Ule Ujumbe Uliookotwa Baada Padri Mushi Kuawa

Ule Ujumbe Uliookotwa Baada Padri Mushi Kuawa

ujumbe uliusoma wewe, tena unauliza mwenye nao.

kwani wewe ulisoma mstari mmoja tu.?
Tatizo lake yeye ni Bubu arafu msema hovyo. Kwahiyo ni vyema kumdharau.
 
Asungwilemwaifunga salaam.

Ninyi Wanyakyusa ndiyo maana mnang'olewa meno, kucha na macho. Mna ujasili mkubwa wa kueleza ukweli.

Huo ndiyo ukweli wenyewe wa matukio haya. Hususani tukio la Arusha. My dear serikali hiyo siyo njia sahihi ya kubaki madarakani. Aliyiyasema Asungwilemwaifunga ndiyo ukweli wenyewe.
 
jamaniEee tusimimine petroli kwenye moto:-

Kwa Heshima na Taadhima kwa wanaJF & Walimwengu;
Natoa Taazia kwa wa Tanzania, Msiba huu umetufundisha mengi. Mheshimwa ulilosema ni la maana kwa jamii yote pamoja na serikali yetu kutafakari. tuungane mikono kwa pamoja Tufungue nyoyo (inner heart ) zetu kwa pamoja
Na TUOMBE kwa MWENYEZZI MUNGU MMOJA atusaidie na atuondolee janga hili. Amin/Amen kweli hatuwezi kupata suluhisho au muarobaini wa kutatua masaibu (mushkeli) huu kwa kuchambua au kuchakachua ya fulani au ya shetani.
Hatuwezi kujustify kwa gharama au mgongo wa DINI yangu au ya mwenzangu Dini ni ya MUNGU mwenyewe sisi ni waumini tu, Siye wote niwatendaji wa imani zetu zilizo jaa. kifupi wandugu serikali lazima ifahamu hili. " Desperation " hufanya watu kutenda mambo yasiyo kubalika kijamii " Ni jumkumu la Raia wote kuwa na ushirikiano na kukubaliana kwa busara na hekima kama Taifa lilivyojengwa kama ngome moja.
jamani uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Hivi ni kwa nini watanzania ni waoga wa kudadisi mambo kwa kigezo cha umoja wa kitaifa? Mtakimbia ukweli mpaka lini? Umoja umejaa uvundo, huku kila anayejaribu kusadisi chanzo anaambiwa aseme ni pafyumu tu. Hekima hizi ni za muda tu, matokeo yake ni mabaya zaidi kuliko kuuchambua ukweli hivi sasa.
 
