ULEMAVU WA kuipenda DAR ES SALAAM KWA WASOMI KIKWAZO CHA KUKOSA AJIRA

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,623
2,000
Naandika kwa masikitiko makubwa mpaka najisikia machozi yananilenga, vijana wetu kila mmoja anataka afanyie kazi Dar, Dodoma au Morogoro, au mwanza na hata Arusha.
Lakini leo hii nenda Mafia, Nenda Nkasi, Nenda Liwale, nenda Busokelo,nenda Mpanda, Nenda Kibondo, Nenda kishapu, nenda Halmashauri zooote za pembezoni kwa hakika kuna upungufu mkuuuuuubwa wa watumishi. kwa bahati mimi mwenyewe nimefika kwa baadhi ya halmshauri hizo na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Vijana wanapangiwa kazi wakifika huko wanaaga kwamba wanafuata mizigo wanaondoka moja kwa moja, then wanakuja humu jamvini kulalamika hawana kazi.....sijui niseme neno gani hapa, lkn inaumiza. unajua nini kinafanyika kutokana na kukosa wafanyakazi.

-wanaajili wafanyakazi vibarua kwa mkataba.
-wengi wao hawana sifa kabisa, lakini kutoka na kukaa kwenye nafasi hizo mda mrefu sasa hivi wameiva kwenye kada zao zaidi ya degreee holder wetu.
-wakikaaa zaidi ya miezi sita wanalamba ajira then wanajiendeleza wakiwa kazini na sasa wengine wameshakuwa hata wakuu wa idara wakilipwa fedha kubwa kubwa na wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

WASOMI WETU WAKO WAPI??????
-Wasomi wako Dar hasa hasa Msewe, Survey na Sinza wamepanga magetho tena wengi wao wanaishi kwa misaada au vibarua wakisaga lami asubuhi mpaka jioni kusaka kazi bandarini,tra,bot na ofisi zenye green pasture jijini Dar.

USHAURI WANGU KWA WATAFUTAJI KAZI WENYE NIA YA KUITUMIKIA NCHI YAO.
-Halmashauri zetu hasa za pembezoni zina upungufu mkuuuuubwa wa watumishi karibia kila idara, nenda huko kwa mguu wako na vyeti vyako uombe kufanya kazi ya kujitolea, au ufanye kazi kwa mkataba amini usiamini utafanikiwa. huko pembezoni kuna makampuni hayana watu wenye sifa wanachofanya wanachukua watu unskilled kabisaaaa wanawaendeleza kwa gharama kuuubwa wakati wasomi wapo wamejificha Dar...aiseeee.

Tuache kuandika barua pekeee tunapoomba kaz then unakaa eti unasubiri majibu....non non no no ,tuwe na mazoea ya kwenda sisi wenyewe face to face, ukiwa nadhifu, na vyeti vyako, omba kukutana na mkurugenzi wa Halmashauri husika mwambie kinaga ubaga kuwa unatafuta kazi ya kufanya aidha kwa kujitolea ama kwa mkataba. ikiwezekana kama kwenye hiyo wilaya una ndugu ama rafik tafuta mtu anayejulikana hapo mjini akusindikize kama referee wako ili mkurugenzi husika akuamini zaidi. Ukisha pata hiyo nafasi hata kama uliomba kujitolea mwisho wa siku utalipwa tuu na baada ya mda watakuombea ajira rasmi then utaingia kwenye payroll bila shida.

kupitia huu mlolongo niliotoa kuna watu hata leo wameajiriwa na hata kesho wataajiriwa na wataendelea kuajiriwa kwa kufuata huo utaratibu niliotoa kwa sababu nyinyi wasomi mko Dar mnasubiri majibu ya barua zenu mlizotuma posta.

wahitimu wetu pale msewe survey,mwenge,sinza na kwingneko tafuteni nauli mwende huko pembezoni mkalitumikie taifa linawategemea
 
MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,350
2,000
Tatizo la hii nchi ni kwamba kuna tofauti kubwa sana na sana kati ya dar es salaam na mikoa mingine,,

Hilo tatizo sio wasomi wa kitanzania tu hadi wazungu linawasumbua, nazani umesikia kuhusu wale wazungu wa gesi wanaofanya kazi mtwara lakini wanaishi dar es salaam kila siku asubuh wanapanda pipa na jioni wanarudi huku gharama kubwa ikiingia..

