Mim mwehu ndama kijana wa kitanzania niliwah kuandika uzi kuomba msaada kuhusu jinsi yakupata visa yakuingia nchini Sweden, na nashukuru Kwa maoni ya baadhi ya wadau nilifanikiwa kufuata ushauri nakufanikiwa kutia maguu ndani ya bara la uropa.
Lakini tangu nilipotoka bongo nakufika hapa ughaibuni huku kichwani nikiwa na lengo la kujilipua nakubaki huku moja Kwa moja maisha yamekua tofauti na nilivyo fikiria..
Ukizingatia mwenyeji wangu nayeye anaishi hapa kiujanja ujanja.
Niliomba visa ya wiki 3 na bahati nzuri baada yakufika hapa na nlipokaribia KUMALIZA muda wangu waliniongeza miezi mingine 3.
Lakini sasa sioni kinachobadilika katika maisha yangu zaidi yakupata huduma nzuri ya chakula nakuvuta hewa Safi hapa Uppsala .
Kiukweli maisha ya hapa yanazidi kuwa magumu Kwa upande wangu sababu nimejaribu kuanzisha mahusiano na mabinti, wanawake watu wazima Hadi vikongwe ili kusudi atakae jaa nioe ili niweze kupata makaratasi lakini nawao wamekuwa wagumu.
Sitaki kujivika status za kikimbizi maana nahisi ntaaribu kabisa mpangilio wote wa maisha yangu nakuitendea ubaya elimu yangu niliyoipata Kwa shida bongo land.
Nimekua mzururaji na cha ajabu hata zile KAZI za kubeba box nilizokua nazisikia zikisemwa Sana na wadau humu jf sizipati.
Kwa kifupi uchumi wangu umedidimia mara 100 zaidi ya hata nilivyokua bongo , mpaka najuta Kwa nini nilitumia pesa yangu nlioichanga Kwa shida kama nauli yakuja huku uzunguni pasipo na manufaa ya kiuchumi kwangu.
Hapa navyoongea nimeshawasilisha ombi la msaada wa nauli ya kurudi nyumbani katika kanisa naloSali hapa Uppsala.
Kwa kifupi narudi nyumbani na nikifika hapo Kwa mkuu jiwe naenda moja Kwa moja kijijini kwetu namanditi songea kulima.
Bye bye wabongo mliopo Sweden mim maisha yamenishinda narudi nyumbani.
View attachment 1389715View attachment 1389716
Sent using
Jamii Forums mobile app