Ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani ulipokuwa mtoto?

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Wakuu,

Watoto na michezo ni kama samaki na maji, wengi tushazama kwenye michezo mpaka tukaja kufatwa na fimbo huko tulipokuwa. Wakati mwingine mzazi mpaka anapata wasiwasi labda mtoto kapotea, kumbe mtu kazama kwenye kombolela huko?

rede.jpg

Katika michezo yote niliyoweza kucheza rede nilikuwa fundi, yaani mpaka watu walikuwa hawataki nicheze maani nikiingia ni kufunga tu, na tukiwa wengi ni mwendo wa kuokoa wenzangu tu. Pia niikua nilikuwa fundi wa kucheza goroli, yaani nilikuwa na makopo yaliyojaa goroli zilizopuna watoto wengine๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

Wewe ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani utotoni?

photo_2023-06-06_10-55-06.jpg
photo_2023-06-06_10-54-41.jpg

photo_2023-06-06_10-54-15.jpg
photo_2023-06-06_10-55-46.jpg
 
Mpira ase alaf nilikua superstar wa timu nacheza namba 9 tu sitaki kukaba nasubiri wenzangu watafute mpira watengeneze assist nifunge, Sasa ole wako uanze kunisema kuwa nawategea kukaba , nikizira kucheza wana wanakutoa uwanjan maana umemkasirisha mchezaji wanae mtegemea

Shida ilikua nikirudi nyumbani nachezea fimbo nyingi sana kwa kosa la kuchelewa kurudi baadae nikaacha kabisa na hivyo ndo zinakufa ndoto za watoto wa kiafrika
 
Mpira ase alaf nilikua superstar wa timu nacheza namba 9 tu sitaki kukaba nasubiri wenzangu watafute mpira watengeneze assist nifunge, Sasa ole wako uanze kunisema kuwa nawategea kukaba , nikizira kucheza wana wanakutoa uwanjan maana umemkasirisha mchezaji wanae mtegemea

shida ilikua nikirudi nyumbani nachezea fimbo nyingi sana kwa kosa la kuchelewa kurudi baadae nikaacha kabisa na hivyo ndo zinakufa ndoto za watoto wa kiafrika
Kweli kabisa, badala ya kutafuta njia nzuri watoto wakafurahia michezo na kupata muda wa kufanya mambo wengine ni mwendo wa fimbo tu.... huenda ungekuwa Messi wetu๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€ ila Messi mvivu ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚ ๐Ÿ˜‚
 
Nilikuwa kichaa wa games

Need for speed 2
Mortal kombat 4
Gta
Thief demo
Delta force
Moto racer
Dave, Mario, Angelo

Sina hamu tena na magem sikuhizi,
 
Wakuu,

Watoto na michezo ni kama samaki na maji, wengi tushazama kwenye michezo mpaka tukaja kufatwa na fimbo huko tulipokuwa. Wakati mwingine mzazi mpaka anapata wasiwasi labda mtoto kapotea, kumbe mtu kazama kwenye kombolela huko?

Katika michezo yote niliyoweza kucheza rede nilikuwa fundi, yaani mpaka watu walikuwa hawataki nicheze maani nikiingia ni kufunga tu, na tukiwa wengi ni mwendo wa kuokoa wenzangu tu. Pia niikua nilikuwa fundi wa kucheza goroli, yaani nilikuwa na makopo yaliyojaa goroli zilizopuna watoto wengine๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚.

Wewe ulikuwa bingwa wa kucheza mchezo gani utotoni?

View attachment 2647601View attachment 2647603
View attachment 2647604View attachment 2647598
Michezo ya baba na mama,Mimi na rikiboy hao mitaa ya Tandale DSM miaka Ile ya late 1990s kwenda the early 2000s

Mimi na rikiboy tulikuwa mababa huku To yeye na Lovie Lady wakiwa wamama

"Usiku" tulikula sana show,ya kinguonguo na ya kinyama nyama
 
Back
Top Bottom