Ulianzaje kukaa gheto?

Wakuu mambo vipi,,Leo naomba tufanye kushare kila mtu jinsi alivyo chomoka Nyumbani kwao..Hii itatoa hamasa kwa wale waliokua nyumbani na kuogopa kuhama na kuanza kujitegemea.

Janga hili linawakumba wana vyuo wengi,unakuta mtu anamalza chuo akiwa labda ana 25 then anarud nyumbani ,mbaya zaid anasubir kazi..alaf kazi zenyew haijulkani utapata lini.

Hii inapelekea wana wengi kua na fear ya kuchomoka home...Kiukwel hali ya kukaa hom inakata sana..Mzee unakuta anachomoka anakuachia mikazi flani hivi howcome.

Ukija upande wa MMU ndio mambo yanakua sio mambo...mtoto anataka aje kukusalmia unaona soo kwasababu upo nyumbani..inakata sana hii

Tukija kwenye maisha ya kujituma tu..sometime unakosa hamasa ya kupambana kwasababu ugali wa bure,unalala bure,kila kitu bure..hii inakua ngumu kuwaza kwa mapana ili kuanza kukamilisha dream zako..

Pia inakata sana..pale wanao unakuta wapo na mageto yao..lakin wewe kwako ni tofauti.

Sasa naomba kila mmoja aseme alichomokaje home na kuanza kukomaa na maisha..Achilia changamoto zake kikubwa hapa ni kusepa kwa maza..

##Mimi binafsi geto nilianza kukaa soon nilivyoingia chuo,,,nakumbuka nilipata room ya elf 50 nikaanza nayo kibish,nikanunua bed ya 150, 5 kwa 6,nikatafuta feni tu ya elf 35..si unajua joto la dar..nikaingia k.koo nikavuta subwoofer ya elf 75 tu...geto bila mziki sio geto ni choo,kujichek mfukoni boom likawa lishakata...basi nikaendelea kuishi geto hadi namalza chuo geto likawa limesheheni tu...
sasa baada ya kumalza chuo. Ndio nikarudi hom..ujinga niliofanya ni kurud hom na baadhi ya vitu niliviuza...Kasheshe ndio ipo saiz..wakuu hom akili inalala,,vibe yote hakuna ,hapa ndio najichanga nichomoke tena nirud geto nianze kupambana..hop ndan ya huu mwaka nitakua nishasepa hom kwa mara nyingine.

Sasa share kitu basi nawewe..

#Nini lilikusukuma usepe home?
#Kitu gani kilikupa mzuka wa kuanza kukaa geto?
#Vipi ulianza kukaa geto ukiwa na kazi au kibishi tu?
#Maisha yalkuaje since day one?
#Je ulienjoy uamuzi wako wa kusepa home?
#ulianza kununa vitu gani vya msingi na kuanza kuishi geto
#Una lipi la kuwaambia wana walioko home hadi leo wakiogopa kukaa geto kisa hawana ajira bado?

Karibuni wakuu..

View attachment 878774
Baada ya kupata kazi mkoa mwengine
 
daa umefanya uzembe kama wangu,nikiwa shule nilikua nakaa na manzi tukanunua kila kitu kwa malengo baada ya shule tuanze maisha.

akiba tukiwa na m.1 na laki 6, uoga kitu cha ajabu sana nikaona ntafanya nini nikala kona kurudi home nikamuachia manzi kila kitu. alinililia sana nirudi ila ule uoga haukuwa wa nchi hii

now nimepanga ila najilaumu sana kumkimbia yule manzi kwa uoga wa maisha mji wa watu
 
Kufupisha story ni kwamba gari ile niliifanya uber kipindi hicho ndo uber imeanza hope nilizisha mapambano kwani nlikuwa nahakikisha nalaza laki kila siku ya mungu na wife wakati yupo na ujauzito mkubwa akaajiri mtu wa kusambaza vitu vyake kwa wateja huku na mimi nikisambaza vyangu kwa gari huku wakati mwengne nikimsambazia na yeye,mwisho wa siku nilifungua duka ambalo wife baada a kujifungua akawa ndo msimamizi na pia deni la mzee la 20k kila siku nililitimiza na mwisho wa siku gari ikawa yetu,nakumbuka siku ya harusi babamkwe akatupa kiwanja kwa ksema altupa mtihani wa kujinunulia wenyewe means ile hela tulokuwa tunampa kila siku aliitu za na kutununulia zawadi ya kiwanja huk nasi tukiwa na vingine vitatu hiyo ndo story yangu ya geto ambayo imenipa mke na nyumba ambayo naimalizia now,watoto wangu mapacha,pamoja na gari 3,maduka na biashara nyingine na kunifanya nisahau kuajiriwa japo nna degree yangu ya first class
mkuu utakuta unachepuka
 
daa umefanya uzembe kama wangu,nikiwa shule nilikua nakaa na manzi tukanunua kila kitu kwa malengo baada ya shule tuanze maisha.

akiba tukiwa na m.1 na laki 6, uoga kitu cha ajabu sana nikaona ntafanya nini nikala kona kurudi home nikamuachia manzi kila kitu. alinililia sana nirudi ila ule uoga haukuwa wa nchi hii

now nimepanga ila najilaumu sana kumkimbia yule manzi kwa uoga wa maisha mji wa watu
Daah kwel mkuu...ila ulitisha kurud kupambana upya.....manz kwaiyo akalisongesha mwenyew? Si ungerud tu mkuu
 
nikiwa mwaka wa kwanza chuo mzee alihamishwa kikazi akaenda botswana na bi mkubwa alihamishwa akahamishiwa kibaha pwani

kwa kuwa na kibaha pia tulikuwa na nyumba basi familia nzima ilihamia kibaha then mimi nikaachwa na nyumba ya downtown ikiwa haina vitu zaidi ya kitanda cha rum kwangu fridge tv pamoja na gari

nilipofika mwaka wa pili mzee alifanya maconection nikapata ajira so nikashift kutoka kusoma full time to night college

baada ya muda nyumba ilijaa vitu vyote vinavyotakiwa kuwa ndani ya nyumba ikiwa ni pamoja kitanda katika kila rum (4rums) nikifanya hivi sababu ya wazamiaji washkaji wakija au my young sis akija

washkaji walinichukia sana sababu ilikuwa ni marufuku kuja kugegedea mule ndani

and the rest is history
Hahah nice mkuu...ilikua kibingwa sana hiyo
 
Nakumbuka nmetoka kwenye pepa na mwenzngu nmempakia kwenye boda boda tunarudi zetu home babamkwe ananipigia simu jerry uko wapi nkamwambia,heb njoo swhemu flani wakati nashuka pale na mwanake anakitumbo namshusha huku namtania mzee alitoka chozi la furaha alivyokuwa anatuangalia,nikaonyeshwa gari aina ya ist,that time ndo ubber imeingia tz,akanambia hii ndo gari nliyowapa but kwa sharti la kuniletea kila siku elfu 20 then baada ya mwaka litakuwa lenu,basi nkachukua piki piki nikaifunga sehemu na kuiweka lock then nkachukue ndinga na wife mpka tumapokaa then baadae nkaifata piki piki mpka kule then nkaileta home.
Ume ni inspire sana mkuu, nimeamini maisha hayana formula kwani popote yanaanzia na siku zote safari moja huleta safari nyingine, na upendo wa shemeji yetu unaoekana dhahiri siyo wa kinafiki, kwani sidhani kama kuna msichana wa chuo ambaye ataacha mambo ya kula bata na kuamua kukomaa na msela mpaka kuhitimu.
 
Umetupa somo zuri sana mkuu
So kupitia mimi hope mtajifunza vijana wenzangu kuwa endapo utalitumia vizuri basi hakika maisha yak yatabadilika.pia la mwisho ni kumtafuta mwenza mwenye maono ila uiangukia kwa kwa hawa makahaba wa mjini utaishia kuhangaika mwisho wa siku unarudi nyumbani ukiwa na miaka 40,bila kufanya lolote
Jerrybanks
 
Ulivyokuwa unaanza kuelezea nilikuchukulia poa, but hadi sasa nadiriki kusema " you are an inspiration ".
 
Mh! hii ya leo balaa,,, kila MTU nilipomaliza chuo,, ooh! First year, watu tumetoka mbali... Kitendo cha kumaliza la saba ndo tiketi ya kuhama nyumbani. Nakumbuka kauli ya mzee huu ndo mlo wako wa mwisho cha ajabu sikumuelewa kilichonikuta asbuh nilijikuta natimuliwa ndani kama mbwa koko aliyekosea njia.nikijichek nimevaa kaptula na kaushi nikajichanganya kitaa.. okota skrepa sana!! nikajichanganya car wash zoote nikawa najulikan mwish wa siku nikaingia geleji. Ila geto letu ndo lilikua balaa watu 14 chin maboksi utajua pakula alafu kunuka kam beberu ilikua kawaida
 
Hahaha msoto kama wote mkuu

Back
Top Bottom