Ulikuwa unafahamu hii?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
871
Kama ulikuwa hujui ndo nakujuza...

Ukiwa Dar es Salaam maduka ya mchele huwa yanajinadi kwa mbwembwe MCHELE SAFI KUTOKA MBEYA

Ukishafika Mbeya unakutana na maduka ya mchele yakijinadi
PATA MCHELE SAFI KUTOKA KYELA

Ukifika zako hapo mjini Kyela unakutana na maduka ya mchele nayo yakijinadi
TUNAUZA MCHELE SUPER KUTOKA IPINDA

Unakufahamu Ipinda wewe? Ukishafika unakwenda zako duka la mchele. Mwuzaji anakwambia
HUU NI MCHELE SUPER KABISA KUTOKA BONDE LA TENENDE

Halafu ikitokea ukazurura hadi Tenende wenyeji wanakwambia MCHELE SUPER NI ULE WA SHAMBA LA MZEE MWAKIPESILE.

Unashangaa? Kila kizuri kina kizuri zaidi yake.
 
Na ukifika kwa mzee mwakipesile unaambiwa Mchele mzuri super ni ule wa kutoka Shamba la mke wake mdogo, aisee
 
Back
Top Bottom