Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulimtambua vipi kuwa huyu ndiye mwenyewe?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Rutashubanyuma, Jun 27, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  ULIMTAMBUA VIPI KUWA HUYU NDIYE MWENYEWE…..
  (Getting to know her/him)


  Hivi mwandani wako ulimtambuaje kuwa ndiye yeye?
  Hivi ni maujanja yepi wewe uliyatumia kumpima yeye?
  Ni vigezo vipi vilikutongoza hadi kujua umelamba dume?
  Hivi ni vichocheo vipi vilikufanya uone ya kuwa umewasili?
  Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


  Kauli yake mwenyewe huitia kitanzini na kuishibisha azma zake!
  Aongeacho mara nyingi sicho kilichopo moyoni kwake wala!
  Tabasamu lake lalenga kuijenga kauli ambayo si lazima iwe na kweli!
  Kamwe kauli au hata tabasamu lake kuwa kioo cha moyo wake!
  Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


  Kauli na taswira yake huoana na moyo wake masijala ya kukataa…
  Pindi moyo wake umekuasi kata katu basi shabaha wewe hulengwa…
  Bila haya au huruma jipu kukupasulia kuwa hakuhitaji nawe kulia..
  Na kwa kufanya hivyo huwa kajitendea mwenyewe ubinadamu..
  Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu


  Ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
  Hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
  Kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
  Kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja!
  Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Dah to me it is a long story !!Kwakuwa nilikuwa naye kama rafiki lakini nikakuta tumekuwa marafiki kwani siku yakwanza tulienda Casablanca ilikuwa kinondoni........then ndo ukawa mwanzowetu na sasa ni Mama watoto na ni family yenye furaha!!kwa kujivunia uwepo wa Baba na mama!!
   
 3. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #3
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Ni mitihani ipi uliitumia kuupima moyo wake?
  Hata kuridhia yeye ndiye na hakuna mwingineo?
  Kama ulienda mkichamkichwa basi ilikula kwako!
  Kama uliserereka na kauli au taswira basi wewe teja!
  Nifahamuvyo kauli na taswira zimejaa hadaa tupu

  Mimi nimeangukia kwenye utenzi wa mwisho.............lol
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  KakaKiiza..long story is yet to be told.......................ulimtambuaje? kwenda Casablanca pekee yake hakutoshi kamwe........kukufanya ukamtambua kuwa she is the one for you and forever and evermore for you safe kkeeping........there must be other reasons..............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Elizabeth Dominic ulitetereshwa na kauli na taswira tu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Lady JayDee hajaiona hii mistari aitolee single?
   
 7. m

  mamajack JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  duh,mie sijamtambua bado!!!!!
   
 8. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #8
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Taswira mwayego...........heri ingekuwa kauli
   
 9. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  huwezi amini alipenda vidole vyangu vya mkononi, aliniona napanda kwenye daladala ya mwenge posta akaona nimeshika mlango ili kupanda, akaadmire vidole kabla hajaona sura wala umbile langu! hakuwa anakuja posta alikuwa amemsindikiza rafikye kupanda daladala ilibidi apande! aliponiongelesha kunisalimia baada ya kushuka posta, i said what a sweet voice, a manish voice! the rest is history, kha umenikumbusha mbali!
   
 10. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  Nitarudi baadae!!
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Taswira bila ya kauli.........hii ni kali nifhamuvyo........................kauli njema humtoa nyoka pangoni.......................lakini wewe Elizabeth Dominic hata neno tu hukulihitaji...........hapo u were more than teja...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  KakaKiiza....................naona umepitwa na kiharusi na kigugumizi kikali sana............
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  cacico.......yeye vidole naye akakugwaya bila ya chenga ,.....................na wewe je what really happended....just a mnly voice?................there ought to be more...................a gentle aura......................that was least threatening to you made you feel safe in his ably hands? Or what was it that made you say I do...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Teja si kidogo, lakini nimejifunza.................suluba nilizozipata si kidogo, mpaka rafiki yangu moja uwa aliniambia ulimtaka mzuri kwani ulitaka kumpika umle...........lol
   
 15. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,273
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  Dah..bado sijampata mimi..
   
 16. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,239
  Trophy Points: 280
  I will be back shortly i have something doing here......then i will let you know all about!:ranger:
   
 17. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,273
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  kwahiyo ulienae sasa hv si mzuri Elizabeth.
   
 18. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,273
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  Dah kuna mtu/watu bwana wana vidole, akikuwekea vidole say amekushika mkono au begani raha sana....
   
 19. d

  decruca JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 295
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  real mi hata sielewei mwenzenu nimejikuta tu nimenasa mikonono mwake, maana sikumpenda day 1 baada ya kunifuatilia muda mrefu sijui ikawaje bac nikajiluta mbele ya paroko na sasa its about ten yrs na ninampenda balaaa. but for sure sijui ilikuwaje.
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Noted KakaKiiza with gratitude......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...