Ila tuacheni masikhara kuna wilaya zingine kuishi ni kazi sana hata kama unalipwa pesa ndefu.

Kwa madogo mnaosaka ajira maisha ni popote maana maisha ya dar bila ajira ni hatari
 
Old Venom

Member
May 2, 2013
40
0
Naandika kwa masikitiko makubwa mpaka najisikia machozi yananilenga, vijana wetu kila mmoja anataka afanyie kazi Dar, Dodoma au Morogoro, au mwanza na hata Arusha.
Lakini leo hii nenda Mafia, Nenda Nkasi, Nenda Liwale, nenda Busokelo,nenda Mpanda, Nenda Kibondo, Nenda kishapu, nenda Halmashauri zooote za pembezoni kwa hakika kuna upungufu mkuuuuuubwa wa watumishi. kwa bahati mimi mwenyewe nimefika kwa baadhi ya halmshauri hizo na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Vijana wanapangiwa kazi wakifika huko wanaaga kwamba wanafuata mizigo wanaondoka moja kwa moja, then wanakuja humu jamvini kulalamika hawana kazi.....sijui niseme neno gani hapa, lkn inaumiza. unajua nini kinafanyika kutokana na kukosa wafanyakazi.

-wanaajili wafanyakazi vibarua kwa mkataba.
-wengi wao hawana sifa kabisa, lakini kutoka na kukaa kwenye nafasi hizo mda mrefu sasa hivi wameiva kwenye kada zao zaidi ya degreee holder wetu.
-wakikaaa zaidi ya miezi sita wanalamba ajira then wanajiendeleza wakiwa kazini na sasa wengine wameshakuwa hata wakuu wa idara wakilipwa fedha kubwa kubwa na wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

WASOMI WETU WAKO WAPI??????
-Wasomi wako Dar hasa hasa Msewe, Survey na Sinza wamepanga magetho tena wengi wao wanaishi kwa misaada au vibarua wakisaga lami asubuhi mpaka jioni kusaka kazi bandarini,tra,bot na ofisi zenye green pasture jijini Dar.

USHAURI WANGU KWA WATAFUTAJI KAZI WENYE NIA YA KUITUMIKIA NCHI YAO.
-Halmashauri zetu hasa za pembezoni zina upungufu mkuuuuubwa wa watumishi karibia kila idara, nenda huko kwa mguu wako na vyeti vyako uombe kufanya kazi ya kujitolea, au ufanye kazi kwa mkataba amini usiamini utafanikiwa. huko pembezoni kuna makampuni hayana watu wenye sifa wanachofanya wanachukua watu unskilled kabisaaaa wanawaendeleza kwa gharama kuuubwa wakati wasomi wapo wamejificha Dar...aiseeee.

Tuache kuandika barua pekeee tunapoomba kaz then unakaa eti unasubiri majibu....non non no no ,tuwe na mazoea ya kwenda sisi wenyewe face to face, ukiwa nadhifu, na vyeti vyako, omba kukutana na mkurugenzi wa Halmashauri husika mwambie kinaga ubaga kuwa unatafuta kazi ya kufanya aidha kwa kujitolea ama kwa mkataba. ikiwezekana kama kwenye hiyo wilaya una ndugu ama rafik tafuta mtu anayejulikana hapo mjini akusindikize kama referee wako ili mkurugenzi husika akuamini zaidi. Ukisha pata hiyo nafasi hata kama uliomba kujitolea mwisho wa siku utalipwa tuu na baada ya mda watakuombea ajira rasmi then utaingia kwenye payroll bila shida.

kupitia huu mlolongo niliotoa kuna watu hata leo wameajiriwa na hata kesho wataajiriwa na wataendelea kuajiriwa kwa kufuata huo utaratibu niliotoa kwa sababu nyinyi wasomi mko Dar mnasubiri majibu ya barua zenu mlizotuma posta.

wahitimu wetu pale msewe survey,mwenge,sinza na kwingneko tafuteni nauli mwende huko pembezoni mkalitumikie taifa linawategemea

Well said Mkuu!!
 
iGodmanhustler

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
611
500
1st.wewe umepata kazi huko wilayani?huko unakokusema wewe ni branches tuu head office zote zipo dar.kila ofisi ukienda unaambiwa hatuajiri hapa sikuizi hadi makao makuu dar....hata wilayani na kwenyewe au halmashauri ya jiji sikuizi hadi kazi za tempo nakujitolea lazima zitoke harmashauri kuu kasoro udereva na office attendance.trust me i have been on this road mpaka nimeamua kuja dar!
 
