Ulianzaje kukaa gheto?

Duh story ndefu balaaaaaaa
 
Interesting,ukipata nafasi lete muendelezo mkuu
 
In Mafian cartel l saying "interesting" leta kisa icho Ndege Tai leta story na wewe mzee wa jicho la mbali
 
Acheni tu vitu vingine sio vya kuandika hapa.. ila nilihama siku ile ile .. usiku wa kwanza nililalia mapazia🤣🤣🤣🤣🤣.
 
Kuondoka Nyumbani kwanza ni swala moja la kujitambua, lakini linaitaji mamuzi magumu sana na sio swala la kujionea huruma au la kujiuliza sasa itakuwaje?

Napenda kuelezea jinsi ya mimi nilivyo ondoka nyumbani na kwenda mtaani na kuanza kupanga geto.

Nilimaliza chuo mwaka juzi nikiwa na umbri wa 25, baada ya graduation nilirudi nyumbani na kukaa mwezi mmoja tu na baada ya hapo nikawaga wazee na kuwambia mimi naenda mtaani kupangisha na kuanza maisha.

Mwanzo walianza kuweka ugumu na kusema subiri kwanza mpaka upate ajira, nikawaeleza kila siku mnasikia swala la ajira ni changamoto ya dunia nzima. Acheni niende nikaanze kupambana huku na kule huwenda itajulikana riziki yangu ilipo.

Uzuri nikiwa chuoni mwaka wa pili toka mwisho, nianza kujipanga kununua kitanda, godoro pamoja na zulia. Kwahiyo nilikuja navyo home.

Nilipanga chumba cha elfu 60 na hapo sikuwa na mziki wala meza wala kochi la kukaa. Huku kichwani na ujuzi tu wa graphics Designs nilio jifunza kipindi nikiwa chuoni kupitia YouTube.

Kwahiyo nikanza maisha hivyo hivyo na laptop yangu, nikaenda mji ambao sijulikani ila kuna mwanangu mmoja alikuwa ananifahamu so akanipa ramani ya kwanza ya kufundisha vijana wa twishen. Nikaifanya weee lakini haikuwa malengo nikacha

Nikarudi kwenye design mana hapo sasa nikanza kufamiana na watu na kupata deal moja na mbili.

Kwahiyo mpaka sasa niko mtaa na hivyo ndivyo niliondoka nyumbani.
 
Kuna mwanangu yupo above 25 ni mwanachuo ila anaishi kwao na msela wake flani hivi ni wa kishua na huyo msela wake anaishi na mama yake pekee yao coz huyo bi mkubwa alizaa kijana mmoja tu

Sasa kila akimuomba yule maza kuwa anaomba akapange bimkubwa anasema hapana asubiri kwanza amalize masomo ndio akaanze maisha yake ila pesa ambazo anataka akapange ni bora azitunze au awekeze ili siku akimaliza awe na pa kushika

Je,jamaa aendelee kusubiri au achague njia yake!??

Majibu tafadhali
 
Jerry Mouse muongo wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…