Uchaguzi 2020 Ukweli wenye ukali: Dkt. Magufuli lazima abadilike, runinga ya Watanzania aitazame na kuizingatia

Kama Magufuli atang'ang'ania kuendelea kuwa Rais, miaka 5 inayofuata itakuwa ya majonzi na mateso makubwa kwa Watanzania:

1) Watu watalipishwa kodi hata wasizostahili. Uwe unatengeneza faida au hasara, lazima utalazimishwa kulipa kodi ili pesa ipatikane kwaajili ya miradi mikubwa iliyoanza ambayo haizalishi fedha. Kutokana na hilo, wengi wataendelea kufunga biashara zao na kufilisiwa kupitia TRA.

2) Wakati anaingia, bajeti yetu ilikuwa inachamgiwa na nchi wahisani. Kutokana na uongozi mbaya, wahisani wengi wamekata misaada. Safari hii, itakapodhihirika ameendelea kuchezea demokrasia, hata wale wachache waliokuwa wamebakia, nao watasimamisha. Kwa vile, naye hatapenda aabike ionekane miradi aliyoanza imeshindikana, pengo hilo litazibwa kwa kuwabambikia watu kodi zisizolipika, kuwabambikia watu kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha matajiri ili waporwe fedha zao.

3) Harakati za wasiojulikana zitaongezeka maradufu. Kwa sababu kutakuwa na shida, manung'uniko yatakuwa mengi. Na yeye hatapenda yasikike. Hivyo kila mtu ambaye atasikika akinung'unika kwa uwazi au kwa kificho atakumbana na nguvu ya wasiojulikana. Kwa kuwa wanaolalamika hawataweza kupelekwa mahakamani, utaratibu wa kupotezwa utaimarika zaidi.

4) Uwekezaji utasinyaa sana. Kwa sababu ya mazingira ya hofu yanayojengwa na uonevu, watu wataogopa kuwekeza, hiyo ni kwa wawekezaji wa ndani na nje. Watanzania wenye mitaji mikubwa wataendelea kuwekeza nje ya Tanzania ili kujinusuru kufilisika. Jina la Tanzania litatajwa sana nje ya nchi kwa ubaya, na kusababishwa uwekezaji wa kutoka nje kukoma.

5) Kutokana na kusinyaa kwa uwekezaji, mzunguko wa fedha utakuwa mgumu sana, ukuaji wa ajira utazidi kuporomoka, vijana watazidi kupoteza matumaini kwa kukosa ajira

6) ili kupambana na wanaolalamika, sheria nyingi za kigandamizaji na kidikteta, zitatungwa ili kuzima sauti za wananchi.

7) Pamoja na kuwabambikia watu kodi zisizolipika, kuwatengenezea watu kesi za uhujumu uchumi, bado serikali haitakuwa na fedha za kukamilisha miradi iliyoanza. Hivyo serikali italazimika kuendelea kukopa mpaka kufikia uwigo wa mwisho wa kukopesheka. Hali hiyo, ikichangiwa na kupungua kwa mauzo ya nje, na kuendelea kuporomoka kwa ukuaji wa sekta ya utalii kutasababisha uhaba wa fedha ya kigeni na kuporomoka kwa sarafu ya Tanzania. Serikali itadhibiti sana upatikanaji wa fedha za kigeni kwa watu binafsi.

8) Viongozi wa ngazi za juu kwenye serikali, NEC, vyombo vya ulinzi na usalama, msajili wa vyama, watawekewa vikwazo kimataifa. Hali hiyo itazidi kuharibu taswira ya nchi mbele ya mataifa na kuathiri sekta zote. Zimbabwe, kama nchi, haikuwekewa vikwazo. Vikwazo waliwekewa viongozi wa serikali, madhara yake kila mmoja anayajua.

Najua haiwezekani lakini Rais Magufuli kama anawahurumia Watanzania, alistahili kutogombea kipindi cha pili cha miaka 5. Amekwishajenga image mbaya kwa wengi. Hata akibadilika, haitakuwa rahisi kurudisha imani kwa wawekezaji wa ndani na nje. Ni rahisi kipngozi kuonesha ana mwelekeo tofauti na mtangulizi wake kuliko yule yule wa zamani kusema kuwa nimebadilika.

Wanasema ukitaka kupambana na nyoka, hasa nyoka jamii ya mamba, ukianzisha tu mapambano, ukamjeruhi, uhakikisha unamwua. Ikitokea amenusurika, kama ilikuwa ni eneo la shamba, hama kabisa, usionekane hapo shambani, maana mtaisha. Uchaguzi huu, mpaka hapa tulipo, umemjeruhi Rahisi mpendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Magufuli hana "hekima" ...,ana kiburi,dharau,ni mnafiki,ndumila kuwili,mkabila,muongo na ana roho ya kishetani.
Hafai kuiongoza tena Tanzania kwa gharama yoyote!Watanzania "tusijaribu" tena kumpa "kichaa" Magufuli nchi inatosha!
 
Kazi za wakala wa shetani anayejifanya malaika wa nuru.Kwa nguvu ya Mwenyezi Mungu hatafanikiwa!
 
Mgombea wetu wa CCM akiwa Zanzibar anawaeleza Wazanzibar kuwa wasiondoke uwanjani hapo maana akimaliza hotuba bado Kuna show kabambe kutoka kwa wasanii na watamuona nae akicheza.... Wazenji nao viburi wakaondoka wakati anazungumza. Aisee!
Majinga sana maccm yani
 
Tumeumizwa sana kwa kweli.
 
Alikuwa akijiita Rais wa wanyonge kwa kuwaumiza wale waliokuwa matajiri, akidhani kwa kufanya hivyo ndio maskini wangetajirika, mpaka leo hajapandisha mishahara, hajawapandisha watu madaraja kazini, wastaafu hawapati pesa zao kwa wakati.
Nawaonea huruma sana matajiri. Wamekimbizwa sana miaka hii mitano. Natamani sana kuuona upinzani nchi hii ukiisemea sekta binafsi katika kampeni na hata baada ya kampeni watakapopewa nchi
 
Akipewa mitano tena, atakuwa mbaya kuliko tano iliyopita.
Hana cha kubembeleza maana katiba inamtaka kukalia kiti miaka10.
Kwa ivo hana cha kupoteza baada mitano mingine.
ASIPEWE
 
Tbc na manyau walimdanganya Sana jamaa kwamba anakubalika walimfeed taarifa za uongo azipendazo ambazo ni kinyume na Hali halisi
 
Hawezi kubadirika, Hana sababu ya kufanya hivyo. Chaguzi za awali CCM ikihofu nguvu ya wapiga kura, leo Sheria nyingi zimepitishwa na NEC ndio mwamuzi. Hakuna uwazi katika kuhesabu kura ndio maana hata mawakala simu sasa marufuku kuzitumia wakiwa kazini. Hana cha kupoteza ndio maana tunaingia uchaguzi huku ajira kwa vijana hakuna, mikopo ya elimu ni geresha ukipata mwaka wa tatu unanyang'anywa bila taarifa.
 
Mgombea wetu wa CCM akiwa Zanzibar anawaeleza Wazanzibar kuwa wasiondoke uwanjani hapo maana akimaliza hotuba bado Kuna show kabambe kutoka kwa wasanii na watamuona nae akicheza.... Wazenji nao viburi wakaondoka wakati anazungumza. Aisee!
Visiwani wanaenzi mila na desturi zao hasa kwa upande wa dini. Wasanii wanacheza minenguo ya kiashki huku wakishika sehemu za siri. Waungwana hawawezi subiri hilo.
 
Kiustaarabu hata kwa mtoto wa kuzaa huwezi mwaibisha mbele za watu. Udhalilishaji anaowafanyia wateule wake unawaumiza wao na sisi wananchi.
 
Lipo kundi dogo linafaidika na anayofanya magufuli, la wateuli na maafisa wakuu wa majeshi. Hali itazidi kuwa mbaya na hatimae nao wataanza kushikana uchawi.
 
Ni vyema watz October tuanze upya tukubali hasara ya miaka 5 ya kuharibiwa nchi yetu
 
Viongozi wa vyama vya upinzani wajitafakari. Hawakupaswa kuingia uchaguzi ambao mwaka mmoja nyuma CCM ilijipa ushindi wa 99.99%. Wapiga kura wengi watakaoipa CCM kura litakuwa kundi la vijijini. Mjini kura za CCM ni masanduku yatakayo ingizwa vituoni na tiss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…