Ukweli wa kifo cha Kighoma Ally Malima ni upi?

Kighoma Ally Malima aliiba mamilioni ya Tsh wakati wa Utawala wa Mzee Mwinyi.
Mzee Mwinyi alipostushwa kuwa Hazina imefujwa akamuondoa mwizi yule, akampeleka Jakaya Mrisho Kikwete katika Wizara ya Fedha , kukafanyika Boonge la ukaguzi, wakafukuzwa na maofisa kumi na mbili.
 
No Research NO RIGHT TO SPEAK! Kusema Kighoma Ally Malima ndo alieanzisha utaratibu wa namba ni Uwongo mtupu na utafutaji wa sifa za kijinga! Wengine tumefanya mitihani ya shule ya Msingi na Sekondari ( form 1-6) miaka ya 80 Kwa kutumia NAMBA kabla Hayati Malima hajawa Waziri wa Elimu, Upotoshaji huu hautusaidii chochote.
Mkuu tunachotaka ni wewe kusema mwaka gani ulikaa mtihani na ukatumia namba badala ya jina hasa kidato cha nne.Sisi wote tumesoma Tanzania tunamjua mtu ama ndugu zetu waliosoma mwaka huo huo unaosema wewe hivyo leta research yako tulinganishe na madai ya hao wengine.
Nijuavyo mimi sisi tulosoma kabla ya Mwinyi tulitumia majina na sio namba, kisha wakati wa Mwinyi yalikuja maswala ya kutumia namba - Je, nani alikuwa waziri wa Elimu? maana usiseme kabisa namba zimeanza kutumika wakati wa Nyerere.. Sii kweli - na hata hivyo nina jamaa zangu wamesoma wakati wa Mwinyi na wametumia vyote yaani majina na namba hasa mitihani ya sekondary.. Kisha twambie ni wakati gani namba zimeacha kutumika tena ikarudi ktk majina kama tulivyoona ya mwaka huu. Wewe mwenye research na right ya ku speak tufahamishe basi?
 
Hizo ndio tunaita facts, kwani bila hizi facts watu wachache wenye nia mbaya za kidini wanaweza kutuyumbisha kama taifa.

Kuna makundi ya Kiharakati wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu kwa maslahi ya makundi yao na wafadhili wao.
Mwaka 1985 nilifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi pale Mzimuni P/school, Magomeni. Watahiniwa wote tulitumia namba badala ya majina; hata karatasi za majibu yetu tuliandika namba, namba yangu ilikuwa 6.
 
je unafahamu prof Malima ameteuliwa wizara hiyo mara mbili. Nadhani we ulikuwapo wakati anateuliwa mara yapili na dhani nimekutosha. Kabla ya kuingia mara ya kwanza kweli ulikuwapo lakini haukufanya kazi akaona ni bora kuurejesha acha ushabiki

Mgongo wa paka,

..Malima amewahi kuongoza wizara ya elimu mara moja tu wakati wa Mzee Ali Mwinyi.

..Wizara ya Fedha ndiyo aliongoza mara mbili, mara ya kwanza wakati wa Mwalimu Nyerere na mara ya pili wakati wa Mzee Mwinyi.

..lakini hebu jiulize utendaji wake ktk wizara ya Fedha ulikuwaje?
 
Mkuu tunachotaka ni wewe kusema mwaka gani ulikaa mtihani na ukatumia namba badala ya jina hasa kidato cha nne.Sisi wote tumesoma Tanzania tunamjua mtu ama ndugu zetu waliosoma mwaka huo huo unaosema wewe hivyo leta research yako tulinganishe na madai ya hao wengine.
Nijuavyo mimi sisi tulosoma kabla ya Mwinyi tulitumia majina na sio namba, kisha wakati wa Mwinyi yalikuja maswala ya kutumia namba - Je, nani alikuwa waziri wa Elimu? maana usiseme kabisa namba zimeanza kutumika wakati wa Nyerere.. Sii kweli - na hata hivyo nina jamaa zangu wamesoma wakati wa Mwinyi na wametumia vyote yaani majina na namba hasa mitihani ya sekondary.. Kisha twambie ni wakati gani namba zimeacha kutumika tena ikarudi ktk majina kama tulivyoona ya mwaka huu. Wewe mwenye research na right ya ku speak tufahamishe basi?

