Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Wewe unadhani mimi namlaumu Mwalimu? Mimi kati ya watu ambao ni watetezi wakubwa wa Mwalimu lakini sikuleta hii mada ili kumhukumu Mwalimu.So???
Nyerere alijaribu kufanya alichofanya kwa kiasi chake, wewe unafanya nini?
Siamini katika kucheza 'mwathirika" (don't play victim)
Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Hazifanani kabisa wala na yale maduka ya RTC. Duka la kaya hupati kitu mpaka mjumbe wa nyumba kumi akutambue kama wewe ni makazi wake halafu unaingizwa kwenye Leja wewe na watu wanaokutegemea. Siku ya mgao inawezekana ikawa kila siku ya jumatatu ndiyo zamu yako kama haupo basi mgao wako unahifadhiwa au mgambo kwa kushirikiana na muuzaji wanauza kwa bei ya kuruka.NMC shops models?
Kisa kikubwa sana kinachokumbukwa wakati wa Duka la Kaya ni pale Mjumbe wa Nyumba Kumi alipozabwa kibao na kufa na kijana ambaye alikuwa anaahirishiwa "zamu" yake kila siku. Kisa hicho kilitokea maeneo ya Manzese kwa mfuga Mbwa!!Duka la kaya lilikuwa noma, nakumbuka la mwisho lilikuwa pale Sinza Matokeo.
Nimekunywa sana uji wa chumvi kulaleki, maana mgao wetu sisi ulikuwa kama kilo 2 za sugar hivi. Sometimes unakata.
Kuna siku mzee akarudi kazini na kiroba cha Sukari sijui alikifumania wapi wacha tufurahi.
Kuna watu wanatolea mfano wa kushindwa kwa sera za Mwalimu Nyerere kwa kuhusianisha na DUKA LA KAYA. Enzi hizo wengine tulikuwa tunakimbizana na magari ya "Ugawaji" kwenye kila duka wanalosimama, wakati mwingine tukiyakimbiza magari hayo umbali wa hadi kilomita tano au sita.
Ilikuwa ni kawaida kupita kwenye maduka na kukuta msururu mreefu wa mawe yaliyopangwa kama alama ili wenye mawe hayo wakija wapate nafasi ya mbele kwenye foleni. Nakumbuka kulazimishwa kununua unga wa muhogo wenye mchanga ili tuweze kupata sukari kilo mbili na nusu kwa mujibu wa Kadi yetu ya Duka la kaya iliyokuwa inayonyesha kwamba nyumba yetu ina wanakaya 5.
Enzi hizo mgambo waliokuwa wanalinda kwenye maduka ya Kaya (Consumer's Cooperative shop) walikuwa wanaabudiwa sana mitaani kwani wao kila ukija mgao na wao hawakosi kupewa, tofauti na watu wa kawaida ambao wao ni mpaka "zamu" yao ifike. Wauzaji wa maduka haya walikuwa hawajui kabisa kubembeleza wateja kwani wateja walikuwa hawana uchaguzi kutokana na kutakiwa kununua mahitaji yao kwenye maduka walikoandikishiwa kama Wateja.
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Mimi sizungumzii kitabu ndugu yangu. Nazungumzia hali halisi, mimi duka langu nalikumbuka mpaka leo ila bahati mbaya lilipokuwa wajanja wameuza eneo pamejengwa duka binafsi. Zilipokuja Rexona na Lifebouy watu tuliona kama tumefika mbinguni!! Dah. Mchele Kitumbo ulipapatikiwa na kina mama kama vile almasi iliyoanguka kutoka mbinguni, watu walikuwa wameshachoka kula mchele mdundiko!!Ndugu,
Wakati huo nilikuwa ndogo wa kutumwa dukani, umenikumbusha enzi hizo. Namkumkuka mwandishi wake mahiri Mh. Ndimara I. Tegambwage, nawakumbuka baadhi ya wahusika kama vile Bibianna. Nakumbuka mzee mmoja aliyelala usingizi chini ya mti mpaka akakosa huduma ya sukari, akawa nyonge na kumwambia mkewe mara baada ya kurudi nyumbani aweke chumvi kidogo kwenye uji wa mjukuu wake.
Asante sana kwa kutukumbusha, je naweza kukipata tena
Wewe ulikuwepo enzi za DUKA LA KAYA? Na ile hali ilikuwa ni halisi au ilisababishwa na uzembe wa Mwalimu kushindwa kuona kwamba kulikuwa na hatari ya njaa inatunyemelea?
Hazifanani kabisa wala na yale maduka ya RTC. Duka la kaya hupati kitu mpaka mjumbe wa nyumba kumi akutambue kama wewe ni makazi wake halafu unaingizwa kwenye Leja wewe na watu wanaokutegemea. Siku ya mgao inawezekana ikawa kila siku ya jumatatu ndiyo zamu yako kama haupo basi mgao wako unahifadhiwa au mgambo kwa kushirikiana na muuzaji wanauza kwa bei ya kuruka.
Mimi nilikuwepo enzi zile tukiishi Mbezi Juu, na maduka yanapatikana Kawe Ukwamani tu. Kwa kweli ilikuwa hali mbaya sana.
Lakini katu siwezi kuilaumu Serikali ya kipindi kile, kwani ile ilitokana na hali ya Hewa na uhaba wa Chakula. SErikali ilijitahidi hata kuanzisha Maduka ya Kaya, Mobile Shops (Malori ya NMC yalikuwa yanapita mitaani na kuuza chakula kama Duka)
Pia Serikali ilijitahidi hata kuagiza Unga wa Njano ili kuwanusuru wananchi wake. KWA KWELI SERIKALI ILIJITAHIDI.
Wakati ule Serikali tu ilikuwa inaruhusiwa kuuza Chakula kwa wananchi, tena nakumbuka hali ilikuwa na unafuu kwani hata chakula kilikuwa na RUZUKU ya serikali hivyo kuuzwa kwa bei ya chini sana.
Na tulikuwa hatuna Rasilimali nyingi kama tulivyo sasa huenda ingelikuwa kama sasa tunaposhuhudia rasilimali zikichimbwa basi maisha yangelikuwa mazuri zaidi na hata kuweza Serikali kuwalipa mishahara / posho wananchi wake wote. Na kula chakula bure na Waisraeli enzi hizo kule Jangwani walipokula MANA.
RIP Mwalimu J. K. Nyerere, RIP E. M. Sokoine, RIP......
MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!