Ni mawazo yangu sio yako. Nikisoma orodha ya watuhumiwa wa tukio la ugaidi la Arusha la tarehe 4/5/2013 ikiwa na majina ya wakristu siamini kama ni majina ya kweli. Kwa nini siamini? Nitaeleza.
Mosi serikali mara nyingi imedhihirika kuwa haisemi ukweli mpaka ibanwe ndipo huumbuka. Mifano iko mingi. Mheshimiwa John Mnyika alipopeleka hoja ya tatizo la maji, Serkali iliibuka na kusema imekwisha tenga fedha za kutatua tatizo analolisemea Mheshimiwa Mnyika. Wabunge walidai Waziri mwenye dhamana onyeshe zipo kwenye Landama gani. Serikali haikuwa na jibu- maana yake ni uongo.
Katika sakata la kutekwa, kupigwa, kuteswa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande kwa Mwenyekiti wa jumuia ya Madaktari Dr. Ulimboka serikali ilimkamata mwehu na kumwonyesha kama ndiye mtuhumiwa wa tukio hilo baya sana. Huu pia ulikuwa ni uongo, kwani Dr. Ulimboka alithibitisha kuwa siye.
Tatu yapo malalamiko kuwa Serikali kupitia usalama wa Taifa(TISS) wamejifunza ugaidi kwa kuwateka, kuwapiga na kuwatesa wale wote wanaoonekana kuipinga serikali. Hata hiyo serikali haijaukubali ukweli huo badala yake inasema vitendo hivi vimekuwa vikifanywa na majambazi. Huu pia ni uongo na kuwabambikizia kesi majambazi. Tabia hii ya kubambikia wengine wasiohusika kutenda mabaya hutendwa na binadamu wanaoishi katika jamii ya watanzania, serikali inadhani ni jambo la siri. Ni kujidanganya sawa na Mbuni anayeficha kichwa mchangani akidhani hataonekana.
Sasa hivi kuna mjadala mkali wa kuchipua kwa udini na ikitajwa wazi kuwa mwaasisi wa udini ni Jakaya Mrisho Kikwete ( sijataja Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa kuwagawa Watanzania sio jukumu analotegemewa kulifanya Rais wa nchi) Kwa kuwa JK ni mwanzilishi wa makundi hata ndani ya chama chake mwenyewe: CCM ni vigumu kujinasua katika kupendelea kundi mojawapo kati ya makundi ya dini Uislam au Ukristo. Ukimsikiliza hotuba zake za udini unabaini pasipo shaka kuwa anaegemea zaidi Uislam. Kwa kuwa matukio mengi ya Kuchoma makanisa kuua viongozi wa dini ya Kikristo kama vile Padri Abrose, Mushi na Mchungaji wa kule Geita upo uwezekano wa kutengeneza tukio la Arusha kutumia majina ya watuhumiwa ya kikristo ili tuamini kuwa jambo hili halihusiani na udini. Huu ni mwendelezo wa mbinu chafu za viongozi wasiokuwa na chembe ya UADILIFU. Ndiyo maana Mhashamu Askofu Porlicalip Pengo wa jimbo kuu Katoliki Dar es Salaam anasema "tusiposema ukweli hatutaweza kuondoa tatizo la udini" Bila shaka anauona unafiki ulio wazi unaosemwa na Jakaya Mrisho Kikwete. Kama anasikia anapaswa kuona aibu kuwa amegundulika na jamii ya watanzania AKIWEMO YEYE MWENYEWE kwa kuwa hawezi kujidanganya yeye mwenyewe kwa jambo analijuwa kwa hakika kuwa anapotosha. Njia ya mwongo kwa kawaida ni fupi. Alianzisha mtandao ndani ya CCM akashindwa kuuvunja akaanzisha tena hoja ya Udini nao pia anashindwa kuuvunja badala yake anatumia mbinu hafifu ya kucheza na imani ya watu. Unaweza kuning'oa kucha, meno na chochote ukitaka, lakini huwezi kuung'oa meno au kucha ukweli. Daima utabaki na daima utakusuta hata ukiwa peke yako gizani.
Naunga mkono hoja
 
Bahati nzur ukristu si kupeana tu majina,siku ya ubatizo unapewa cheti kitachokutambulisha wewe au mimi kama mkristu.
Ambrosi anaweza kuwa mkristu kwa jina lakin he is not a christian.
Kuna jambo me linatitaza kidogo,kwa nini hili swala linajadiliwa kwa misingi ya vyama?je pale kanisani kulikuwa na wafuasi wa chama kimoja?
 
Hivi ni kwa nini watanzania ni waoga wa kudadisi mambo kwa kigezo cha umoja wa kitaifa? Mtakimbia ukweli mpaka lini? Umoja umejaa uvundo, huku kila anayejaribu kusadisi chanzo anaambiwa aseme ni pafyumu tu. Hekima hizi ni za muda tu, matokeo yake ni mabaya zaidi kuliko kuuchambua ukweli hivi sasa.

Nakuja kwawema na kuingia jamvini kwa kuheshimu rai za wenzangu, Nafahamu kuwa unasonga maudhui wa kuikabili
Serikali yetu kwa presha,Lazima uelwe mipasuko ipo kila sehemu hapa Duniani na kuna mifarakano katika kila jamii na hata kifamiliya zipo tafauti..... Sasa Umoja wetu nchini ni LAZIMA tuuNUSURU kwanza na njia ya kunusuru ni kuutafakari kwa busara na kujadiliana kiutu uzima na kukubali kuCOMPROMISE mambo mwanzo mwanzo, ili tuweze kuwa na uwazi wa mapatano muwafaka ya uhakika na ukweli. Hapo tutaweza kukwepa DAMAGE, hatari, Madhara yanayo jichipua katika
vita au mapambano ya sisi kwa sisi Wakuu wenzangu tusisahau hisia zote hizi ni IMANI !! na imani kitu kizito sana na hakina macho wala rangi hata halina thamani ya kuwa DAMU ni NZITO kuliko maji.!!
Mie nakubali nawe kuwa tusikiimbie TATIZO hili, kwa hiyo tuendelee kuungana na tuelekeze msafara wetu hadi huko SERIKALINI wote kwa nguvu moja... Watakao bainika ni wanafiki au vibaraka wa njama hizi basi washitakiwe kisheria.
Idara za mahakama zina mitandao yao hadi huko majuu kwa hiyo yote yanaonekana.
Tafadhali wandugu tusikate tamaa bado hatujachelewa.
Mungu atunusuru.
 
Back
Top Bottom