Mkandara,

..mimi nimefanya mtihani wakati wa Mwalimu Nyerere na nilitumia nambari ya mtihani.

..hakuna kitu kama kuandika jina lako ktk karatasi ya mtihani.

..kukumbusha baraza la mitihani la taifa limeanzishwa mwaka 1973.

..labda wewe ulifanya mitihani ya baraza la east africa au ulifanya mitihani ya cambridge.

..je, wakati wenu mlikuwa mkitumia majina???

NB:

..Dr.Ndalichako kaeleza vizuri sana mchakato mzima wa kutunga na kusahihisha mitihani.

..huwezi kuleta ujanja-ujanja mle zaidi ya kuiba mtihani wenyewe.

..halafu ukizingatia kwamba mtihani unahusisha material za miaka 4 huwezi kushinda bila kuwa mwanafunzi mzuri. naamini hiyo ndiyo sababu ya watu kuiba mtihani lakini bado wanashindwa.
 
Kuna makundi ya Kiharakati wanatoa majibu mepesi kwa maswali magumu kwa maslahi ya makundi yao na wafadhili wao.
Mwaka 1985 nilifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi pale Mzimuni P/school, Magomeni. Watahiniwa wote tulitumia namba badala ya majina; hata karatasi za majibu yetu tuliandika namba, namba yangu ilikuwa 6.
Na mtihani wa sekondary kidato cha nne?
 
Ukweli ni kuwa namba za mitihani zilitumika kwa miaka mingi. Hivyo wanaosema namba za mitihani hawana ukweli wowote.

Kitu Malima alichofanya akiwa kama Waziri wa Elimu ni kutoa namba kwa shule za sekondari binafsi au usajili wa sekondari binafsi kuwa vituo vya mitihani.

Shule nyingi za binafsi kama vile za kidini, shule za wazazi na jumuia nyingine zilikuwa hazipati usajili au kuwa na namba kama kituo cha mitihani. Matokeo yake ni kuwa watu walikuwa wanamaliza shule lakini mitihani walifanya kama private candidates.

Waislamu walikuwa na wakati mgumu wa kusajili shule. Lakini hawakuwa peke yao. Kuna Madhehebu mbalimbali ya Kikristo na taasisi zinginge zilishindwa kusajili shule zao. Hii ilikuwa ni sera ya serikali YA KIJAMAA kuzuia mfumo wa shule binafsi wakati yenyewe haiwezi kutoa huduma za shule.

Kwa mfano kule Mwanza, walianzisha shule za Wakulima. Shule ya kwanza ilikuwa shule sekondari Geita. Wanafunzi wengi wa mwanzo wa shule hii walimaliza bila kuwa na nafasi ya kufanya mitihani na athari yake ilikuwa kubwa kwa wenyeji wa wilaya ya Geita.
 
trend gani na wewe.hivi kwanza hao wasomi sana wa kikristo wapogo wapi?kuna kina lipumba,shivji,safari,bilali,haroub e.t.c.
Ukiacha profesa lwaitama na kingereza chake cha la tatu hivi kuna profesa ama dr gani christian na kwanini hawasikiki?

Avumae baharini ni papa lakini na wengine wapo; nyie mmewazoea watu wanaojitangaza kwenye luninga na magazetini lakini kuna wengi magwiji ambao hawataki publicity!!vizuri hujiuza lakini vibaya shalti vijitembeze.
 
Mkandara,

..mimi nimefanya mtihani wakati wa Mwalimu Nyerere na nilitumia nambari ya mtihani.

