Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

ray jay

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
1,084
Reaction score
485
Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.Mivutano ifuatayo ndiyo inayomtia kitanzini mzee wa kimyakimya.

VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.

Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi.

Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.

CHRISTOPHER OLE SENDEKA:

Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara. Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri.

Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.

SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:

Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.

Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.

Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.

BARAZA KUU UVCCM :

Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma. Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa. Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda.

Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia kazi
kwa kina.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.
 
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Hivi Lowasa bado ana ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania? Kaaatuuuuuu!
 
Mavijana ya ccm yanawaza Rushwa tu.

Bila rushwa hayaende haya matoto ya panya nayo ni mapanya tu.
 
Kalete drama nyingine hii imechuja

mbaazi ukikoss maji husingizia jua....

ray jay Kama ishu ni nyepesi namna hiyo mbona kuna kigugumizi kizito kuiachia ripoti ya escrow hadharani?
 
Last edited by a moderator:
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Ukweli upi hapo? majungu tu, tunataka uwajibikaji, pinda kapiga milioni 456 za Singa singa ni lazima awajibishwe ipasavyo , kwa sakata la IPTL msitafute huruma kwani mengi au mkono ndio aliwatuma kukwapua fedha za umma? PINDA, MUHONGO, MASWI and TIBAIJUKA and their Co must go
 
Halafu mkuu mbona kila siku hawa jamaa wakisema "ukweli kuhusu..." baada ya muda mchache tu tunagundua pia ni kanusho la uongo
Mavijana ya ccm yanawaza Rushwa tu.

Bila rushwa hayaende haya matoto ya panya nayo ni mapanya tu.
 
Upuuzi tu huu! tena huna akili timamu kabisa, yaan sisi ndo unatuletea upuuzi huu hapa!! nyambafu kabisa...Tuna akili zetu timamu wengine...
 
Hatari wakuu. Kila muadilifu madisadi wanataka kumchafua. Sasa sijui nani atabaki hapa
 
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Teh teh teh

Kama huu ndio ukweli mbona ripoti haiwekwi hadharani?

Unaongeleaje suala la waliojipambanua ni wasafi kuchota mabilioni haya ya umma kwa maslahi binafsi?

Labda Kama unaishi hapa kwa kusimuliwa tu but ungebahatika kuona kilichopo ndani ya ripoti usingejiabisha Ku comment utoto huu
 
Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.Mivutano ifuatayo ndiyo inayomtia kitanzini mzee wa kimyakimya.

VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.

Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi.

Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.

CHRISTOPHER OLE SENDEKA:

Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara. Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri.

Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.

SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:

Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.

Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.

Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.

BARAZA KUU UVCCM :

Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma. Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa. Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda.

Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia kazi
kwa kina.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.

Acheni ujinga .Subirini ripoti ya CAG

Hatasalimika mtu hapa.Tumeziona nyaraka na tunaendelea kuzipata...

Safari hii mtakoma.Kazi ya kuwashambulia akina Zitto,Kafulila,Kangi Lugola na Filkunjombe ifanyeni baada ya Ripoti ya CAG
 
Vp tena mnapingana na kuulizana wenyewe kazi kweli kweli. Hapa mlipofikia na ulivyoandika ndio tunajua Membe,Lowassa, Pinda ni yupi. Mnalo lenu ilo.
 
Hatari wakuu. Kila muadilifu madisadi wanataka kumchafua. Sasa sijui nani atabaki hapa

Muadilifu nani? mtaje kwa jina tumjue.....

Au unamwongelea yule alokabidhiwa fuko la hela za BMK akatokomea nazo na kupiga chenga kuzirudisha??

Unaongelea waadilifu wanaokwapua mapesa ya NSSF.... wafadhili Wa kiarabu kusaka urais?

Tutajie majina ya hao waadilifu basi......

uko too low ktk this game utaaibika bure....
 
Acheni ujinga .Subirini ripoti ya CAG

Hatasalimika mtu hapa.Tumeziona nyaraka na tunaendelea kuzipata...

Safari hii mtakoma.Kazi ya kuwashambulia akina Zitto,Kafulila,Kangi Lugola na Filkunjombe ifanyeni baada ya Ripoti ya CAG

Ha ha ha ktk hili nakuunga mkono mkuu

Kama anaona anayoyasema mepesi aiweke report hapa asilete porojo

Sipati picha wanaowatuma watakua na ajenda gani ya kujiuza kwa watu maana ya uadilifu itazimika punde hata isipowekwa Leo tutaisema bila woga 2015
 
Mkuu, ni lini umeanza kuwa na mapenzi na Zitto?
 
Ha ha ha ktk hili nakuunga mkono mkuu

Kama anaona anayoyasema mepesi aiweke report hapa asilete porojo

Sipati picha wanaowatuma watakua na ajenda gani ya kujiuza kwa watu maana ya uadilifu itazimika punde hata isipowekwa Leo tutaisema bila woga 2015
Ben Saanane ni mtu wa ajambu sana. Nakushangaa mkuu Lusundo kwa kuunga mkono hoja anbayo huijui
 
Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.
Sasa mbona hatujaona ''your take'' kwenye post yako?
 
Wewe umepewa sh ngapi kumsafisha Linda? Ebu wekeni report wazi tuchambue wenyewe pumba na mchele.
Yaani familia chache zipige hella alafu wewe uchukue muda wako kuwasafisha na kuwachafua wengine.safari hatoki mtu wote tunawatia kitanzi.
 
Ben Saanane ni mtu wa ajambu sana. Nakushangaa mkuu Lusundo kwa kuunga mkono hoja anbayo huijui

Wow mkuu Sana Chabruma umerudi??

Habari za kazi na masahibu mengi?

Ktk sakata la ESCROW hakuna nisichokijua maana mie ni miongoni mwa vidagaa tunaohangaishwa maofisini kuziba matundu boma lisibomoke....

Mimi naangalia kweli... Kweli tupu ndio maana siangalii nasaba...imani au itikadi ya MTU ktk utoaji Wa maoni isipokuwa content....

Swali la kizushi: Kama hili suala ni jepesi na la kitoto mbona ripoti haiwekwi hadharani?

Kama ni jepesi hivyo tunahangaika nini kiasi cha kukosa usingizi kutafuta Huruma ya wafadhili?

Hizi danadana za nini?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom