Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.Mivutano ifuatayo ndiyo inayomtia kitanzini mzee wa kimyakimya.

VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.

Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi.

Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.

CHRISTOPHER OLE SENDEKA:

Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara. Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri.

Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.

SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:

Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.

Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.

Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.

BARAZA KUU UVCCM :

Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma. Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa. Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda.

Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia kazi
kwa kina.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.

We ndo mwendawazim kabisa! Iko wapi report ya uchunguzi wa hii scandal?
 
306681_10151063016359743_1581996414_n.jpg
 
Hakuna kitu hapo ray jay.

1. Kwanza kama huyo Mkono alikuwa analipwa hela nyingi na TANESCO, si wao wenyewe ndio waliingia naye huo mkataba au alikuwa anajilipa yeye mwenyewe hizo pesa?

2. Kuhusu hao unaosema wanatumika kupitia sakata la ESCROW, suala la msingi ni hili; je, huo ufisadi wa escrow ni sahihi? Kama ni sahihi, hatutaki kujua anayekomaa nao ana sababu zipi binafsi na hao mafisadi. La msingi kwanza mafisadi wawajibishwe, halafu ninyi ndio mrudi huko chamani kwenu muanze kushughulika na hizo kambi zenu. Kwa sababu tu kuna kambi ndani ya chama chenu haimaanishi kuwa mafisadi wasamehewe au waonewe huruma. Hayo mtayashughulikia baadaye kwenye vikao vya ndani kama mnavyofanya siku zote. [MENTION]IPTL Bring Back Our Money[/MENTION], na wahusika wawajibishwe!
 
Hakuna kitu hapo ray jay.

1. Kwanza kama huyo Mkono alikuwa analipwa hela nyingi na TANESCO, si wao wenyewe ndio waliingia naye huo mkataba au alikuwa anajilipa yeye mwenyewe hizo pesa?

2. Kuhusu hao unaosema wanatumika kupitia sakata la ESCROW, suala la msingi ni hili; je, huo ufisadi wa escrow ni sahihi? Kama ni sahihi, hatutaki kujua anayekomaa nao ana sababu zipi binafsi na hao mafisadi. La msingi kwanza mafisadi wawajibishwe, halafu ninyi ndio mrudi huko chamani kwenu muanze kushughulika na hizo kambi zenu. Kwa sababu tu kuna kambi ndani ya chama chenu haimaanishi kuwa mafisadi wasamehewe au waonewe huruma. Hayo mtayashughulikia baadaye kwenye vikao vya ndani kama mnavyofanya siku zote.

#IPTL-Bring-Back-Our-Money

...na wahusika wawajibishwe!
 
Acha kushoboko subiri riport ya CAG! Mbwembwe za nini? Namchukia Muhongo kama mavi!
 
Mimi sioni msafi ndani ya ccm,ata lipoti siwezi kuiamini sana.Tuwe na fikra mpya ya ku DELETE CCM.
 
Msikurupuke..ngojen ripoti ya CAG...!! Hakuna ulichoeleza hapa kujenga jungu juu ya jungu!! waache wabunge wafanye kazi yao,,, na ripoti ikija ndio hivo....

''Nyumba ya mfalme, malkia hafai hata kusingiziwa!!!!!
 
Acheni ujinga .Subirini ripoti ya CAG

Hatasalimika mtu hapa.Tumeziona nyaraka na tunaendelea kuzipata...

Safari hii mtakoma.Kazi ya kuwashambulia akina Zitto,Kafulila,Kangi Lugola na Filkunjombe ifanyeni baada ya Ripoti ya CAG

Lugora nae amekuwa na tabia za kipare za bendera fuata upepo, huyu si katika bunge lilopita alisema watu hawajui escrow account ni kitu gani na yeye ni polisi zile nyaraka za Kafulila ni karatasi za kufungia maandazi, kumbe Lugora yeye mwenyewe ndiye maandazi.
 
Hakuna kitu hapo ray jay.

1. Kwanza kama huyo Mkono alikuwa analipwa hela nyingi na TANESCO, si wao wenyewe ndio waliingia naye huo mkataba au alikuwa anajilipa yeye mwenyewe hizo pesa?

2. Kuhusu hao unaosema wanatumika kupitia sakata la ESCROW, suala la msingi ni hili; je, huo ufisadi wa escrow ni sahihi? Kama ni sahihi, hatutaki kujua anayekomaa nao ana sababu zipi binafsi na hao mafisadi. La msingi kwanza mafisadi wawajibishwe, halafu ninyi ndio mrudi huko chamani kwenu muanze kushughulika na hizo kambi zenu. Kwa sababu tu kuna kambi ndani ya chama chenu haimaanishi kuwa mafisadi wasamehewe au waonewe huruma. Hayo mtayashughulikia baadaye kwenye vikao vya ndani kama mnavyofanya siku zote. [MENTION]IPTL Bring Back Our Money[/MENTION], na wahusika wawajibishwe!
Ray jay hana taarifa zaidi ole sendeka ni rafiki mkubwa Wa Mizengo pinda na angependa ndiyo awe rais wa JMT. Sendeka vilevile hampendi Lowassa na Membe. Siku zote ni matamanio yake kwamba nchi hii itawaliwe na Sumaye au Mzee wa michakato ile ya kimyakimya. Ila yeye hamtaki Lowassa Kwa sababu anaogopa kuwa anaweza kulipiza kisasi dhidi ya ndombolo ya solo aliyocheza bungeni siku Lowassa alipojiuzulu uwaziri mkuu Kwa sababu ya siasa uchwara. Kutokana na Sendeka kuwa critique wa serikalini ya JK anahisi yeye pamoja na Mengi watakuwa kwenye first 11 Wa maadui wa joka la mdimu. Naomba kuwasilisha hoja.
 
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Hivi Lowasa bado ana ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania? Kaaatuuuuuu!

Kawajuza nini? Hivi Lizaboni bado upo kwa Membe? Zile pesa za Marehemu Gadafi naona mnaanza kuzitumia sasa kueneza Uongo na Kuwachonganisha Lowasa na Pinda , Hivi Membe hachoki tu na mbinu zake ? Tambueni Kuwa ile Roho ya Barozi wa Libya aliyejiua baada ya kuchukuchiwa Mkwanja wa Gadafi na Membe bado ipo na inawalilia wote waliomdhulumu hivyo itakuwa vigumu kuingia ikulu kwa kununua njia kwa kuzitumia pesa za Marehemu Gadafi. yaani hata mkimchafua Lowasa kila Dakika mjue Baba yako membe hawezi Kuwa Rais , Membe hata akisimamishwa na Jiwe Nina imani Hilo Jiwe litaibuka Kuwa Mshindi. Nchi hii Hakuna kiongozi aliye msafi kiasi cha kumnyoshea mwenzake kidole, kila Mtu ana madhambi na mapungufu yake ukifika mda tutayaanika mmoja baada ya mwingine.
 
Mimi sioni msafi ndani ya ccm,ata lipoti siwezi kuiamini sana.Tuwe na fikra mpya ya ku DELETE CCM.

Wamechakachua Mchakato wa katiba sembuse hiyo Report ambayo ipo huko ndani kwa ndani ! Hapo usitarajie jipya ww simama kwa kile unachokiamini tu kwani hata kura za maoni juu ya Katiba Mechi imeshachezwa nje ya Uwanja Matokeo ni Kura za Ndiyo wamepata ushindi wa 90% na Hapana 10% tu. chezea ccm wewe....
 
Ukweli upi hapo? majungu tu, tunataka uwajibikaji, pinda kapiga milioni 456 za Singa singa ni lazima awajibishwe ipasavyo , kwa sakata la IPTL msitafute huruma kwani mengi au mkono ndio aliwatuma kukwapua fedha za umma? PINDA, MUHONGO, MASWI and TIBAIJUKA and their Co must go
Mzee wa ipp yupo Pia na Zito lakini inaelekea Kama hajawapa chao chote si unajua Yule ni Mangi pesa anaisikilizia sana ndiyo Maana Wameamua kuvuta huku na huku Zito kala pande zote lakini Kafulila amekula za Mkono na mengi sasa anatamani za huko kwa mhindi wa IPTL akipewa tu anapiga Kiimya hadi Mengi awamalizie balance Yao ndipo wataanza tena kupiga moyowe, hii ndiyo Tz siasa za maji Taka hazitaisha kamwe.
 
kila nisemapo hila ndio inawapeleka ccm shimoni hawanielewi, sasa kamba imekatika wamedumbukia jumla
 
Kuna wabunge wamegeuza issue ya IPTL Kuwa Mladi aw kuvuta pesa,wanaenda kwa Mkono wanavuta kisha wanaenda kwa mengi wanavuta wakitoka hapo wanaelekea kwa Prof mhongo wanavuta huku Pia wakijipendekeza kwa Pinda kinafiki, yaana hili sakata ni mwendo wa Fursa kwa Wajanja ( kufa kufaana ) Wengi wameliwa pesa pasipo kujua hatima yake ni nini ! Hii ndiyo Tanzania Nchi ya Vioja hakika huu ni Upepo utapita tu.
 
Kwa hiyo na wewe kambi yako ni ya Pinda? Hongera. Na wewe nenda katafute za mzee wa kulia lia.
 
Back
Top Bottom