Ulega Ambana Mkandarasi Barabara Kuelekea Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ)

Ulega Ambana Mkandarasi Barabara Kuelekea Makao Makuu ya Jeshi (JWTZ)

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,428

ULEGA AMBANA MKANDARASI BARABARA KUELEKEA MAKAO MAKUU YA JESHI (JWTZ).

Amtaka akabidhi barabara ifikapo Disemba mwaka huu

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amemtaka Mkandarasi Kampuni ya CHICO kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kikombo – Chololo - Mapinduzi (Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi-TPDF) yenye urefu wa kilometa 16.4 kwa kiwango cha lami ifikapo mwezi Disemba, 2025.

Ulega ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma Juni 01, 2025 akiwa ameongozana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax na kukagua barabara hiyo ambayo utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua kwa sababu ya upungufu wa wafanyakazi na mitambo ya ujenzi.

“Tumekagua barabara hii, Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wake sasa nitoe maelekezo mahususi kwa barabara hii, Mkandarasi afanye kazi usiku na mchana, aongeze vifaa na mitambo ya ujenzi lakini pia azalishe ajira kwa wakazi wa maeneo haya ili barabara hii ikamilike kwa viwango na muda tuliompa kimkataba”, amesisitiza Ulega.

Waziri Ulega amemuagiza Mkandarasi CHICO kuhakikisha anaboresha mpango kazi wake ili aweze kukamilisha kazi zilizobakia zikiwemo ujenzi wa makalvati pamoja na madaraja katika barabara hiyo.

Aidha, Waziri Ulega amebainisha kuwa Serikali hivi sasa ipo katika hatua za mwisho za manunuzi za kumpata Mkandarasi wa kujenga barabara ya njia nne na sita kuanzia Chamwino Ikulu hadi katikati ya jiji la Dodoma.

Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax ameeleza kuwa ni matumaini yake ujenzi wa barabara hiyo utakamilika kwa muda uliopangwa na ikiwa na ubora na viwango vinavyotakiwa.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj. Jabir Shekimweri amewashukuru Mawaziri hao kwa kufika na kukagua hatua za barabara hiyo kwani lengo la barabara hiyo ni kuleta muunganiko na ukaribu kati ya Wilaya za Dodoma Mjini na Chamwino hivyo utachochea maendeleo katika maeneo husika.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa miradi kutoka TANROADS, Mhandisi Japherson Nnko amewahakikishia Mawaziri hao kuusimamia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo ili ikamilike kwa muda uliopangwa ambapo hadi sasa umefikia asilimia 51.
 

Attachments

  • ULEGA AMBANA CHICO KUKAMILISHA BARABARA YA KIKOMBO.MP4
    80.9 MB
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.31.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.31.jpeg
    774.6 KB · Views: 20
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.32.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.32.jpeg
    701.4 KB · Views: 17
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.32 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.32 (1).jpeg
    805.4 KB · Views: 16
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.33.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.33.jpeg
    716.5 KB · Views: 16
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.34.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.34.jpeg
    785.7 KB · Views: 18
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.35.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.35.jpeg
    574.9 KB · Views: 15
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.36.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.36.jpeg
    845.4 KB · Views: 21
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.36 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.36 (1).jpeg
    817.4 KB · Views: 14
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.37.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.37.jpeg
    568.6 KB · Views: 22
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.38.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.38.jpeg
    509 KB · Views: 15
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.39.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.39.jpeg
    593 KB · Views: 15
  • WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.40.jpeg
    WhatsApp Image 2025-06-01 at 20.51.40.jpeg
    540.8 KB · Views: 20
Chura a.k.a Dalali MKUU n wateule wake woote wamekosa uzalendo kwa TAIFA l Tanganyika. Aiwezekani road NYINGI MNO haziki ktk kiwango kabisa n wao wapowapo tu.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Kitakachomrudisha bungeni labda viti maalum,hawamtaki hata kunsikia watu wa Mkuranga. Anyway bara bara ya Kongoe Kisemvule kijijini kwao vipi? Magari yanarudi nyuma na kuuwa watu.
CCM hakuna mtu anayejitambua
 
Back
Top Bottom