Ulikuwa na miaka mingapi kipindi Nyerere anafariki?

Ulikuwa na miaka mingapi kipindi Nyerere anafariki?

I was 24, nakumbuka kuna vijana walisindikiza Geneza la Mwalimu toka Airport hadi Mikocheni mbio wakiimba...

Nyerere kafaaaaa....... mtuteseeee
Nyerere kafaaaaa.... mtuteseeee

Wamama mitaani walikuwa wakiangua na kuzirai wakishuhudia Geneza la Mwalimu likipita. Hiyo siku ilikuwa ni balaa kubwa.

Kwa kweli hao Vijana ambao sasa wapo 40 hadi 50 by age wanashuhudia Taifa lao likiuzwa kama nguo za mtumba mnadani.
Walijua watateswa na kweli 😅

Kwani Mzee alikuwa tofauti na hawa? Ukiacha suala la ufisadi.
 
Umri kapuni lakini nakumbuka sana sauti ya mtangazaji wa VOA, Elias Maghembe akitangaza juu ya hali ya kiafya ya Mwl JK Nyerere kila siku jioni hadi alipofariki ST Thomas Hospital/Clinic London.
 
Nakumbuka nikiwa kwenye pitapita zangu mjini Musoma siku Moja, nikaona Land Cruiser VX ilivyokuwa imembeba Mwalimu akitokea Butiama kuelekea airport. Alipanda ndege kuelekea Dar es Salaam ikiwa ndiyo safari yake ya kwenda kuelekea London Uingereza kwa ajili ya matibabu. Hapo nikiwa bado mwanafunzi shuleni. Na hatimaye Oktoba tukatangaziwa kuwa Mwalimu hayupo nasi tena. Siku wanamleta kutoka Dar, mji wa Musoma ulizizima, tulijana airport ya Musoma kushuhudia shujaa wa taifa akitua katika ardhi ya Mkoa wa asilia yake akiwa amelala. Vilio vilikuwa vingi mnoo siku hiyo. Waombolezaji walisafiri Kwa wingi kwenda kumzika shujaa. Nami sikukubali kubaki nyuma. Nilitua katika Kijiji Cha Ujamaa Butiama, nikawa miongoni mwa maelfu ya watu walioshuhudia kuagwa na hatimaye kuzikwa Kwa nguri huyo wa siasa za bara la Afrika.
Asnte kwa ukumbusho huu mzuri
 
Wazee wetu nyie Mungu azidi kuwaweka
 
Wengine tulianza kupungiza hizo vitu zaidi ya miakaa thelathini iliyopita,sasa kazi kwenu mnaoelekea tulipo viizee vyenu japo ni wabishi kutusikiliza na kutuelewa!
😀😀
 
😀😀
Wengine humu mtuite vibabu ama vibibi,mtakapo jaliwa kula angalao chumvi kiasi mtaanza kuelewa msiyoyaelewa leo.Na siri ni kuishi maisha halisi ya hali yako.
 
Back
Top Bottom