Nakumbuka nikiwa kwenye pitapita zangu mjini Musoma siku Moja, nikaona Land Cruiser VX ilivyokuwa imembeba Mwalimu akitokea Butiama kuelekea airport. Alipanda ndege kuelekea Dar es Salaam ikiwa ndiyo safari yake ya kwenda kuelekea London Uingereza kwa ajili ya matibabu. Hapo nikiwa bado mwanafunzi shuleni. Na hatimaye Oktoba tukatangaziwa kuwa Mwalimu hayupo nasi tena. Siku wanamleta kutoka Dar, mji wa Musoma ulizizima, tulijana airport ya Musoma kushuhudia shujaa wa taifa akitua katika ardhi ya Mkoa wa asilia yake akiwa amelala. Vilio vilikuwa vingi mnoo siku hiyo. Waombolezaji walisafiri Kwa wingi kwenda kumzika shujaa. Nami sikukubali kubaki nyuma. Nilitua katika Kijiji Cha Ujamaa Butiama, nikawa miongoni mwa maelfu ya watu walioshuhudia kuagwa na hatimaye kuzikwa Kwa nguri huyo wa siasa za bara la Afrika.