..kukumbusha baraza la mitihani la taifa limeanzishwa mwaka 1973.

..labda wewe ulifanya mitihani ya baraza la east africa au ulifanya mitihani ya cambridge.

..je, wakati wenu mlikuwa mkitumia majina???
Sawa kabisa NECTA ilianzishwa mwaka 1973, lakini nilikuwa sijakaa mtihani wa kidato cha nne na nilifanya mtihani kwa kutumia JINA sio namba na hata majibu yalipotoka yalikuwa kwa majina yetu. Hata Primary mitihani ya baraza la EA iliondolewa baada ya Azimio la Arusha waliokaa mtihani ya mwaka 1969 hadi kuendelea kuanzia darasa la saba hawakufanya mtihani wa EA...
 
Mi alinifurahisha alipokuwa anatetea majina yasitumike ktk mitihani - badala yake zitumike namba, NICE MOVE

Prof Malima aliukuta mfumo wa namba kwenye mitihani, nami nilitumia namba 1985 hata Prof Malima hajawa Waziri.
Mnadanganyika kirahisi mno na ndo maana Waislamu ni kundi lililo rahisi kutumika kwa maslahi ya Wanasiasa.
 
Mkandara,

..mimi nimefanya mtihani wakati wa Mwalimu Nyerere na nilitumia nambari ya mtihani.

..hakuna kitu kama kuandika jina lako ktk karatasi ya mtihani.

..kukumbusha baraza la mitihani la taifa limeanzishwa mwaka 1973.

..labda wewe ulifanya mitihani ya baraza la east africa au ulifanya mitihani ya cambridge.

..je, wakati wenu mlikuwa mkitumia majina???

NB:

..Dr.Ndalichako kaeleza vizuri sana mchakato mzima wa kutunga na kusahihisha mitihani.

..huwezi kuleta ujanja-ujanja mle zaidi ya kuiba mtihani wenyewe.

..halafu ukizingatia kwamba mtihani unahusisha material za miaka 4 huwezi kushinda bila kuwa mwanafunzi mzuri. naamini hiyo ndiyo sababu ya watu kuiba mtihani lakini bado wanashindwa.

Mkuu,

Dr. Ndalichako anazungumza utumbi tu. Mambo yote ni supply and demand.

Watu wanaiba mitihani sio kwa sababu ya kuwa mwanafunzi wabaya. Wanaiba mitihani kwa sababu ya competition. Katika miaka ya 80s, 90s ni 3% ya wanafunzi waliendelea na masomo ya sekondari. Na kabla ya kuanzisha mashule ya kata, kulikuwa na zaidi ya wanafunzi 700,000 wanaomaliza darasa la saba, na kati ya hao ni 10,000-20,000 waliendelea na shule za sekondari za serikali 10,000 private. Na waliofanya kidato cha sita ni 20,000 na waliondelea na vyuo vikuu chini ya 5000.
 
kim kardash utaenda peponi inshaallah!
Mkuu Kim amenena vyema. Sijui habari za msikiti wa Malima lakini ni kweli kwamba waislam wengi hutenga/hutengewa sehemu za kuabudu hasa kwenye maofisi ya serikali. Utawaona mchana saa saba wanaenda kuchukua udhu na kujihudhurisha kwenyd ibada. Ofisini kwetu huwa nawaona. Nadhani hili si tatizo tatizo ni kujenga msikiti.
 
Sawa kabisa NECTA ilianzishwa mwaka 1973, lakini nilikuwa sijakaa mtihani wa kidato cha nne na nilifanya mtihani kwa kutumia JINA sio namba na hata majibu yalipotoka yalikuwa kwa majina yetu. Hata Primary mitihani ya baraza la EA iliondolewa baada ya Azimio la Arusha waliokaa mitihani ya mwaka 1969 hadi kuendelea darasa la saba hawakufanya mtihani wa EA...

Mkandara,

Nilitumia namba. Tena darasa la saba. Lakini hili upate namba ni lazima shule yako iwe imesajiliwa na iwe kituo cha mitihani.

Malima alichofanya ni kuakikisha kuwa shule binafsi zinapata namba za usajiri wa kuwa vituo vya mitihani. Hili iliwezesha shule nyingi binafsi kusajiliwa na kuwa vituo vya mitihani.

Hivyo shule nyingi za kidini na taasisi zingine ambazo kwa miaka mingi zilikuwa hazina usajili zipata namba.
 
Mkuu,

Dr. Ndalichako anazungumza utumbi tu. Mambo yote ni supply and demand.

Watu wanaiba mitihani sio kwa sababu ya kuwa mwanafunzi wabaya. Wanaiba mitihani kwa sababu ya competition. Katika miaka ya 80s, 90s ni 3% ya wanafunzi waliendelea na masomo ya sekondari. Na kabla ya kuanzisha mashule ya kata, kulikuwa na zaidi ya wanafunzi 700,000 wanaomaliza darasa la saba, na kati ya hao ni 10,000-20,000 waliendelea na shule za sekondari za serikali 10,000 private. Na waliofanya kidato cha sita ni 20,000 na waliondelea na vyuo vikuu chini ya 5000.
Mkuu mimi nakubaliana na wewe sana tu na ndivyo nilivyoelewa mimi kwamba tulishindwa kuendelea na masomo kwa sababu hatukuwa na shule za sekondary na vyuo vya kutosha.

Lakini inapofikia watu wanaanza kubishana kuhusu matumizi ya namba na majina, nafasi ya Malima ktk ELimu nchini ndipo naposhangaa na kujiuliza tena pengine kuna ukweli ktk madai ya Malima. haiwezekani kabisa waziri mzima aandike barua na kupinga mfumo wa Elimu nchini halafu watu waje kutetea hapa na kumwita yeye ndiye mdini na wasipinge hoja yake. Yeye alikuwa kichaa? Haya leo hii mimi Mkandara napinga kabisa mfumo wa elimu nchini unaounganisha serikali na CSSC naonekana kicha vile vile.. Lakini ukweli ni upi?.. kesho watu watakuja bishana vile vile kwamba serikali haiwajawahi kushirikiana na kanisa.
 
Mkandara,

Nilitumia namba. Tena darasa la saba. Lakini hili upate namba ni lazima shule yako iwe imesajiliwa na iwe kituo cha mitihani.

Malima alichofanya ni kuakikisha kuwa shule binafsi zinapata namba za usajiri wa kuwa vituo vya mitihani. Hili iliwezesha shule nyingi binafsi kusajiliwa na kuwa vituo vya mitihani.

Hivyo shule nyingi za kidini na taasisi zingine ambazo kwa miaka mingi zilikuwa hazina usajili zipata namba.
Darsa la saba sina wasiwasi najua wanatumia namba ila sielewi mwaka gani ilianza na hadi leo bado wanatumia namba. Mimi nazungumzia hili la sekondari limeanza lini maana nijuavyo mimi sisi tulitumia majina, kisha ikawa namba na majina sasa imerudi ktk majina.. Hii imetokea vipi na lini kumekuwa na mageuzi au marekebisho haya..mwenye data atujuze maana najua vitu vyote vimetokea.
 
Mkuu,

Dr. Ndalichako anazungumza utumbi tu. Mambo yote ni supply and demand.

Watu wanaiba mitihani sio kwa sababu ya kuwa mwanafunzi wabaya. Wanaiba mitihani kwa sababu ya competition. Katika miaka ya 80s, 90s ni 3% ya wanafunzi waliendelea na masomo ya sekondari. Na kabla ya kuanzisha mashule ya kata, kulikuwa na zaidi ya wanafunzi 700,000 wanaomaliza darasa la saba, na kati ya hao ni 10,000-20,000 waliendelea na shule za sekondari za serikali 10,000 private. Na waliofanya kidato cha sita ni 20,000 na waliondelea na vyuo vikuu chini ya 5000.

Zakumi,

..Ndalichako ametetea integrity ya zoezi la utungaji mtihani na usahihishaji.

..kuna watu wanadai hata ktk kusahihisha wamejaa wakatoliki wengi ambao wanawanyima maksi Waislamu.

..sasa ndiyo mimi nikaeleza kama mambo yako kama alivyobainisha Dr.Ndalichako basi huwezi kufanya udanganyifu zaidi ya kuiba mtihani wenyewe. zaidi nikaeleza hata ukiiba mtihani, ili ufaulu, you have to be a good student kwasababu maswali ya mtihani yana-cover material ya miaka 4 kwa o-levels na miaka 2 kwa a-levels.

..binafsi nilipokuwa jeshini nili-solve paper ya mtihani wa form 4 kwa madogo fulani, na nilikuwa very curious kuona matokeo yao yangekuwaje. well, matokeo yalipokuja vijana wale waliambulia div 4 na wengine wakabahatisha 3. ndiyo maana nime-conclude kwamba paper iliyoibiwa only helps the brighter and capable students.
 
Darsa la saba sina wasiwasi najua wanatumia namba ila sielewi mwaka gani ilianza na hadi leo bado wanatumia namba. Mimi nazungumzia hili la sekondari limeanza lini maana nijuavyo mimi sisi tulitumia majina, kisha ikawa namba na majina sasa imerudi ktk majina.. Hii imetokea vipi na lini kumekuwa na mageuzi au marekebisho haya..mwenye data atujuze maana najua vitu vyote vimetokea.

Mkandara,

..haiyumkiniki mtihani wa std 7 watumie namba halafu wa form 4 watumie majina.

..utaratibu wa kutumia nambari za mtihani kwa mitihani ya taifa haukuanza na Prof.Malima.
 
we kweli hujui hii nchi imetoka wapi? yani hujui malima alikua waziri wa elimu na ndiye aliyeanzisha mfumo wa namba? na wewe bado unaamini mpaka leo trend ya ufaulu wa waislam ipo vilevile?

Mbona sisi tuliofanya Mtihani wa Cambridge Overseas Schools Cerficate mwaka wa 1952 tulitumia namba na sio majina yetu? Kwani kulikuwa na Waziri aliyefuta utaratibu huo baada ya Uhuru?

Kwa swali langu namaanisha siyo sahihi kumpa credit Kighoma Malima kwamba ndiye aliyeanzisha utaratibu wa kuwa na Namba badala ya majina wakati wanafunzi wakifanya pan-territorial examinations. Badala ya sisi hapa JF kubishana, tuombe Wizara ya Elimu kuthibitisha ni lini mtindo wa namba kwa wanafunzi ulianza na ulianzishwa na Waziri gani wakati huo wa ukoloni.
 
Mkandara,

..haiyumkiniki mtihani wa std 7 watumie namba halafu wa form 4 watumie majina.

..utaratibu wa kutumia nambari za mtihani kwa mitihani ya taifa haukuanza na Prof.Malima.
Mkuu wangu nina mke, watoto na ndugu ambao wametumia majina na namba ktk mtihani wa kidato cha nne, tunabishana kitu gani. MImi nimesema sikutumia namba na naomba uniamini hilo halafu kama wewe umetumia namba basi jua kuna watu wengine wametumia majina na namba (kujaza karatasi ya mtihani) sababu sizielewi na pengine ndio kinachotutatiza ktk hoja hii.. why others watumie namba na wengine watumie majina na namba..na hata majibu yao yalipotoka tulienda kusoma majina yao. Sikumbuki kusoma namba za mtihaniwa ktk majibu au matokeo ya elimu nchini.. Miaka yote hatuna kitu privacy acha mbali malalamiko mengineyo.
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom