Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe?

Kwanza lazima uwe na vigezo vya mtu unayemtaka na ndani yake uwe na vile vya muhimu ambavyo havina mjadala. Mfano.
1. Awe na elimu gani?
2. Una kikwazo cha dini/kabila?
3. Umri uwe range gani?
4. Kazi zipi hupendi mwenzi wako afanye?
5. Utumiaji wa kileo unakumbua?
6. Je unapenda shape gani. Mwembamba au mnene?
6. nk
Unapomwona kimya kimya unampitisha kwenye vigezo vyako kuona alivyo
Ukoridhika unapropose uone kama na wewe upo kwenye vigezo vyake. Sio vibaya ukampeleleza kujua anataka mtu wa aina gani kabla hujapropose.
 
Kwanza lazima uwe na vigezo vya mtu unayemtaka na ndani yake uwe na vile vya muhimu ambavyo havina mjadala. Mfano.
1. Awe na elimu gani?
2. Una kikwazo cha dini/kabila?
3. Umri uwe range gani?
4. Kazi zipi hupendi mwenzi wako afanye?
5. Utumiaji wa kileo unakumbua?
6. Je unapenda shape gani. Mwembamba au mnene?
6. nk
Unapomwona kimya kimya unampitisha kwenye vigezo vyako kuona alivyo
Ukoridhika unapropose uone kama na wewe upo kwenye vigezo vyake. Sio vibaya ukampeleleza kujua anataka mtu wa aina gani kabla hujapropose.

Penzi linafunika kila kitu.
 
Alikuja home from church..alikua amevaa sket ndefu, bahat nzur nlikuwa home mwenyewe..akakaa kidogo kuwasubiri wazazi alikuwa ametumwa..
So akawa anakata kucha kwa meno, nkachukua nailcut nkaaanza kumkata, from there ile care tuu ya kumkata kucha teyariii
 
Mi wangu alikuwa kishapangwa na wazazi lakini nilitaka kumjua kwanza kabla ya ndoa nilipoongea nae tu kwenye simu i knew he was the one mpaka sasa tuna miaka miwili ndani ya ndoa na tuna mtoto mmoja am happy to be with him.
 
Nakumbuka kuna chuma flani hivi nilienda kuliiba nyumbani kwao mida ya saa kumi na moja kasoro asubuhi kwa bahati mbaya nikakamatwa na baba yake, nikala kipigo cha kutosha kisha akawaamsha wanae(wote wa kike) basi nikapigwa mpaka na masufuria kisha wakanipeleka polisi,
Mida ya saa saba mchana nikaitwa na askari kutoka sero, ile kuja nakutana na sura ya moja ya wale walonipiga, tukachukuliwa mpaka kwenye ofisi flani tukaandika maelezo, yeye akasema ameamua kufuta kesi akawapa askari hela wakaturuhusu,
Tulipotoka nje hata hakuweza kunitazama, alichoniambia ni ''sio vizuri ulivyofanya" halafu akaondoka
Jioni akanitumia msg ya kuniomba msamaha kwa kile kipigo mimi sikumjibu kitu ila nae hakukata tamaa, baada ya wiki tukaanza kuchat then baada ya muda tukawa wapenzi, ila mtihani ilikua yeye kunitambulisha kwao,
Nashukuru sana kwa kunifundisha maisha na kunikataza wizi japo ilikua ni mara yangu ya kwanza na ya mwisho.
 
nakumbuka tulikuwa tukifanya kazi pamoja.... kukawa na party ya ofc ya kumuaga Dean wa faculity yetu.. boyfriend aliyenileta hakurudi kunichukua na ilikuwa ni usiku saa 5.. imagine enzi hizo UDSM hapakuwa na usafiri wa public kama ilivyo sasa... huyu kaka alikuwa akiishi kimara lakini alitake trouble ya kwenda ubungo kuchukua taxi, akaja nayo UD na kunichukua hadi oysterbay nilikokuwa naishi... kwa kweli nilimpenda ghafla, nikajua ni mtu anaejali..; tangu wakati huo tukawa marafiki, marafiki weee mwisho tukaanza kutupana kitandani... nikamshit yule wa kwanza nikaendelea na huyo mpya.. alikuwa anajua kunijali, kunitunza, kunipa raha za mwili na roho... alimradi tu nilikufa nikaoza mwisho tukaamua kuoana.. hadi leo tuna miaka 22 pamoja tuna mtoto 1 yuko university na tunapendana utadhani tumekutana jana! life is sooo sweeeet

Hongereni sana...
 
hahaaa ingawa bado sijaamua kufanya maamuzi ikiwemo Uchumba na ndoa, mara ya kwanza sikujua nini kinaendelea maana mara ya kwanza tulienda kama vijana(wavulana na wasichana) kama 27 hivi katika Shule moja hapa mjini Dar. ilikuwa ni tour tu kubadilishana mawazo na kuwatembelea wanafunzi, tuliingia katika moja ya madarasa na baadhi ya wanafunzi tukawa tunabadilishana mawazo, baada ya muda kidogo kama nusu saa tukaondoka lakini mwalimu aliyekua katukaribisha pale shuleni akasema tuandike majina na hata namba zetu za simu, tukafanya hivyo mimi nikaandika mpaka namba yangu ya simu na jina langu, tukaagana tukaondoka zetu,

baada ya muda kama miezi mitatu simu yangu ikaita sauti ya binti ikawa inazungumza baada ya kuipokea simu, na akajitambulisha yeye ni fulani kutoka Oysterbay kuna siku mwezi wa tisa tulienda kuwatembelea shuleni kwao, akaniambia mpaka jina lake, nikamuuliza kama ni namba yake ni ya simu aliyonipigia akasema ni ya dada wa kazi pale kwao akaniambia any time ninaweza kumpigia, kuanzia hapo tukawa tunawasiliana mara kwa mara, na nilimchukulia kama mdogo wangu tu, kuna siku akaniambia tukutane Ubungo kuna mizigo alikua ameenda kuisubiria kutoka Arusha, na nilikua na hamu ya kumuona kweli maana sauti yake na maneno yake ya unyenyekevu nilikua na hamu sana ya kumuona.

nilijiandaa fasta nikawahi ilikua ni jumamosi mchana saa nane nilipanda gari mpaka ubungo , nikampigia simu nilipofika pale nikaonana nae tukasalimiana tukapiga story kidogo kama dakika tano akaja kaka yake akanitambulisha kwa Kaka kua mimi ni rafiki yake hapo ilikua mwaka 2009, kaka yake alikuja na gari tukasubiri mpaka gari likaja tukapokea mizigo tukaondoka zetu tukaenda mpaka Blue Pearl Hotel tukanywa juice tukawa tunapiga story kidogo, kaka yake binti alikua ni mpole na mtaratibu sana asiye na makuu, baada ya kumaliza kunywa juice tukaondoka zetu. waliniacha mitaa ya home Africa Sana-Sinza wao wakaenda zao home kwao Oysterbay..
tuliendelea kuwasiliana kama kawaida na siku tuliyoonana usiku wake tuliongea kama masaa matatu, niliendelea kuwasiliana huyu binti kila wakati na kila muda alinitumia sms za kunijulia hali.....

kwa miaka miwili niliendelea kuwasiliana nae hatimaye tukajikuta tumeshapendana, ameanza chuo mwaka jana nikawa napata nafasi ya kwenda kumtembelea chuoni kwake na nilikua napata muda mrefu wa kukaa nae na alinitambulisha kwa marafiki wenzake nikawa nimejulikana kama Mr Somebody pale chuoni...

Season ya Christmass mwaka jana nilikaa nae muda mrefu kama siku 9 tulifanya tour Ruaha national park na mambo mengine mengi, tumendelea kua pamoja kwa kila hali japo tunakwaruzana lakini maisha yansonga na ananijali na kunipenda sana sana...

mwezi wa tano mwaka huu nilipata ajali mbaya na yeye akatoroka Chuo akaja kunitembelea mpaka Dar, na hapo Mama yangu alimjua huyu Binti na alikua anakaa pale Hospital muda mrefu maana mimi nilikua hata sielewi nini kinaendelea maana nilikaa siku 6 bila fahamu, binti aliendelea kukaa mpaka nilipozinduka alikuwepo alinikumbati na kunibusu shavuni kwangu mbele ya mama yangu nilitoka Hospital baada ya kupata fahamu siku hiyo na binti akarudi tena Chuoni..

wakuu nina mengi ya kuandika lakini, that is How i Met her

Natamani uendelee kutiririka... Huyo binti ukichelewa utapokonywa tonge mdomoni
 
Back
Top Bottom