muziki ya TV-E ya kampuni inayomiliki E-FM.Hii channel iko katika mfumo wa Full HD yaani resolution yake 1080i.Hii ni mara ya kwanza kupata channel ya HD kutoka hapa ikiwa FTA.Tp yake ni 3995H2333 DVB-S2 QPSK
 
Imeongezeka channel ya muziki ya TV-E ya kampuni inayomiliki E-FM.Hii channel iko katika mfumo wa Full HD yaani resolution yake 1080i.Hii ni mara ya kwanza kupata channel ya HD kutoka hapa ikiwa FTA.Tp yake ni 3995H2333 DVB-S2 QPSK
Mkuu vipi nikiongeza lnb nyingine kwenye dish la ft8 lililotazama 64°e, naweza pata hiyo startv..?
 
Mkuu vipi nikiongeza lnb nyingine kwenye dish la ft8 lililotazama 64°e, naweza pata hiyo startv..?
Ukijitahidi maana kuna kagape kakutosha hapo.
1481556755055.jpg
 
Back
Top Bottom