Ulaji wa Nguruwe wapigwa Marufuku

Ulaji wa Nguruwe wapigwa Marufuku

Thread zingine bwana!!! sasa ona huu uzi matokeo yake nimeharibu bajeti yangu ya kula chakula cha mchana, nimeisoma, nimeona picha za baadhi ya wachangiaji nimepata hamu, nimepiga simu kwa Mangi nitengenezewe nusu, saa saba nakwenda kula!!!🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
 
Tuheshimu funga ya wenzetu. Na huo ndio ucha Mungu.
 
73748494ba5b4abe2fa343e9fd9f3ee5.jpg
Mdudu[emoji39] [emoji39] [emoji39]
 
Watafute tu hiyo tiba soon ila kuacha kabisa kula mdudu ni mtihani mkubwa huo
 
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme, amepiga marufuku uingizaji na uchinjaji wa nguruwe, kufuatia mlipuko wa homa ya nguruwe.

Alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na madiwani na watendaji wa Manispaa ya Dodoma.

Alisema hadi sasa zaidi ya nguruwe 200 tayari wameshakufa kutokana na mlipuko huo.

Aliwataka wakazi wa manispaa hiyo kutokula mizoga ya nguruwe ili kuepuka maambukizi ya homa ya nguruwe ambayo kwa asilimia 100 inaua.

Aliwataka kula nyama ya nguruwe iliyopimwa na wataalamu wa afya.

Alisisitiza madiwani kutoa elimu kwa usahihi kwa wananchi wao kuhusu madhara ya mlipuko huo.

Alitaja kata zilizokumbwa na mlipuko huo kuwa ni kata ya Ipagala na Miyuji ambayo zaidi ya nguruwe 200 wameshakufa.

Aliagiza kufanyika doria na kuwakamata watu wote watakaobainika kukaidi amri hiyo.

“Ninawaagiza nyinyi madiwani pamoja na watendaji hakikisheni mnatoa elimu iliyo sahihi kwa uwazi bila kificho, ukizingatia kuwa ugonjwa huu unaua tena kwa asilimia mia moja, hivyo ni marufuku kuingiza ndani ya wilaya hii na wala kuchinja pasiporuhusiwa na wataalamu wa afya,” alisema.

Alisema ingawa ufugaji wa nguruwe ni sehemu ya kujiingizia kipato, kipindi hiki cha mlipuko hakuna sababu ya kupuuza bali wanatakiwa kujiepusha ulaji holela wa nyama hiyo.

Aliwataka wafugaji kujiepusha na uchukuaji wa vyakula vinavyobaki hotelini na sokoni kwa kuwa vinasadikiwa kuwa na vimelea vinavyochangia uwepo kwa homa hiyo.
[emoji56]
 
mmmmmmmmmmmmhhh! jamani nimeumia nilivyosoma hiyo comment yako, huyu dada Christina (DC) kaolewa na binamu yangu kabisa!!! yeye ni Mnyamwezi, jina la Mndeme ni la Mr wake.
Mkuu hivi ndivyo wanavyoumia ndugu wa wengi tunaowatupia matusi na kuwazushia kashifa za uongo. Mfano huyo kiongozi wasiompenda wanaoisoma namba. Na hivi ndivyo wanavyo umia wahanga wa Mange Kimambi. Vuta picha yule mama Rita M alivyotupiwa matusi na tuhuma za kweli na uongo watoto wake ndugu na jamaa wameumua kiasi gani? Jiulize Mama Jessy au Mke wa RC wa mjini wanavyoumizwa na matusi na kashifa za humu jukwaani. Usimtendee mtu usichopenda kutendewa. Ni rahisi tu kutukana mtu mtandaoni lakini athari yake kwa mlengwa ni kubwa mno beyond imagination.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom