CHAI CHUNGU
JF-Expert Member
- Feb 20, 2012
- 7,113
- 950
ni mwana ccm huyo!mh mrema ndio anaujua ukweli wote.muulizeni yeye!
Kama mtaendelea kutafua hivi viji-sababu visivyo na mshiko mtaendelea kuwa nyuma ki-ELIMU milele. Ninajua ndivyo mnavyodanganywa huko misikitini.
From the horses mouth, mimi nilifanya mitihani wakati huo Waziri wa Elimu akiwa Jackson Makweta, Rais akiwa Julius Nyerere na tulitumia NAMBA katika mitihani yetu.
Sasa hili la kwamba Prof. Kighoma Malima ndiye aliyeleta mfumo na NAMBA kwa wahitimu linatoka wapi?! FYI, wakati huo Kighoma Malima alikuwa Lecturer UDSM akifundisha economics, hata SIASA alikuwa hajaingia. Ingawa sio vizuri kumsema marehemu lakini Prof. Kighoma Malima alikuwa MDINI sana kiasi cha kujenga ka-msikiti pale Wizara ya ELIMU. Sipati picha kama Jackson Makweta angejenga ka-kanisa wizara ya ELIMU sijui kelele zingekuwa je?
Mfumo wa namba za kabla ya Malima ni kuwa ulikuwa na namba na jina na Malima akanzisha kubakisha namba na majina ya mechishwe baadae na namba. Hiyo ndio tofauti.
Baada ya Malima namba na majina zikarudi kama kawa, tena nadhani namba zikabaki kuwa ni serials tu na majina ambayo ni rahisi sana kubagua kwa mfumo uliokuwepo wa kujaza nafasi zilizokuwepo ilikuwa ni rahisi sana ukichukulia kuwa idara za serikali zinaajiri wakatoliki kwa 83%. Kama unabisha hesabu idara uliopo.
sijawahi changia post yenye udini lakini wewe umenifanya nichangie kwa kuwa umeonyesha ni kwa kiwango gani wewe ni mpumbavu au taahira,nani kakuambia kwenye kazi huwa unaulizwa wewe ni mkristo wa thehebu gani? Hata kwenye cv zetu tunaandika dini tu hatuspecify kuwa thehebu gani au nyinyi huwa mnaandika kama ni mwislam unaandika dhehebu kama shia, au answar sunn? Kama umeona kuna wakatoliki wengi wameajiriwa hiyo inatokea automatically kwa sababu zifuatazo.
1. Idadi ya wakatoliki ni wengi tanzania ukilinganisha na makanisa mengine
2. Wakatoliki ndio walioanzisha shule nyingi na ndio wanaongoza kwa kuwa na shule nyingi binafsi na zenye elimu bora wakifuatiwa na walutheri, hvyo idadi kubwa ya wakatoliki walibahatika kwenda shule kutokana na maeneo yao kuwa na shule
nakushauri ukiwa kama mwislam ujue tatizo lenu liko ndani yenu nyinyi wenyewe. Nimekaa Tanga wilaya Mkinga kuanzia pale amboni hadi horohoro hakukuwa na shule hata moja ya sekondari na ni sehemu yenye waislam wengi(wadigo'waduruma,na washirazi),mkisto ni mmoja mmoja tena mhamiaji, shule zimekuja kujengwa na serikali miaka ya 1994 (maramba sec), 1995(zingibari sec) na zote hizo hazina Alevel sasa jiulize jumuia ya Kiislamu ilikuwa wapi muda huo wote badala ya kuwasaidia waislam wenzao kujenga shule?. Maeneo ya wakisto yote yanashule yzilizojengwa na makanisa tangu tu ukisto ulipoingia maeneo hayo na si shule tu bali na zahanati au hospitali. Kuna shule za kikristo zina mpaka miaka 150 tangu kuanzishwa kwake,je waislamu shule zeenu kongwe ziko wapi? Kama sio kujenga misikiti tu halafu leo hii mnakuja kulalamika kuwa mnabaguliwa, acheni hizo amkeni,adui ya mwislam ni mwislam mwezie na si mkisto,mfano bakwata wameuza hata viwanja vyenu. Funguka!
Kama mtaendelea kutafua hivi viji-sababu visivyo na mshiko mtaendelea kuwa nyuma ki-ELIMU milele. Ninajua ndivyo mnavyodanganywa huko misikitini.
From the horses mouth, mimi nilifanya mitihani wakati huo Waziri wa Elimu akiwa Jackson Makweta, Rais akiwa Julius Nyerere na tulitumia NAMBA katika mitihani yetu.
Sasa hili la kwamba Prof. Kighoma Malima ndiye aliyeleta mfumo na NAMBA kwa wahitimu linatoka wapi?! FYI, wakati huo Kighoma Malima alikuwa Lecturer UDSM akifundisha economics, hata SIASA alikuwa hajaingia. Ingawa sio vizuri kumsema marehemu lakini Prof. Kighoma Malima alikuwa MDINI sana kiasi cha kujenga ka-msikiti pale Wizara ya ELIMU. Sipati picha kama Jackson Makweta angejenga ka-kanisa wizara ya ELIMU sijui kelele zingekuwa je?
Na pia Rais kipindi hicho cha kifo chake alikuwa "Mkatoliki" Alhaj Alhasan Mwinyi ambaye "Aliuchukia sana" Uislam. Walitaka kuua uislam.allikua na mpango wa kuweka wazi sababu ya kuwa na gap kubwa la elimu kati ya waislam na wakristo kumbuka huyu alikua waziri wa Elimu aliyeanzisha mfumo wa kutumia namba badala ya majina. mtakatifu nyerere alipopata taarifa akamfuata uingereza then malima akarudi maiti. habari ndio hiyo
mnyika hii itangaze kwa thread yake
Hivi ni wakristo wangapi waliosoma shule za kikristou ni waislam wangapi waliosoma shule za kiislam?mimi nadhani na niko tayari kukosolewa wengi hapa tumesoma shule za serikali,hivyo basi michango yetu hapa isitekwe na mashindano ya nani mwenye shule nyingi,kwani hizo shule hata kama zimejengwa na wakristo si nyerere aliagiza zichukue watu wa madhehebu yote bila kujali dini?hivyo hii hoja ya nani ana shule nyingi then kuitumia kama ndio sababu ya kwanini wengine wanaachwa kielimu sidhani kama itatusaidia kupata majibu bali mtoa hoja kama hii anaweza kushinda ubishani but sio majibu.Tujiulize tatizo liko wapi,kama tatizo liko serikalini basi serikali ilirekebishe kama liko kwa ndugu zetu waislam waislam basi tuwasaidie,kwakuwa hatuwezi kujidanganya tunasonga mbele wakati kuna watu ambao ni sehemu yetu tunawaacha,hilo ni bomu ambalo likija kulipuka haya ma certificates yetu na majoho yetu ya uhitimu yatakua hayana kazi...
Alipojiengua CCM na kuhamia NAREA(NRA), Al-marhumu Prof KIGHOMA ALLY MALIMA alienda Makka katika hijja ya UMRA. Kabla ya kwenda kwake huko aliahidi pindi atakapo rudi Tzania, atakuja kutoa yaliyopo moyoni mwake. Baada ya kumaliza hijja alielekea Uingereza namauti yakamkuta huko. Ilienea katika kila kona ya Tanzania kuwa inawezekana kuna FITNA iliyopelekea kifo chake though wengine wanasema hakuna FITNA yoyote. Anayejua vema suala hili atujuze, KULIKONI??
Siyo lazima wote mnaishia na majina ya "Kalagabaho" muwe na uhusiana wa kindugu, huo ndio msingi wa swali langu wala sina mawazo hasi kumuhusu Adam au Marehemu Ally Malima
Mfumo wa namba ulikuwepo kabla Marehemu Malima hajawa waziri wa elimu. Jaribu kuuliza waliosoma kabla huyu jamaa hajapata huo uwaziri wa elimu watakudhibitishia hili. Pia kama namba ilikuwa sababu mbona bado miaka kibao imepita na trend ni ile ile ya ufaulu?
