Muongozo wa ufugaji wa nguruwe.

Muongozo wa ufugaji wa nguruwe.

Chakula Kibaya

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2022
Posts
792
Reaction score
1,733
Habari ya Leo wakubwa,bila shaka mnaendelea salama na majukumu yenu.
Nina mpango wa kuanzisha mradi wa kufuga nguruwe kibiashara na Nina eneo la hekari moja.
Ninaomba kujuzwa mambo yafuatayo;
1.Mbegu nzuri ya nguruwe hasa kwaajili ya kuzaa na nyama.
2.Bei ya kununulia nguruwe wadogo huanzia bei ipi Hadi ipi?
3.Kwa kuanza na nguruwe 15 natakiwa kuwa na kianzio Cha mtaji wa shilingi ngapi Hadi kuja kuanza kuwauza?
4.Changamoto ya ufugaji nguruwe.
5. Tahadhali ninazotakiwa kuwa nazo kabla na wakati wa kuanza ufugaji.
Asanteni
 
Kila la kheli katika biashara yako ya laana
 
Upo mkoa gani
 
Mkuu hongera,shida kuu ya hili la ufugaji wa nguruwe kwa sasa ni ile homa ya nguruwe ambayo kwa kipindi cha mvua huenea kwa kasi sana.
 
Mtafute malafyale ni member humu jf,huyu ameandika kitabu kinaitwa ufugaji wa nguruwe wenye tija kitakusaidia
 
Ningependa kujifunza na kufahamu majibu ya maswali yako, Changamoto ni kwamba ni Vigumu kupata wachangiaji wa kutosha kwenye mada nyingi katika Jukwaa la Kilimo, Ufugaji, Uvuvi & Biashara.

Siamini kuwa hakuna members ambao ni Wafugaji, Wakulima, Wafanyabiashara n.k, Najua wapo wengi sana wenye majibu ila changamoto sijui ni Kitu gani!

Vijana wanajiajiri vipi ikiwa upatikanaji wa taarifa & maarifa kutoka kwa wazoefu wa shughuli hizo ni changamoto?
 
Kila la heri katika biashara yako mkuu 🙏🏿

IMG-20250319-WA0032.jpg
 
Mbegu nzuri za nguruwe ni Duroc,Large white,Landrace,na Pietrain Pia mbegu nzuri kwa nyama ni cross ya Duroc na Large white.Ufugaji wa nguruwe wenye tija kitu cha msingi ni mbegu bora na chakula bora chenye virutubisho nazungumzia matumizi ya Concetrate.Bei za piglets kwa mbegu nzuri za kisasa huanzia 300,000 kwa weaned piglets.Changamoto kubwa ya ufugaji wa nguruwe ni usimamizi tu,magonjwa mengi yanatibika na kuzuilika,pia kuepuka muingiliano na watu wengi ni nzuri kwa ustawi wa project.
Mwisho;ukihitaji meneja/msimamizi mzoefu wa project ya nguruwe tuwasiliane.
 
Back
Top Bottom