Naandika kwa masikitiko makubwa mpaka najisikia machozi yananilenga, vijana wetu kila mmoja anataka afanyie kazi Dar, Dodoma au Morogoro, au mwanza na hata Arusha.
Lakini leo hii nenda Mafia, Nenda Nkasi, Nenda Liwale, nenda Busokelo,nenda Mpanda, Nenda Kibondo, Nenda kishapu, nenda Halmashauri zooote za pembezoni kwa hakika kuna upungufu mkuuuuuubwa wa watumishi. kwa bahati mimi mwenyewe nimefika kwa baadhi ya halmshauri hizo na kujionea hali ilivyo ya kutisha. Vijana wanapangiwa kazi wakifika huko wanaaga kwamba wanafuata mizigo wanaondoka moja kwa moja, then wanakuja humu jamvini kulalamika hawana kazi.....sijui niseme neno gani hapa, lkn inaumiza. unajua nini kinafanyika kutokana na kukosa wafanyakazi.
-wanaajili wafanyakazi vibarua kwa mkataba.
-wengi wao hawana sifa kabisa, lakini kutoka na kukaa kwenye nafasi hizo mda mrefu sasa hivi wameiva kwenye kada zao zaidi ya degreee holder wetu.
-wakikaaa zaidi ya miezi sita wanalamba ajira then wanajiendeleza wakiwa kazini na sasa wengine wameshakuwa hata wakuu wa idara wakilipwa fedha kubwa kubwa na wanafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
WASOMI WETU WAKO WAPI??????
-Wasomi wako Dar hasa hasa Msewe, Survey na Sinza wamepanga magetho tena wengi wao wanaishi kwa misaada au vibarua wakisaga lami asubuhi mpaka jioni kusaka kazi bandarini,tra,bot na ofisi zenye green pasture jijini Dar.
USHAURI WANGU KWA WATAFUTAJI KAZI WENYE NIA YA KUITUMIKIA NCHI YAO.
-Halmashauri zetu hasa za pembezoni zina upungufu mkuuuuubwa wa watumishi karibia kila idara, nenda huko kwa mguu wako na vyeti vyako uombe kufanya kazi ya kujitolea, au ufanye kazi kwa mkataba amini usiamini utafanikiwa. huko pembezoni kuna makampuni hayana watu wenye sifa wanachofanya wanachukua watu unskilled kabisaaaa wanawaendeleza kwa gharama kuuubwa wakati wasomi wapo wamejificha Dar...aiseeee.
Tuache kuandika barua pekeee tunapoomba kaz then unakaa eti unasubiri majibu....non non no no ,tuwe na mazoea ya kwenda sisi wenyewe face to face, ukiwa nadhifu, na vyeti vyako, omba kukutana na mkurugenzi wa Halmashauri husika mwambie kinaga ubaga kuwa unatafuta kazi ya kufanya aidha kwa kujitolea ama kwa mkataba. ikiwezekana kama kwenye hiyo wilaya una ndugu ama rafik tafuta mtu anayejulikana hapo mjini akusindikize kama referee wako ili mkurugenzi husika akuamini zaidi. Ukisha pata hiyo nafasi hata kama uliomba kujitolea mwisho wa siku utalipwa tuu na baada ya mda watakuombea ajira rasmi then utaingia kwenye payroll bila shida.
kupitia huu mlolongo niliotoa kuna watu hata leo wameajiriwa na hata kesho wataajiriwa na wataendelea kuajiriwa kwa kufuata huo utaratibu niliotoa kwa sababu nyinyi wasomi mko Dar mnasubiri majibu ya barua zenu mlizotuma posta.
wahitimu wetu pale msewe survey,mwenge,sinza na kwingneko tafuteni nauli mwende huko pembezoni mkalitumikie taifa linawategemea