Adam Malima kasota wapi?kasoma Shaaban Robert,Mzizima, Chuo Kikuu UK, Masters Uk, Kazi BOT then ubunge na Uwaziri?.Binafsi sioni tofauti ya Adam Malima na Ridhwan KIkwete na Abbas Mwinyi,January Makamba n Co.Walewale tu!Msikiti hakujenga bwana walikua wanamsingizia tu,ni sehemu tu ambayo ilikua hata hivyo haitumiki yeye akaitenga kwa ajili ya kufanyia ibada ili asipoteze muda wa kuwatumikia watz na kwenda kufanya ibada kariakoo mchana na kurudi ofisini,akaona awe anafanya ibada zake za saa saba na saa kumi pale kwa dk 15 then anaendelea kuchapa kazi,wengi wanaofanya ibada mara tano kwa siku kwa mujibu wa uislam wanafanya hivyo maofisini mwao,hata dau pale ofisi kwake ikifika saa saba wengine wakienda lunch yeye anajifungia ofisini kwake anachukua mkeka wake anamuomba mungu 15minutes then anarudi kwenye kiti chake na kuendelea na kazi,ni ajabu malima angejenga msikiti si ungepigwa hata picha basi tuuone maana msikiti ni lazima wangekua na watu wengine wanaingia kufanya ibada utajenga msikiti wapeke yako...sema fitna zilikua nyingi,malima wafanyabiashara wakiongozwa na mengi hawakumpenda kabisa sababu alikua anawabana ndio wakaanzisha media kampeni dhidi yake,ndio mana mpaka kesho ADAM MALIMA na mengi ni chui na paka kwa kuwa ule ugomvi ADAM kaurithi na aliapa kulipa kisasi kwa mengi kumchafua babake wakati hakua na mali yeyote kighoma malima,hata familia yake imesota sana,huyu adam mwenyewe kasota sana msimuone hivi sasa,alikua kama chizi kuna kipindi,kabla ya kupewa kibarua na AZIM DEWJI!
Hayo ya namba siyajui kama yalikuwepo huko nyuma kipindi cha nyerere kama kweli yalikuwepo basi kuna kipindi inawezekana yalisitishwa ndio malima kweli akayarejesha,hii nakumbuka kabisa.na kuhusu udini,ni kwa sababu alipofika elimu alijitahidi kuwapa nafasi waislam wasomi waliokua hawajapandishwa vyeo muda mrefu na kwa mara ya kwanza katika historia ya wizara ile toka uhuru akateua ama akawapendekeza wakurugenzi wa elimu ya msingi na sekondari waislam kwa mara ya kwanza narudia toka tupate uhuru hakukuwahi kuwa na waislam kwenye chances hizo kama ilivyokuwa kwa waziri wa wizara hiyo muislam yeye ndio alikua wziri wa kwanza toka uhuru muislam pale.Je tukiweka ushabiki pembeni na kufuata haki malima pale alikua na kosa kama kweli hao waislam walikua na sifa?mimi nadhani kama walikua na sifa na hawajapandishwa vyeo muda mrefu mtu yeyote mpenda haki asingefanya tofauti na malima.Tuache jazba na ushabiki kupita kiasi.
Ukiongelea suala la Kighama Ally Malima kabla ya kifo chake alikuwa Waziri wa fedha na ndiye sababu ya THB (Bank ya nyumba) kufilisiwa.Mkewe wa kwanza alikuwa Mkatoliki na aliitwa Isabella kabila Mhehe.Alibadili dini siku chache kabla ya kifo chake. Tuangalie ukweli wa mambo je ni kweli watoto wakiislamu hawakupewa nafasi? Nimesoma Korogwe Secondary miaka ya 1980 na asilimia kubwa ya watoto walitoka Handeni wengi wakiwa waislamu,karibu nusu ya wasichana hao waliona shule inawapotezea muda kwani wanawake wanaishia kuolewa tu,na umuhimu wa kusoma hwakuuona,hata ukikaa naye kwenye group moja aliona unamsumbua tu.Wakulaumiwa ni wazazi na watoto wenyewe wala siyo Mwl.Nyerere wala waalimu waliowafundisha. Tuongee ukweli tusiyumbishe makosa wazazi wa watoto hao ndio wakulaumiwa. Hili sijaambiwa nimeona mwenyewe kwa macho na kusikia kwa masikio yangu sababu nimesoma nao darasa moja.
