Ukweli wa Handeni kuhusu wanachama waliokihama CHADEMA

Ukweli wa Handeni kuhusu wanachama waliokihama CHADEMA

Taarifa zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya magezeti (Uhuru, Jambo leo, na Majira). Kuhusu kuhama kwa viongozi na wanachama wa chadema na hivyo kupelekea kufungwa kwa ofisi ya Chadema wilaya ya Handeni sio za kweli bali za kupikwa.

Mtakumbuka kuwa imekuwa kawaida ya ccm kusema na kuzusha uongo ili kuendelea kuhadaa watu kwa manufaa ya siasa nyepesi ili kukwepa kujibu au kutatua mambo mazito yanayo kabili jamii na taifa kwa ujumla.

UKWELI NI UPI.

1. Shabani Ngido aliyetajwa kama katibu hakuwa katibu wala mwanachama wa Chadema, katibu halali wa Chadema wa wilaya ya Handeni anaitwa Ramia Ibrahimu Kisalazo anaishi Mkata umbali wa zaidi ya kilometa 20 kutoka Handeni mjini. Huyo Shabani Ngido alikuwa mwanachama wa ADC hakuwahi kuwa mwanachama wa Chadema.

2. Ni kweli mwenyekiti wa wilaya Bwana Lucas Elisa Selemani amehamia ccm kwa sababu anazojijua yeye moja kubwa ikiwa ni pamoja na kutishiwa kuchomewa tena nyumba. Alisha chomewa nyumba mara ya kwanza na wafuasi wa CCM.

3. Idadi ya wanachama zaidi ya 300 iliyo tolewa kuwa wamehama Chadema sio ya kweli na imejaa takwimu za uwongo. Wanachama walio kihama Chadema na kuhamia ccm haizidi 10, miongoni mwa hao kuna aliyetajwa kuwa alikuwa mwenyekiti wa Kabuku, hakuwa mwenyekiti bali mwanachama wa kawaida.

4. Baadhi ya wanachama wa ccm walipewa kadi bandia ili watakapo zirudisha ijenge taswira kuwa wanahandeni wameanza kuikataa Chadema, hili limefanyika kwenye ziara nyingi za mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya ccm. Mfano ukiwa wilaya ya Hai ambako kadi na walioitwa wanachama wa Chadema zaidi 300 walitajwa kuwa wamerudisha kadi na kurejea ccm wakati ilikuwa ni uwongo.

5. Ccm walidiriki kununua bendera za chadema kati ya shilingi 20000 na 30000 ili zisipepe kwenye maeneo ambayo Bulembo alikuwa anapita au kwenda kufanya mikutano na kushindwa kujali na kutatua shida ya maji inayo ikumbuka wilaya ya Handeni kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

Mwisho.

CCM waache kufanya siasa nyepesi zenye ghiriba na kuhadaa wananchi, ni wakati wa wanahandeni kuungana pamoja kuendelea kufanya mabadiliko ya kukataa chama chenye serikali iliyoshindwa kuleta ya huduma ya maji.

Imetolewa na Mashuve Aroni

Mwenyekiti wa BAVICHA TANGA

0756 923 945
Kuna mtu wa Handeni aliniambia kuwa huyu Athumani Ngido alikuwa Katibu wa Chadema wa Wilaya ila mwaka jana alisimamishwa kwa utendaji wake duni na akaamua kuhamia chama kipya cha ADC mwanzoni mwa mwaka huu na ndio sasa kaamua kwenda CCM. Hili likoje Mkuu?
 
Namfahamu vizuri sana Bulembo , uwezo wake ni mdogo mno, hawezi kufunga ofisi ya mtu yeyote .

Bulembo alishindwa udiwani na kijana wa chadema wa kata ya kijitonyama anayeitwa uloleulole nashangaa mtu aliyeshindwa udiwani kupewa jumuiya ya wazazi ana achwa na chama chake asambaze hadaa na uwongo! Jumuiya gani inayoendeshwa na mzazi aliyeshindwa na muongo?
 
Hivi hata kiswahili huwa kinakupa taabu kuelewa.!? nilijua ugonjwa wako ni Kiingereza tu.
Teh teh teh! Kwa hiyo hii ndiyo itasaidia Chadema isikimbiwe Handeni!
 
Siasa bana, mmmmmmh...ngoja nikasome theory za karl marx, nampenda sana, mwanccm yeyote naamini hawezi kumpenda huyu jamaa...
 
Wewe nani amekuambia ccm inaitaji propaganda iendelee kuwepo?

Mwenyekiti wa C.C.M alishawahi kvamka wazi kua kitengo cha propaganda ni muhimu sana kwa uhai wa chama...sasa wewe unapingana nae?
 
Mfa maji ahachi kutapatapa, kama zilikuwa za uongo ungewaacha wajindanganye wenyewe? Kulikuwa hamna haja ya kutapatapa huku jf

Ila ujue bibi yangu kule kijiji cha milanzi -Sumbawanga hawezi kujua kama ni za kupika au laa ila akisikia zimekanushwa ataelewa ukweli... hicho unachokisema ni sawa na mwalimu akikuuliza swali darasani eti hautamjibu kwa sababu jibu unalo...atajuaje kama umemuelewa? Na je uhuru, na watu wa sembe escot( Jambo leo) na waliopokea bahasha za mangula(Majira) kwanini nao wasinge kaa kimya?
 
Kuna mtu wa Handeni aliniambia kuwa huyu Athumani Ngido alikuwa Katibu wa Chadema wa Wilaya ila mwaka jana alisimamishwa kwa utendaji wake duni na akaamua kuhamia chama kipya cha ADC mwanzoni mwa mwaka huu na ndio sasa kaamua kwenda CCM. Hili likoje Mkuu?

Mkuu kwenye bandiko lako hapo juu umekiri kuwa alishafukuzwa kwa utendaji duni na baadae kuhamia ADC. Kwa kauli hiyo tayari huwezi kumhesabu kuwa ni chadema! Huwezi kufukuzwa chadema na kwenda ADC halafu bado ukabaki kuwa Mwanachadema.

Hapo ndio ujiulize ccm walipa ujasiri wa kumtangaza kuwa ni mwanachadema na sio ADC?! Njia ya muongo ni fupi. Wamezoea uwongo!

Wamesahau usia wa baba wa taifa muasisi wa ccm ambayo leo imejaa waongo. Alisema "ili Tanzania iendelee inahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora", kupitia kauli ya baba wa taifa nani anaweza kuthubutu kuwa kwa hili dogo la Handeni lina ashiria siasa safi na uongozi bora?

Sitataja yale mengine ya ufisadi, sembe, upunda wa kina masogange, na ugaidi.
 
Chadema ni chama cha watu flani wenye nia flani na malengo flani. Ni chama hatari kwa mustakabali wa nchi yangu ya Tanzania.

pimbi na harakati zake.....ujinga kitu kibaya sana
 
Ritz basi toa ushuhuda wa ukweli la sivyo hata wewe utakuwa una lalama tu!
Nimesoma malalamiko yako sijaona huo ukweli uliousema kwenye heading.

Unacholalamika sijui ni nini unataka watu wakusaidie nini.

Tutakuamini vipi kwani wewe ni msemaji wa watu wa Handeni.
 
Ccm ni uchafu tuutokomeze wa Tanzania kwa gharama yoyote
 
Ccm ni uchafu tuutokomeze wa Tanzania kwa gharama yoyote
 
Nimesoma malalamiko yako sijaona huo ukweli uliousema kwenye heading.

Unacholalamika sijui ni nini unataka watu wakusaidie nini.

Tutakuamini vipi kwani wewe ni msemaji wa watu wa Handeni.

Hapo kweny RED inamaanisha Haya magazeti yaliyoripoti ni magazeti ya Handeni pamoja na waandishi wake? kwa hiyo kilichoandikwa hapo haujaona sehemu yeyote inayokanusha ile habari ya awali au umeamua KUJIVUA UFAHAMU ndugu?
 
C.D.M for life mimi na familia yangu chama chetu ni chadema.
 
Mimi binafsi kama mwanaCCM simkubali kabisa huyo mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi CCM, Abdallah Bulembo na pia yule 'kuwadi..' wake Le Mutuz(Willium Malecella).
Hao jamaa ni waongo na wazushi sana.

Mkutano wao wa hadhara hauzidi watu Mia mbili halafu hapo hapo wanadai kuna wanaCHADEMA zaidi ya mia tatu wamerudisha kadi na kuhamia CCM!!!
 
Back
Top Bottom