ULEMAVU WA kuipenda DAR ES SALAAM KWA WASOMI KIKWAZO CHA KUKOSA AJIRA

Mtoa mada hajahamia digital.
Ungekuwa umehama analojia usingeleta mada hii jamvini.
Nakupa mfano mdogo tu kwamba mwaka jana niliitwa kwenda interview Lindi, check umbali wa kutoka Dodoma hadi Lindi achia mbali nauli yake kwa mtu ambaye hana kazi.
Niliamua nisiende kwa sababu ya kukosa nauli lakini kuna rafiki yangu mmoja akaniongezea kidogo na kunisisitiza nenda maana watu wengi hawataenda kwa sababu ya umbali na mazingira ya huko. Nikapanda gari nikaenda, sikuwahi kufika huko-nifupishe tu kwamba nafasi zilikuwa 12 na tuliitwa watu 178 takriban watu 170 walihudhuria nikiwemo mimi.
Sasa mtoa mada sijui kama unaelewa kiu ya watu kupata kazi. Yawezekana unawadhihaki watafuta ajira.
 
tungepitia national service tusingekuwa na woga wakwenda huko maporini (wrong) vijijini kuanza maisha!
kuliko kusaga lami kuishia kudhalilika ni heri kwenda huko wilayani etc kuanza maisha kisha kama umegrow unaweza kurudi Dar! NI kweli Dar iko tofauti sana na mikoa mingine, lakin ikwa uzalendo wetu tungeweza kufanya mambo kadhaa kusaidia kuchangia maendeleo katika mikoa mingine kuliko kung'ang'ania Dar!
Na ajira sio lazima uajiriwe halmashauri! Tnauhitaji ubunifu, utulivu, ujasiri, uzalendo na uvumilivu sana!
 
Tatizo siyo wasomi bali mfumo wa nchi na mamlaka zake katika utoaji wa ajira, mimi naona mikoa na wilaya kama mapambo au njia ya kupitisha maagizo ya serikali kuu.Binafsi naichukia Dar but kutokana na influence inabidi sometimes, licha ya ukweli kwamba sina ndoto ya kuishi Dar na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 5. Tatizo la mfumo wetu ni kwamba, unaweza pata tatizo la stahiki za kikazi,utasumbuliwa sana mwisho watakwambia nenda hazina Dar. Ukiwa na matatizo na bima haswa inapoiva, ili usisumbuke sana nenda Dar.Ndo mfumo ulivyo, makao makuu Dodoma lakini ofisi zote za juu Dar.Hata ukita marupurupu au semina zenye malipo, fanya kazi Dar na ndo maana hata Rais huwa anaongea na wazee wa Dar.Napenda hali ya hewa na mazingira ya Mbeya,Iringa,Morogoro,Arusha na Mwanza lakini mara kadhaa najikuta nipo Dar lol!
 
Back
Top Bottom