Gambisgrey

Member
May 4, 2013
18
0
Mtoa hoja hajafanya utafiti, mimi nipo mikoani na nilishawahi kuhudhulia interview ilikuwa Halmashauri ya wilaya ya kilolo, yaani ni mbali sana kutoka iringa mjini usafiri wenyewe ni malori mtu unafika kwenye interview umejaa vumbi cha kushangaza nilivyofika nikaona mtu nyomi. Nikapata marafiki wengine wanatokea Dar, Arusha na Tabora. Maisha ya kuchagua Dar ilikuwa zamani kwa sasa watu wanafanya kazi popote ila baadae wengi wao wanaomba uhamisho wa kuja dar ili waweze kujiendeleza kielimu. Huku mikoani kazi hamna ukiuliza wanakuambia mpaka makao makuu (Dar). Halmashauri haziajiri, ajira zote karibia zinatoka psrs. Wasomi kukaa Dar sio kama wanapenda ila angalau uishi jikoni unaweza kushiba Harufu.
 
Benaire

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
1,957
1,500
Kwanza napingana na wewe....
Sio wasomi wako dar...watu wa SAUT wengi hupenda kufanya au kupata kazi mwanza....yaani wahitimu wanaobaki dar lengo lao kubwa ni kupata kazi na sio kupata kazi dar....ninao rafiki zangu walikuwa dar but kazi walipata na kupangiwa mikoani kama kigoma na mtwara...
Kitu kingine...inategemea na dhamira ya mtu kitaaluma labda anataka kuishi karibu na chuo ili ajiendeleze...
Ila huo utaratibu unaozungumzia sio utaratibu rasmi wa ajira za serikali....na unawapa mwanya wa kutoa au kupokea rushwa kwa mazingira hayo ulioainisha katika kutafuta ajira!
 
Nivea

JF-Expert Member
May 21, 2012
7,457
2,000
kama hawakuua vile viwanda huko tanga,sido na vingine vyingi sana hawa wasomi usinge waona hapa ,pia kama tungefanikiwa kupata viongozi wenye akili wakajenga vyuo vikuuna wizara nyingi kila mikoa na kuiondoa hapa DSM usingewaona jinsi DSM na PWANI ILIVYOJAA ------ ANAJENGA TENA BANDARI BAGAMOYO,NA CHUO KIKUU TENA BAGAMOYO UNATEGEMEA WATU WAENDE WAPI KAMA SIO HAPA MJINI ,VIWANDA VYOTE MIKOANI VIMEBAKI MAGOFU WATU WAENDE HUKO KUFANYA NINI MKUU,USIBAKI KULAUMU PIA FIKIRIA MBALI.TANZANIA IKI CENRALIZE KILA MKOA NA SHULE TOSHA NA VYUO VIKUU ANGALAU VIWILI MAJI NA BARABARA ,UMEME .HUTAWAONA WATU NA BARUA HUKU MJINI WATAJIAJIRI WENYEWE
HEBU SERIKALI IRUDISHE VILE VIWANDA KILA MKOA UONE KAMA KUNA MTU ATAJAZANA HAPA MJINI,
LL IN ALL KAMA WEWE SIO MZARAMO NA WEWE NI WALE WLE UTOFAUTI NI KUWA ULIWAHI AU UMEJIKUTA UMEZALIWA HAPA!!
 
KIMAROO

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
453
250
ukumbuke pia kwamba ajira nyingi zatokea dar coz ya serikali yote kuwepo hapa mjini
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,623
2,000
Mkuuu naendelea kusisitiza hiviiii, kwa mfumo nilioutoa hapo juuu hadi hii leo watu wameajiriwa, na kesho wataajiriwa na wataendela kuajiriwa. Usitake niweke hadi data humu ndani kwamba nini kinaendelea wapi. Ukweli ndio kama nilivyoeleza hapo, huko ulikokosa inategemea ulienda kuomba kazi na approach gani. Believe me mkuu ajira za mtindo huo ndio kila kitu kwa sasa kwa wale mahasla.

mf. wataalamu wa Kompyuta kuna Mkoa fulan unahitaj wataalamu 21 lakini mkoa mzima yupo mwarabu mmoja wa Mtaani ndie anatumika kama IT specialist, Kuna mKoa hauna Mtaalam wa maji, kuna Mkoa hauna mtaalam wa Majengo kuna mkoa hauna Mtaalam wa ardhi na huko kwenye social sciences ndo usiseme. Nenda kule mtwara kama hutakuta drama za kutosha. lkn huu niliotoa ni ushauri hulazimishwai kuamini wala kuufuata. nawasilisha mkuu
 
Simple lady

Member
Dec 6, 2012
28
0
Problem ukienda kuomba kazi huko unakosema unaambiwa ss hatuajiri,waajir wapo dar ndiko makao makuu mi npo Mbeya nmeomba kazi mpaka nmechoka sn km unaweza kunisaidia nikupe namba yangu plz
 
mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,455
2,000
Umesema MKUU; Taifa limesomesha kwa gharama....
wapi uzalendo.
wapi Utaifa.
Fadhila ya punda....'
Mkuu taifa lipi linasomesha wananchi wake kwa gharama siku hizi? Tanzania??????? Mkopo asilimia 5 au 10 na unaurudisha??? Taifa lilikuwa zamani. wakati wa mwinyi na mkapa. Ndio hali halisi ya tanzania penda usipende
 
life is Short

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
4,741
2,000
Mkuu taifa lipi linasomesha wananchi wake kwa gharama siku hizi? Tanzania??????? Mkopo asilimia 5 au 10 na unaurudisha??? Taifa lilikuwa zamani. wakati wa mwinyi na mkapa. Ndio hali halisi ya tanzania penda usipende
Nimekupata mkuu, nashukuru kunijuza si bora hiyo kuliko kukosa kabisa kama yaliyotukuta sie siku hizooooo!!
tuvumilie uhalisi wa nchi yetu!! kama ipo choice WHY not.
Jioni njema
 
option

JF-Expert Member
Jan 15, 2013
1,814
2,000
mleta uzi uko sahihi na tafiti yako sema umekosea kitu kimoja ambacho ni mda wa kupost huu uzi. uzi kama huu at least ungepost miaka minne iliyopita. sa hivi mambo yamebadirika huko mikoani walikuwa wanaitana wanafamilia office moja sa hivi wanakuambia makao makuu ndio mpango mzima.
 
vegas

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,043
2,000
Halmashauri haziajiri kama wanaajiri basi hatujui kwa mfumo gani, mi nimejitolea kazi hapa halmashauri ya sumbawanga sasa mwaka unaisha kila ajira zikitoka sipati naambiwa watu wanaletwa kutoka makao makuu, na hao wanaokuja kutoka makao makuu hawaji kwa mkupuo huwa wanakuja mmoja mmoja kwa vipindi tofauti. Ingawa idara nyingi zinauhaba wa wafanyakazi.
 
Mama Brian

JF-Expert Member
Feb 7, 2010
321
195
Naandika kwa masikitiko makubwa mpaka najisikia machozi yananilenga, vijana wetu kila mmoja anataka afanyie kazi Dar, Dodoma au Morogoro, au mwanza na hata Arusha.
Lakini leo hii nenda Mafia, Nenda Nkasi, Nenda Liwale, nenda Busokelo,nenda Mpanda, Nenda Kibondo, Nenda kishapu, nenda Halmashauri zooote za pembezoni kwa hakika kuna upungufu mkuuuuuubwa wa watumishi. kwa bahati mimi mwenyewe nimefika kwa baadhi ya halmshauri hizo na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Vijana wanapangiwa kazi wakifika huko wanaaga kwamba wanafuata mizigo wanaondoka moja kwa moja, then wanakuja humu jamvini kulalamika hawana kazi.....sijui niseme neno gani hapa, lkn inaumiza. unajua nini kinafanyika kutokana na kukosa wafanyakazi.

-wanaajili wafanyakazi vibarua kwa mkataba.
-wengi wao hawana sifa kabisa, lakini kutoka na kukaa kwenye nafasi hizo mda mrefu sasa hivi wameiva kwenye kada zao zaidi ya degreee holder wetu.
-wakikaaa zaidi ya miezi sita wanalamba ajira then wanajiendeleza wakiwa kazini na sasa wengine wameshakuwa hata wakuu wa idara wakilipwa fedha kubwa kubwa na wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

WASOMI WETU WAKO WAPI??????
-Wasomi wako Dar hasa hasa Msewe, Survey na Sinza wamepanga magetho tena wengi wao wanaishi kwa misaada au vibarua wakisaga lami asubuhi mpaka jioni kusaka kazi bandarini,tra,bot na ofisi zenye green pasture jijini Dar.

USHAURI WANGU KWA WATAFUTAJI KAZI WENYE NIA YA KUITUMIKIA NCHI YAO.
-Halmashauri zetu hasa za pembezoni zina upungufu mkuuuuubwa wa watumishi karibia kila idara, nenda huko kwa mguu wako na vyeti vyako uombe kufanya kazi ya kujitolea, au ufanye kazi kwa mkataba amini usiamini utafanikiwa. huko pembezoni kuna makampuni hayana watu wenye sifa wanachofanya wanachukua watu unskilled kabisaaaa wanawaendeleza kwa gharama kuuubwa wakati wasomi wapo wamejificha Dar...aiseeee.

Tuache kuandika barua pekeee tunapoomba kaz then unakaa eti unasubiri majibu....non non no no ,tuwe na mazoea ya kwenda sisi wenyewe face to face, ukiwa nadhifu, na vyeti vyako, omba kukutana na mkurugenzi wa Halmashauri husika mwambie kinaga ubaga kuwa unatafuta kazi ya kufanya aidha kwa kujitolea ama kwa mkataba. ikiwezekana kama kwenye hiyo wilaya una ndugu ama rafik tafuta mtu anayejulikana hapo mjini akusindikize kama referee wako ili mkurugenzi husika akuamini zaidi. Ukisha pata hiyo nafasi hata kama uliomba kujitolea mwisho wa siku utalipwa tuu na baada ya mda watakuombea ajira rasmi then utaingia kwenye payroll bila shida.

kupitia huu mlolongo niliotoa kuna watu hata leo wameajiriwa na hata kesho wataajiriwa na wataendelea kuajiriwa kwa kufuata huo utaratibu niliotoa kwa sababu nyinyi wasomi mko Dar mnasubiri majibu ya barua zenu mlizotuma posta.

wahitimu wetu pale msewe survey,mwenge,sinza na kwingneko tafuteni nauli mwende huko pembezoni mkalitumikie taifa linawategemea

Are you sure with what your talking, kwa jinsi hali ilivyombaya ya ajira watu wanalilia hata kupata ktk hayo maeneo hawapati kama hawajatangaziwa kwamba kuna upungufu watajipeleka wenyewe?
 
mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,623
2,000
Halmashauri haziajiri kama wanaajiri basi hatujui kwa mfumo gani, mi nimejitolea kazi hapa halmashauri ya sumbawanga sasa mwaka unaisha kila ajira zikitoka sipati naambiwa watu wanaletwa kutoka makao makuu, na hao wanaokuja kutoka makao makuu hawaji kwa mkupuo huwa wanakuja mmoja mmoja kwa vipindi tofauti. Ingawa idara nyingi zinauhaba wa wafanyakazi.

hicho unachofanya hapo kwenye red ndio nasisitiza vijana wafanye badala ya kupiga mihayo mitaa ya posta huko dsm. believe me kuna ofisi ya Halmashauri ina wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 40, na wafanyakazi wa mikataba zaidi ya 60.

ahsante kwenye bluuu, vijana wauza nyago na washangilia mipira ya nje bila kufanyakazi wamepata ujumbe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom