Wazalendo Wanapopukutishwa Bila Woga!!

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,244
Hivi inaweza kuwa kweli?

Ukimjumlisha na huyu bwana wa EWURA Wazalendo na Wasema Kweli Wataisha.

1400597359994.jpg 1400597388453.jpg 1400597408317.jpg
Ndugu zangu,
Watanzania wanajiandaa kumzika aliyekuwa
Waziri wa Fedha (Mweka Hazina Mkuu wa
Serikali) marehemu William Mgimwa, maziko
ambayo yatafanyika Jumatatu kijijini kwao
Magunga, mkoani Iringa.
Kumekuwepo na tetesi nyingi kupitia vyombo
vya habari kwamba huenda waziri huyo
mkimya amelishwa sumu. Hakuna
aliyethibitisha madai haya tangu kutokea kifo
hicho Januari Mosi 2014.
Kifo cha Mgimwa kimeingia kwenye mlolongo
wa vifo kadhaa vyenye utata vilivyowahi
kutokea nchini katika kipindi cha miaka 20
iliyopita.
Mawaziri wawili waliopata kuongoza Wizara
ya Fedha nao wanadaiwa kufa katika
mazingira ya kutatanisha, miongoni mwao
akiwa Profesa Kighoma Ally Malima aliyekufa
Julai 16, 1995.
Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA (NRA),
Prof Kighoma alikwenda Makka katika hijja
ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko
aliahidi pindi atakaporudi Tanzania atakuja
kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya
kumaliza hijja alielekea Uingereza na mauti
yakamkuta huko.
Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa
inawezekana kuna FITNA iliyosababisha kifo
chake japokuwa wengine wanasema hakuna
FITNA yoyote.
Steven Kibona, aliyepata kuwa Waziri wa
Fedha enzi za Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
pamoja na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu,
Gilman Rutihinda, nao walikufa vifo vya
utata.
Kuna taarifa zilizodai kwamba, wazalendo
hao walikataa kuchapisha fedha na
kuziingiza kwenye mfumo kwa kutambua
kwamba kufanya hivyo kungeongeza
mfumuko wa bei na ugumu wa maisha
ungeongezeka.
Kibona alipelekwa na aliporejea huko
akaanza kuumwa. Ikaelezwa kwamba
amekula vyakula vya Kihindi ndiyo maana
alikumbwa na tumbo la kuhara kwa sababu
ya ugeni wa chakula. Hakukaa muda mrefu
akafariki dunia.
Rutihinda naye alipata ajali asubuhi tu akiwa
anatoka nyumbani kwake. Taarifa
zilizokuwepo ni kwamba ilikuwa ajali ya
kawaida!
Mwingine ambaye kifo chake kina utata ni
Horace Kolimba. Huyu anajulikana kwa kauli
yake aliyoitoa kwamba CCM haikuwa na dira
wala mwelekeo. Akaitwa Dodoma 'kuhojiwa'.
Lakini Machi 15, 1997 majira ya saa 11 jioni
wakati akijiandaa kutoa maelezo yake,
akadondoka ghafla. Walipompeleka hospitali
ya Mkoa wa Dodoma tayari alikuwa 'wa
jana'.
Hivi, hakuna anayeweza kutoa taarifa rasmi
kuhusiana na vifo hivi vyenye utata au kifo
cha kiongozi yeyote kinapotokea mpaka
tusubiri 'redio mbao'?
Nawasilisha.
 
Hivi hao akina marehemu Mgimwa, Malima, Kibona etc walifanya kitu gani katika Taifa hili cha kupigiwa mfano? Naomba mtu anayefahamu jambo walilofanya hao mawaziri anieleze. Ule UONGO wa kutumia number kwenye NECTA exams, hapa sio mahala pake.
 
Hakika kila roho itaonza mauti, hata wale waganga wa kienyeji wanaouza dawa za kuua binadamu nao kuna siku wanakufa!!! Hata matajiri wa dunia hadi leo wameshindwa kukizuia kifo!!! Iko siku nao wataonza mauti!!!
 
Huu ni ushauri kwa wote: Ikiwa utapata kuhisi kuna kitisho kinakuandama, tumia smart phone yako jirekodi, eleza hali halisi, mfano nani kakutishia, kwa njia gani, kwa nini unatishiwa, halafu iweke youtube. Likitokea la kutokea, kusiwe na maswali mengi. Bora uitwe kichaa ila uokoe maisha yako. Hebu tutumieni technologia kujiokoa.
 
Ukiwa mkweli na muadilifu ndani ya Taifa hili unaeza kujinyonga.
Ndo maana Uwazi na Uwajibikaji havitakiwi.
 
Mbona hujamuweka CHACHA WANGWE au yeye hakuwa mzalendo?

Si ungeanzisha thread ya Marehemu Chacha Wangwe wewe? Buku 7 zinakufanya unaweweseka na kila thread humu.Kamsaidieni mh. Kinana kubaini mizigo mkaiondoa kwenye utendaji, siyo kukaa kwenye keyboard zenu na kuanza kutetea maovu na uzembe unaokithiri kila kukicha.
 
Kigoma Malima angekuwa hai hadi leo tanzania ingekuwa na tatizo la alshabaab
 
Back
Top Bottom