Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

Ukweli wa tuhuma za Pinda huu hapa

Wow mkuu Sana Chabruma umerudi??

Habari za kazi na masahibu mengi?

Ktk sakata la ESCROW hakuna nisichokijua maana mie ni miongoni mwa vidagaa tunaohangaishwa maofisini kuziba matundu boma lisibomoke....

Mimi naangalia kweli... Kweli tupu ndio maana siangalii nasaba...imani au itikadi ya MTU ktk utoaji Wa maoni isipokuwa content....

Swali la kizushi: Kama hili suala ni jepesi na la kitoto mbona ripoti haiwekwi hadharani?

Kama ni jepesi hivyo tunahangaika nini kiasi cha kukosa usingizi kutafuta Huruma ya wafadhili?

Hizi danadana za nini?

Mkuu lusungo..
Heshima nyingi sana kwako.. Naomba nikupongeze sana maana kwa hili unaongozwa na uzalendo wako kwa taifa.. Hawa akina Chabruma & co wanaongozwa na tamaa binafsi za kujaza matumbo yao na wako tayari kuutetea uovu ili mradi tu wananufaika wao..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, ni lini umeanza kuwa na mapenzi na Zitto?

Ben daima ana mapenzi na ukweli hangalii aliyesema ukweli anatoka upande gani (Si kwa ZZK au Nape) kama vile wewe ukiona mtu kaisema vizuri CDM kwa kufanya mazuri bado wewe huishia kupinga tu kama chizi fulani
 
Acheni ujinga .Subirini ripoti ya CAG

Hatasalimika mtu hapa.Tumeziona nyaraka na tunaendelea kuzipata...

Safari hii mtakoma.Kazi ya kuwashambulia akina Zitto,Kafulila,Kangi Lugola na Filkunjombe ifanyeni baada ya Ripoti ya CAG

Comment hii toka kwako nimeipenda. Like ni halali yako
 
porojo hizi nazifananisha na mavi. yaani pesa zetu zimeibiwa halafu wapumbavu kama wewe unakuja na utumbo wako hapa? maajabu haya.
between pesa zetu zirudi; hakuna cha mjadala kwenye hili.
 
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Hivi Lowasa bado ana ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania? Kaaatuuuuuu!

Si ni mwenzenu katika chama? Hatakiwi kuwa na ndoto hizo?

By the way, ikiwa mnamfahamu kuwa ni fisadi, chama kimemchukulia hatua gani?
 
Hatari wakuu. Kila muadilifu madisadi wanataka kumchafua. Sasa sijui nani atabaki hapa

Naombea mnipe kama milioni moja niwarushie bundle wotw humu JF. labda niwe chizi kugawa pesa.
 
Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.Mivutano ifuatayo ndiyo inayomtia kitanzini mzee wa kimyakimya.

VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.

Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi.

Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.

CHRISTOPHER OLE SENDEKA:

Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara. Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri.

Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.

SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:

Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.

Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.

Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.

BARAZA KUU UVCCM :

Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma. Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa. Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda.

Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia kazi
kwa kina.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.
Hata wasipomchafua, tuwe wakweli Pinda urais hauwezi na yeye mwenyewe alishawahi kusema hana nia ya kuwania nafasi hiyo. Sasa kama anakuwa bendera fuata upepo ataanguka vibaya
 
Tunaamua kumpigia debe Mkuu wa nchi mwenye ndoto za kufuga nyuki, mkulima? Hili taifa limerogwa na nani? Ifika mahala thread zinazomhusu huyu mtoto wa mkulima kama zinahusu kuutaka urais hapa Jf zifutwe.
 
Hapana atakuwa amenyimwa haki yake ya msingi wacha tu ajadiliwe kama atapata atapata tu na kama ni kukosa atakosa tu!!
 
Hatari wakuu. Kila muadilifu madisadi wanataka kumchafua. Sasa sijui nani atabaki hapa

Kwa hiyo kwa akili zako ulivyoziaminisha Pinda ni muadilifu? kwa sasa ndani ya CCM hakuna msafi
 
Hatari wakuu. Kila muadilifu madisadi wanataka kumchafua. Sasa sijui nani atabaki hapa

Kwa hiyo kwa akili zako Pinda ni muadilifu. sijui umetumia kigezo gani au umetumia Sura?
 
Wakuu habari za asubuhi .Kile kinachoonekana kuwa ni kuchafuliwa kwa eaziri mkuu mh. Mizengo Pinda hivi karibuni kimebainika.
Vigogo wasaka urais na Wabunge mbalimbali kama David Kafulila, Sendeka, Serukamba na Ligola wakiwa wamelishika sakata la bilioni 200 za Escrow na wengine wakiwa wanataka Pinda ang'olewe katika nafasi yake ya waziri mkuu.

Imefahamika kuwa si kweli kuwa mtoto huyu wa mkulima anahusika. Bali ni vita kati ya wabunge, baadhi ya mawaziri na Urais 2015.Mivutano ifuatayo ndiyo inayomtia kitanzini mzee wa kimyakimya.

VITA YA WABUNGE :Inasemekana David Kafulila anatumiwa na mh. Mbunge tajiri Nimrod Mkono. Mkono ana ugomvi mkubwa na TANESCO kutokana na malipo yake ya mamilioni ya dola aliyokua analipwa na serikali kila mwezi kupitia TANESCO kusitishwa na Muhongo na katibu mkuu wake Maswi.

Malipo haya tata yalikuwa ni ya kazi ya Mkono kama mwanasheria wa TANESCO. Hoja hapa ilikua ni kubainika kuwa malipo hayo yalikuwa mkubwa sana na yaligubigwa na giza katika kiwango cha malipo. Hivyo Mkono anataka Prof Muhongo ang'olewe katika wizara ya nishati na madini kama kisasi.

Ndipo David Kafulila akapewa kazi hiyo kupitia ESCROW na anakula pesa za Mkono kwa kazi hii.

CHRISTOPHER OLE SENDEKA:

Huyu ni Mbunge wa Simanjiro na rafiki kipenzi wa Reginald Mengi wa IPP. Mtakumbuka vita ya mzee Mengi na Muhongo juu ya vitalu vya gesi hivi karibuni. Wawili hawa walichapana sana hadharani na kwenye makongamano huku Muhongo akidai kuwa Mengi ni dalali na sio mfanyabiashara. Hasira za Mengi zimeelekezwa katika kumng'oa prof Muhongo katika kiti chake cha uwaziri.

Hii ilibainika wakati wa kupitisha bajeti ya prof Muhongo mwaka huu. Baadhi ya wabunge wanasemekana kuhongwa ili wamshambulie Muhongo na kukwamisha bajeti yake. Kazi hii inafanyika sasa kupitia sakata la ESCROW. Ole Sendeka anasemekana kutumiwa na bilionea Mengi kumchapa Muhongo kama kisasi cha sakata la vitalu lililomvua nguo Mengi.

SERUKAMBA,FILIKUNJOMBE:

Wabunge hawa wanaongoza kundi la wabunge wa kambi ya mgombea Urais mmoja wa CCM mwenye nywele nyeupe. Hawa nia yao hasa ni kumchapa Pinda. Wanatumwa na kupewa fedha ili kuhakikisha kwa gharama yoyote wanatumia vuguvugu hili kama fursa ya kumsafishia njia mgombea wao kwa kumuhusisha Waziri Mkuu Pinda na sakata la ESCROW.

Lengo hapa ni kumuondoa madarakani japo hahusiki ili ionekane kuwa hata mgombea wao aliwajibika kisiasa tu na hivyo kumsafishia njia nywele nyeupe. Aidha katika siku za karibuni Pinda anasemekana tangu kuanza kutajwa kugombea Urais amepata kuungwa mkono sana na kuvuna wapambe wengi wa wagombea wengine akiwemo Nywele nyeupe.

Pinda ameonekana kuwapiku wenzie walioanza mbio hizi mapema kutokana na uadilifu wake na kuwa ni mtu anayependa watu, asiye na majivuno na aliyekuwa karibu sana na baba wa taifa hayati mwalimu Nyerere . Hivyo ni lazima ashughulikiwe apunguzwe kasi na ikiwezekana ajiuzulu kabisa ili kufanya safari ya nywele nyeupe kuwa nyepesi.

BARAZA KUU UVCCM :

Juhudi za kumchafua Pinda zimeendelea pia wakati wa vikao vya BARAZA KUU la UVCCM Dodoma. Kazi hii inaratibiwa na kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Somalia akiwa ameweka kambi Dodoma. Kada huyu ameleta kundi la vijana zaidi ya 30 wasiokua wajumbe wala watumishi wa CCM kutoka sehemu mbalimbali.

Vijana hawa walikua Dodoma wakila na kunywa na kulipwa posho Kazi yao kubwa ikiwa ni kurandaranda katika baa na kumbi zote za Dodoma usiku na mchana kufuatilia wafuasi wa Pinda wamekaa na nani na namna bora ya kumchafua Waziri Mkuu kwa kumuhusisha na ugawaji wa pesa. Kundi hili lilizagaa Dodoma kama paka wa baa kunusa kila mahali na kuandika mitandaoni kumchafua mzee Pinda.

Inasemekana posho yao ilikua kati ya sh 100,000 na 200,000 kulingana na taarifa unayopeleka kwa kada huyo Msomali. Uroho wa pesa uliwafanya vijana hao kupeleka taarifa za uongo mradi wapate kula yao.Hii ndio hali halisi wakuu juu ya mambo haya ambayo nimeyafanyia kazi
kwa kina.

Pinda anaonekana ni tishio kwa wataka Urais ndani ya CCM.

Pamoja na Mh.Pinda kuonekana bayana hana mvuto kuwa rais kw amantiki ya vigezo hata wewe uliyeandika huu uzi HUNA NGUVU YA USHAWISHI KWA KUTUMIA MAANDISHI
 
Dah! Mafisadi watatumaliza. Ahsante mkuu kwa kutujuza ukweli

Hivi Lowasa bado ana ndoto ya kuwa Rais wa Tanzania? Kaaatuuuuuu!

Hivi vijana wa Buku7 walishukiwa na roho wa Bwana au kibarua cha lumumba kiliota mbawa?
 
Panya jike amempa mimba paka dume, ngoje tuone itakukwaje hadithi hii na mkasa huu
 
Back
Top Bottom