Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe?

taanzania tanzania nakupenda kwa moyo safiiiiiiiiiiiii nchi yangu tanzaniaaaaaaa nakupeendaaaaa
 
duu... unanikumbusha mbali san!! wangu nilimdanganya sana kuhusu my life lakini hata alipojua ukwel bado alizidikunipenda sasa yuko home na watoto wawil tunalea raha mustarehee!
 
duuu.. unanikumbusha mbali san!! wangu nilimdanganya sana kuhusu ma life lakin hata alipogundua ukweli alizidi kunipenda sas yuko home na watoto wawili tunalea!
 
Merrita maujanja ni kuuchunguza moyo wake ili kuibua kile alichonacho .....ukishe kijua basi utajipanga vilivyo kukabiliana na khali kama inavyojitokeza...........
 
ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe…..
(getting to know her/him)


hivi mwandani wako ulimtambuaje kuwa ndiye yeye?
hivi ni maujanja yepi wewe uliyatumia kumpima yeye?
ni vigezo vipi vilikutongoza hadi kujua umelamba dume?
hivi ni vichocheo vipi vilikufanya uone ya kuwa umewasili?
nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


kauli yake mwenyewe huitia kitanzini na kuishibisha azma zake!
aongeacho mara nyingi sicho kilichopo moyoni kwake wala!
tabasamu lake lalenga kuijenga kauli ambayo si lazima iwe na kweli!
kamwe kauli au hata tabasamu lake kuwa kioo cha moyo wake!
nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


kauli na taswira yake huoana na moyo wake masijala ya kukataa…
pindi moyo wake umekuasi kata katu basi shabaha wewe hulengwa…
bila haya au huruma jipu kukupasulia kuwa hakuhitaji nawe kulia..
na kwa kufanya hivyo huwa kajitendea mwenyewe ubinadamu..
nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja!
nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

Rutashubanyuma unatafuta nini best sasa unataka maujanja haya mkuu
 
Last edited by a moderator:
Nivea............................you never know........................what is bestowed for me.....................wahega husema....."Be prepared and your time will come."
 
Wajamani Nivea kweli yawezekana si kila king'aacho ni dhahabu walakini pia.....................................lakini baadi ya vingaavyo ni dhahabu pia...............naona unachofanya ni stereotyping..........................ya kuwa samaki mmoja akioza basi wote wameoza....there are hunk of men whoare really God-sent angels......................though they are very few.............................one of them I know because my sister marreid him and she is living in the moon of blissful consummation..............
 
nakumbuka tulikuwa tukifanya kazi pamoja.... kukawa na party ya ofc ya kumuaga Dean wa faculity yetu.. boyfriend aliyenileta hakurudi kunichukua na ilikuwa ni usiku saa 5.. imagine enzi hizo UDSM hapakuwa na usafiri wa public kama ilivyo sasa... huyu kaka alikuwa akiishi kimara lakini alitake trouble ya kwenda ubungo kuchukua taxi, akaja nayo UD na kunichukua hadi oysterbay nilikokuwa naishi... kwa kweli nilimpenda ghafla, nikajua ni mtu anaejali..; tangu wakati huo tukawa marafiki, marafiki weee mwisho tukaanza kutupana kitandani... nikamshit yule wa kwanza nikaendelea na huyo mpya.. alikuwa anajua kunijali, kunitunza, kunipa raha za mwili na roho... alimradi tu nilikufa nikaoza mwisho tukaamua kuoana.. hadi leo tuna miaka 22 pamoja tuna mtoto 1 yuko university na tunapendana utadhani tumekutana jana! life is sooo sweeeet
 
Dah! Mimi hata sikumbuki ilikuwaje, lakini baadaye niligundua kuwa nimechemsha nikaamua kujiweka pembeni kuepusha msongamano
 
hahaaa ingawa bado sijaamua kufanya maamuzi ikiwemo Uchumba na ndoa, mara ya kwanza sikujua nini kinaendelea maana mara ya kwanza tulienda kama vijana(wavulana na wasichana) kama 27 hivi katika Shule moja hapa mjini Dar. ilikuwa ni tour tu kubadilishana mawazo na kuwatembelea wanafunzi, tuliingia katika moja ya madarasa na baadhi ya wanafunzi tukawa tunabadilishana mawazo, baada ya muda kidogo kama nusu saa tukaondoka lakini mwalimu aliyekua katukaribisha pale shuleni akasema tuandike majina na hata namba zetu za simu, tukafanya hivyo mimi nikaandika mpaka namba yangu ya simu na jina langu, tukaagana tukaondoka zetu,

baada ya muda kama miezi mitatu simu yangu ikaita sauti ya binti ikawa inazungumza baada ya kuipokea simu, na akajitambulisha yeye ni fulani kutoka Oysterbay kuna siku mwezi wa tisa tulienda kuwatembelea shuleni kwao, akaniambia mpaka jina lake, nikamuuliza kama ni namba yake ni ya simu aliyonipigia akasema ni ya dada wa kazi pale kwao akaniambia any time ninaweza kumpigia, kuanzia hapo tukawa tunawasiliana mara kwa mara, na nilimchukulia kama mdogo wangu tu, kuna siku akaniambia tukutane Ubungo kuna mizigo alikua ameenda kuisubiria kutoka Arusha, na nilikua na hamu ya kumuona kweli maana sauti yake na maneno yake ya unyenyekevu nilikua na hamu sana ya kumuona.

nilijiandaa fasta nikawahi ilikua ni jumamosi mchana saa nane nilipanda gari mpaka ubungo , nikampigia simu nilipofika pale nikaonana nae tukasalimiana tukapiga story kidogo kama dakika tano akaja kaka yake akanitambulisha kwa Kaka kua mimi ni rafiki yake hapo ilikua mwaka 2009, kaka yake alikuja na gari tukasubiri mpaka gari likaja tukapokea mizigo tukaondoka zetu tukaenda mpaka Blue Pearl Hotel tukanywa juice tukawa tunapiga story kidogo, kaka yake binti alikua ni mpole na mtaratibu sana asiye na makuu, baada ya kumaliza kunywa juice tukaondoka zetu. waliniacha mitaa ya home Africa Sana-Sinza wao wakaenda zao home kwao Oysterbay..
tuliendelea kuwasiliana kama kawaida na siku tuliyoonana usiku wake tuliongea kama masaa matatu, niliendelea kuwasiliana huyu binti kila wakati na kila muda alinitumia sms za kunijulia hali.....

kwa miaka miwili niliendelea kuwasiliana nae hatimaye tukajikuta tumeshapendana, ameanza chuo mwaka jana nikawa napata nafasi ya kwenda kumtembelea chuoni kwake na nilikua napata muda mrefu wa kukaa nae na alinitambulisha kwa marafiki wenzake nikawa nimejulikana kama Mr Somebody pale chuoni...

Season ya Christmass mwaka jana nilikaa nae muda mrefu kama siku 9 tulifanya tour Ruaha national park na mambo mengine mengi, tumendelea kua pamoja kwa kila hali japo tunakwaruzana lakini maisha yansonga na ananijali na kunipenda sana sana...

mwezi wa tano mwaka huu nilipata ajali mbaya na yeye akatoroka Chuo akaja kunitembelea mpaka Dar, na hapo Mama yangu alimjua huyu Binti na alikua anakaa pale Hospital muda mrefu maana mimi nilikua hata sielewi nini kinaendelea maana nilikaa siku 6 bila fahamu, binti aliendelea kukaa mpaka nilipozinduka alikuwepo alinikumbati na kunibusu shavuni kwangu mbele ya mama yangu nilitoka Hospital baada ya kupata fahamu siku hiyo na binti akarudi tena Chuoni..

wakuu nina mengi ya kuandika lakini, that is How i Met her
 
Back
Top Bottom