Kwanini Wanawake mnapenda kutujaribu kwenye mahusiano?

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
5,707
11,959
Habarini, natuma ujumbe huu nikiwa nje kujitafutia chakula sehemu nyingine.

Ipo hivi, unakuta mwanaume unawajibika kutafuta mahitaji ya ndani, unahakikisha vitu vimenunuliwa na kubalance lishe ili familia ipate chakula kizuri ndani na kusiwe na usumbufu.

Shida inaanza na ratiba ya upikaji chakula kuwa haieleweki. Mwanaume unaamka asubuhi ukitegemea mke wako atashughulika kukuandalia chai unaamka unaenda meza unakutana na vyombo vya chakula vya jana havijatolewa. Mwanamke hana habari amelala na wala hana wazo la kuamka kukuandalia chochote.

Unaona usilete nongwa, unaingia kwenye friji unachukua mkate kama upo unapakaa asali na siagi ya karanga, unachukua maziwa unapasha unakunywa, unachukua ndizi unaondoka zako utafune njiani wakati ukienda kwenye harakati za maisha.

Mchana unafika unasema ngoja niende home nikapate msosi so unawahi kabla ya luch hours yaani kuanzia majira ya saa sita mchana. Unafika unakuta ndio kwanza mwanamke anapambana na kile kiporo cha wali wa jana hakuna kilichopikwa anajiandaa kutoka kwenda kwenye utafutaji. Unafika anakushangaa kwamba umekuja ghafla kula.

Anachukua kiporo akuandalie na wewe ule hivi kweli tena anakuwekea na chai, mchana mimi unilishe kiporo na chai na hili jua la Dar kweli?!

Unaamua kuwa muungwana unamzuga utakula baadae basi unawahi sehemu. Unatoka zako unaondoka unakwenda tafuta mgahawa unaagiza chakula unakula unarejea kwenye harakati zako za utafutaji.

Unarejea nyumbani baadae sana majira ya saa moja jioni. Unafika hakuna kilichofanyika na mwanamke hajarejea unavuta muda na yeye ndipo anaingia akifika anasema ngoja apike fasta fasta mle chakula unamuuliza sasa mtakula nini muda huo anaanza kutaja fast foods. Sasa huko kote nilikopita si nimeacha fast foods si ningekula?!

Dah, unavumilia tu basi mle hicho hicho kitakachopikwa ili tu kusiwe na shida. Hii routine ya kero inajirudia mara kwa mara. Unaona isiwe shida. Unamwambia malkia kama vipi ngoja tu tupate msaidizi wa kazi akupunguzie majukumu.

Anakubali na unamleta house girl ambaye yupo vema sana. Anafika naamua kuketi nae chini na kuanza kumpatia utaratibu wa majukumu.

Dada wa kazi anafanya vema kazi anaamka asubuhi mapema sana by saa moja chai tayari ipo mezani. Chakula cha mchana kipo mezani saa sita. Chakula cha jioni saa moja kasoro tayari kimeshaiva tayari.

Ratiba ya chakula inakwenda vema, binti kabla hajapika anakupigia simu anakuuliza Kaka leo utapenda kula chakula gani, na nikirejea nakuta chakula nilichoambiwa. Ila mke alikuwa anapika anachojiskia ukija utakutana nacho, usipojiskia kula anaanza kuhoji unaumwa au umekula wapi au haujapenda mapishi yangu. Yaani kuna mambo ni kero aisee.

Sasa huyu dada anasimamia vema sana majukumu, mchele ukiisha nilishampa malekezo ukifika kilo tano anijulishe,mafuta yakibakia kidogo anaijulishe,sukari ikikaribia kuisha anijulishe na anafanya hiyo kazi vema kabisa aisee hadi kichwa changu sasa kinakuwa chepesi. Ni gesi tu ndio inamsumbua kujua ikikaribia kukata.

Umeme huwa pesa namuwekea kwenye simu sababu huwa kwa mwezi tunatumia wa 12,000 hadi wa 15,000 so huwa namwekea kama 50,000 kwajiri ya maji, umeme na vocha na hiyo hudumu nayo miezi miwili. Akinijulisha kuisha huwa ni hadi karibia na mwezi wa tatu mbele huko. So yupo vema kibajeti.

Matumizi ya vitu ndani yanakwenda vema sana hakuna upotevu stock za chakula zinadumu sana na hii imesaidia katika eneo la bajeti maana familia ni ndogo.

Sasa mke anaanza visa maana anaona kama majukumu yake house girl anayaingilia. Amekuwa mtu wa kumpa kazi za kumkatisha majukumu ya ndani mfano anaweza mtuma kupeleka vifurushi vya wateja wake sehemu ya mbali ambayo itamfanya house girl achelewe kufanya majukumu yake kama usafi na kupika. Sasa recently ilikuwa too much alimuagiza house girl aende nyumbani kwa rafiki yake aliyejifungua akamsaidie majukumu ya mtoto.

Uzuri binti alinitext na kunijulisha kuwa dada kampatia hayo maelekezo. Nikamwambia sawa msaidie kabla ya saa kumi na mbili muage mwambie kaka ameniulizia nyumbani dada yako akikuuliza mwambie anipigie. House girl akarejea mapema sana na kuendelea na majukumu. Dada yake anampigia na kumlaumu kwann ameondoka dada wa watu anateseka si alimuelekeza kumsaidia kwa muda atarudi kwann kaondoka tena. Akasema kaka alinambia nirudi na saa hii nipo nyumbani napika. Wakamaliza kuongea , nikaenda jikoni nikamwambia niachie mimi nitaongea nae.

Aliporejea nikamuweka chini nikamwambia kwamba huyu dada nimemleta kwaajiri ya hapa ndani ili asimamie majukumu ya hapa ndani sababu wewe yanakinzana na ratiba zako. Sasa sijui umeshauriana na nani kumpeleka kwa rafiki yako. Kama una mjali sana rafiki yako nakuruhusu nenda ukamsaidie ila naomba tuheshimu kazi ya dada hapa ndani sitapenda nisikie anafanya majukumu nje ya hapa ndani.

Alijaribu kujitetea pale kuwa rafiki yake kaagiza dada ndio anakuja kwahiyo atamsaidia kwa siku hizi chache nikasema basi mimi nimekataa naomba tusiendelee zaidi mwambie rafiki yako atafute hata mdogo au ndugu ampe sapoti then akija dada wa kazi watapokeana. Huyu ni wa hapa ndani sitaki kushare na mtu.

Alikwazika ila akakubaliana na maamuzi yangu. Namuona kama anataka kumuwekea chuki huyu binti ila nimemwambia dada kwa lolote atakalokwambia nijulishe kabla haujafanya chochote.

Wanawake mnavisa sana aiseee. Yaani mkiona utulivu basi mnatafuta sababu ya kukosana na mwenza na unakuta mtu anakaa na wewe vizuri tu ila basi tu ili mradi akutibue umbadilikie aanze kusema mwanaume ananinyanyasa.
 
Mwanangu ni kweli mkeo hasikii lakini haya uliyataka mapema tu yalipooanza kutokea maana ulikaa kimya na bila kumwambia lolote.

Binafsi hata ungekuwa Mimi mkeo kuniletea mfanyakazi ningemaindi maana naona ananiibia mume, nimeshindwa majukumu ya nyumbani.

Hapo ukae na mkeo muongee ajirekebishe lasivyo ndoa itatia doa kubwa ikiwezekana mtu mmoja katika familia yao aitwe ili akae sawa lasivyo uyo dada wa kazi atanyanyasika sana na hata kuondoka bila kumwambia

TAFUTA SULUHISHO ILI MKEO AACHE TABIA ZAKE MBAYA.
 
Habarini, natuma ujumbe huu nikiwa nje kujitafutia chakula sehemu nyingine.

Ipo hivi, unakuta mwanaume unawajibika kutafuta mahitaji ya ndani, unahakikisha vitu vimenunuliwa na kubalance lishe ili
Hahaha kuna wa dada wa kazi wana roho nzuri aseee. Duuh mpaka basi,,,

Na wengi wanajua majukumu yao ipasavyo

Huyo mtunze mkuu atakusaidia mengi, ilimradi tu mipaka iwepo tu

Lakini hizi ndoa hizi zinachekesha sana anyway asante kwa taarifa mkuu 😊😁😁😁🙂
 
Hahahahahaha sio kwa saa saba hii
Ndio maana uko bitter na Wanawake kumbe ndani panawaka moto

Pole mwaya, kiufupi umetawaliwa na mkeo huna kauli kwa lugha nyepesi ni kwisha habari yako

#Kaa Mguu pande, utawala wa Mwanamke unakuja Duniani#
 
Hahahahahaha sio kwa saa saba hii
Ndio maana uko bitter na Wanawake kumbe ndani panawaka moto

Pole mwaya, kiufupi umetawaliwa na mkeo huna kauli kwa lugha nyepesi ni kwisha habari yako

#Kaa Mguu pande, utawala wa Mwanamke unakuja Duniani#

Dr. Mariposa
Dr. Mariposa
Mwanangu, majibu yako yanakata, yanakereketa na kuumiza.
Hasa unapomalizia..
##utawala wa mwanamke...##

Leo sisemi sana😁😁
 
Huyo mwanamke atamchukia huyo binti kinoma, hapo fanya kumuelewesha mkeo friendly maana huyo binti akiondoka kumpata mwingine kama huyo ni bahati... alaf inaonekana mkeo anakutawala.. ilitakiwa siku ya kwanza hujakuta chai alitakiwa atoe maelezo ni kwa nini kwa maneno yasiyopungua 1000.
 
Dr. Mariposa
Dr. Mariposa
Mwanangu, majibu yako yanakata, yanakereketa na kuumiza.
Hasa unapomalizia..
##utawala wa mwanamke...##

Leo sisemi sana
Hahahahaha huyo namchokoza hua tunakutana kwenye angle fulani tunaparurana weee kisha kila mmoja anashika njia yake, ananiita feminist kumbe ndani na yeye ana feminist wake anamzungusha kama tiara

Speaking about majibu yangu itabidi nibadilike naona wengi wanalalamika ila mimi binafsi nayaona yako poa tu au ndio uchokozi wangu mwanangu
 
Mwanangu ni kweli mkeo hasikii lakini haya uliyataka mapema tu yalipooanza kutokea maana ulikaa kimya na bila kumwambia lolote...
Sasa hivi hii Dunia ya leo ni ya kumfundisha mwanamke ratiba ya kuandaa chakula, kuniandalia chakula ninachopenda kula.

Yaani nimpigie simu mke wangu kumuuliza atanipikia nini leo?!

Sasa hapo nina mwanamke au nipo na mtu anafanania na mwanamke ila kaja nimfundishe uanamke?

Swala la kupika mwanamke anapewa trainings kwao na sio kuja kujifunzia kwa mwanaume.

Mwanamke lazima afahamu kuwa anawajibika kumpikia mwanaume wake chakula tena kwa kuzingatia ratiba sio kwa kujiamulia yeye anataka kula nini au saa ngapi anatapika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom