Ukweli wanawake wapinzani ni makini zaidi ya wanaume

Ukweli wanawake wapinzani ni makini zaidi ya wanaume

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,663
Reaction score
15,225
Tuseme ukweli tu wanaume wengi wapinzani ukiwauliza tofauti ya sera hata hawajui. Wengine wengi wamekuwa wakipewa madaraka ya juu bila kuwa na ujuzi, moyo wa kujiamini na hata wengine wamekuja upinzani kwa kutafuta pesa.

Na hili ni hata kwa wakina Lowassa na Sumaye ukiwauliza kwanini walikuwa upinzani hawana sababu za kiundani wala wanayosema hayatoki moyoni ni kuhitaji madaraka tu.

Wanawake tuangalieni ndiyo wasomi zaidi, ndiyo ambao hawababaiki na kufuata mikumbo, ndiyo wanaoweza kueleza shida za Mtanzania wa kawaida.

Ukimuuliza wanawake wengi wa upinzani sababu ya kuwa upinzani watakupa sababu zao na ni za kweli. Utamaduni wetu wanaume wa Tanzania hasa wazee ni wazembe tuseme ukweli tu.

Shughuli za nyumbani nyingi wamewaachia wakina mama, bei za vyakula wanajua wakina mama, matatizo ya watoto wanajua wakina mama, wakina mama wanaongea shida zao.

Wanaume wanaondoka asubuhi wapitie bar na kuongea siasa na wengine kuongelea mitandao na wakina diamond, wengine kutafuta vi binti, na wengine kutafuta wa kuwatapeli.

Lakini wengine wanakuja mbuzi bar wakati hawajui nyumbani watoto wanakula nini!

Yaani nilikuwa bar na jamaa ana gombana na mke wake kwa kiasi cha kuacha nyumbani kwa ajili ya chakula cha watoto wake wakati yuko bar ana choma mbuzi.

Nasema ukweli tu mimi diaspora nimekuja huku na kujua kufanikiwa ni kushirikiana.

Yaani nilienda nyumbani baba yangu mzazi sijawahi kumuona anafanya kazi za nje hata siku moja kushika hata fagio au kusafisha choo chake mwenyewe!

Ni wafanyakazi au Mama sasa eti bado nikituma pesa nimtumie yeye ndiye aamue ampe Mama kiasi gani! Haiwezekani namtumia Mama yangu.

Dunia imebadilika na tutumie siku hii ya wanawake kujitafakari na kubadilika na kusadia.

Ujue mtoto wako ataenda kutumikiswa na kunyanyaswa kama Mama yako au bibi yako
 
Back
Top Bottom