Adam Malima kasota wapi?kasoma Shaaban Robert,Mzizima, Chuo Kikuu UK, Masters Uk, Kazi BOT then ubunge na Uwaziri?.Binafsi sioni tofauti ya Adam Malima na Ridhwan KIkwete na Abbas Mwinyi,January Makamba n Co.Walewale tu!Msikiti hakujenga bwana walikua wanamsingizia tu,ni sehemu tu ambayo ilikua hata hivyo haitumiki yeye akaitenga kwa ajili ya kufanyia ibada ili asipoteze muda wa kuwatumikia watz na kwenda kufanya ibada kariakoo mchana na kurudi ofisini,akaona awe anafanya ibada zake za saa saba na saa kumi pale kwa dk 15 then anaendelea kuchapa kazi,wengi wanaofanya ibada mara tano kwa siku kwa mujibu wa uislam wanafanya hivyo maofisini mwao,hata dau pale ofisi kwake ikifika saa saba wengine wakienda lunch yeye anajifungia ofisini kwake anachukua mkeka wake anamuomba mungu 15minutes then anarudi kwenye kiti chake na kuendelea na kazi,ni ajabu malima angejenga msikiti si ungepigwa hata picha basi tuuone maana msikiti ni lazima wangekua na watu wengine wanaingia kufanya ibada utajenga msikiti wapeke yako...sema fitna zilikua nyingi,malima wafanyabiashara wakiongozwa na mengi hawakumpenda kabisa sababu alikua anawabana ndio wakaanzisha media kampeni dhidi yake,ndio mana mpaka kesho ADAM MALIMA na mengi ni chui na paka kwa kuwa ule ugomvi ADAM kaurithi na aliapa kulipa kisasi kwa mengi kumchafua babake wakati hakua na mali yeyote kighoma malima,hata familia yake imesota sana,huyu adam mwenyewe kasota sana msimuone hivi sasa,alikua kama chizi kuna kipindi,kabla ya kupewa kibarua na AZIM DEWJI!
Hayo ya namba siyajui kama yalikuwepo huko nyuma kipindi cha nyerere kama kweli yalikuwepo basi kuna kipindi inawezekana yalisitishwa ndio malima kweli akayarejesha,hii nakumbuka kabisa.na kuhusu udini,ni kwa sababu alipofika elimu alijitahidi kuwapa nafasi waislam wasomi waliokua hawajapandishwa vyeo muda mrefu na kwa mara ya kwanza katika historia ya wizara ile toka uhuru akateua ama akawapendekeza wakurugenzi wa elimu ya msingi na sekondari waislam kwa mara ya kwanza narudia toka tupate uhuru hakukuwahi kuwa na waislam kwenye chances hizo kama ilivyokuwa kwa waziri wa wizara hiyo muislam yeye ndio alikua wziri wa kwanza toka uhuru muislam pale.Je tukiweka ushabiki pembeni na kufuata haki malima pale alikua na kosa kama kweli hao waislam walikua na sifa?mimi nadhani kama walikua na sifa na hawajapandishwa vyeo muda mrefu mtu yeyote mpenda haki asingefanya tofauti na malima.Tuache jazba na ushabiki kupita kiasi.
trend gani na wewe.hivi kwanza hao wasomi sana wa kikristo wapogo wapi?kuna kina lipumba,shivji,safari,bilali,haroub e.t.c.
Ukiacha profesa lwaitama na kingereza chake cha la tatu hivi kuna profesa ama dr gani christian na kwanini hawasikiki?